Daah! Kitilya Ateuliwa Kuendelea Kuongoza TRA for 2 More Yrs. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daah! Kitilya Ateuliwa Kuendelea Kuongoza TRA for 2 More Yrs.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngwanakilala, Aug 12, 2011.

 1. Ngwanakilala

  Ngwanakilala JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Rais Jakaya Kikwete amemteua tena Harry Kitillya, kuendelea kuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kipindi kingine cha miaka miwili kuanzia Agosti 2, Mwaka huu.


  Aidha, Rais Kikwete amemteua Benard Mchomvu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo kwa kupindi cha miaka mitatu kuanzia Agosti 2, Mwaka huu. Taarifa hizo zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha nchini Mustafa Mkulo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kwenye sherehe ya kutia saini mkopo uliotolewa na benki ya Stanbic kwa serikali ya Tanzania.

  Mkulo alisema kwamba kazi iliyosalia baada ya Rais kufanya uteuzi wa mwenyekiti wa bodi ya TRA ni kwa yeye kuteua wajumbe watakaoingia kwenye bodi hiyo, kazi ambayo ataifanya hivi karibuni.


  “Kuna wajumbe ambao wanaingia moja kwa moja kwenye bodi hiyo kutokana na nyadhifa zao, kama kwa mfano Gavana wa Benki Kuu (BOT) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Waliosalia nitawateua muda si mrefu.Kwa hiyo naomba kupitia kwenu wanahabari muwataarifu wananchi juu ya uteuzi huo” alisema.

  Chanzo: Nipashe
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi kati ya watanzania milioni 40 na ushee hakuna mtu mwingine anaweza kushika hii nafasi ya ukamishna wa TRA? Kitilya alitakiwa awe amestaafu tangu 2006, lakini wanaongeza muda kila kukicha! Kuna nini hapa?
   
 3. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..issue ni Utendaji kazi mzuri, Uwajibikaji, Ufanisi, Kutanguliza utaifa mbele, na kuzingatia maadili ya kazi. Katika hayo yote niliyotaja, Kitilya is Fit.
  kama bado ana uwezo wa kuyafanya hayo kwa miaka miwili zaidi kwanini asiendelee.
   
 4. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  ALISHAMEZA DOZI YA LOLIONDO HUYU?
   
 5. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,081
  Trophy Points: 280
  nimeipenda avatar yako, vipi unaweza ukafanya msaada kuchapisha posters zake tuzisambaze nchi nzima ili kuwataarifu waTZ juu ya ststus ya nchi yao!?
   
Loading...