Daah, baadhi ya wanawake nyie, ni wauaji kabisa!!!

CHIEFMANGU

JF-Expert Member
Dec 19, 2016
499
736
Ni siku kadhaa zimepita toka niwasimulie mkasa ulionipata kutoka kwa mdada wa ki Iraq,ahsante Mungu hilo lilipita.

Ninajiuliza nimemkosea nini Mungu wangu,kwa haya ninayoyapitia!!!? Kama wiki mbili zilizopita,nilikutana na mwanamke maeneo ya stand ya mabasi Dodoma,alikuwa mchangamfu sana kwa bahati mbaya huwa sina kawaida ya kujichekesha chekesha kwa wadada hasa nisio wafahamu.
Dada huyu alinichangamkia kupita maelezo nikajiuliza kunani anichangamkie namna hii!!! cha jabu alikuwa akiniita majina yangu,hapo kidogo nikapata ujasiri wa kuongea naye,akajitambulisha pale kumbe ni mtu wa kwetu Mbeya huko,na anatokea kijiji jirani na kwetu,kaka yake nilisoma naye,(baada ya kunikumbusha,nikagundua ni kweli).

Baada ya kufahamiana,tukapanda gari moja (bus)kuelekea Morogoro (ndiko ninakoishi,yeye aliniambia anaishi Kilosa,ni Nurse huko).Tukiwa kwenye gari tuliongea mengi kuhusu kwetu Mbeya,na mwishowe tukabadilishana namba,tulipofika Dumila alishuka,mimi naikaendelea na safari kurudi Morogoro.

Alinitafuta mara kwa mara,akinijulia hali,namimi kadhalika nilimtafuta mara kadhaa kumjulia hali,baadaye aliniuliza maswali kadhaa ya kichokozi,kama kutaka kujua endapo nimeoa au lah,nikamdanganya kuwa nimeoa,juzi aliniambia leo ana safari ya kuja Morogoro mjini,nikamkaribisha.

Leo majira ya saa nne alikuwa safarini kuja Moro,namimi pasipo kuwa na shaka yoyote,nimeenda kumpokea kama ndugu yangu,nimemkaribisha kwangu alipofika na kukuta nipo mwenyewe ameshangaa sana.

Baadaye nikwambia twende tukale kwa kuwa mimi kwangu napika lakini mara chache sana,tukiwa tunakula nikaona macho yake kuna jambo yanaashiria,kwani alikuwa akinitazama macho fulani hivi,nikamuuliza kama ana mahusiano,akaniambia hapana,alishakuwa na mtu lakini walishindana,na sasa yupo single!!

Nikamuuliza kama anaweza kulala leo kwangu,akasita kidogo then akambia "bro ntakuja next week nikae hata siku tatu hivi sio mbaya" nikamsimulia na mkasa ulionipata juu ya muiraq na mama wa mtoto akanipa pole sana,nimemsindikiza akaondoka.akiwa njiani akanitext "nahisi maumivu ya tumbo kama mp hivi" na mimi nikamjibu "Pole sana,una hakika ni mp or chakula nilichokulisha leo?"

Sasa balaa lake ni usiku huu,nikiwa nimekaa zangu nasoma kitabu simu yangu imeita,baada ya kupokea nikasikia sauti ya mwanaume ananiuliza (kwa ustaarabu kabisa)naongea na fulani (anataja jina langu) nikamjibu ndiyo,

YEYE;Unaishi wapi?

MIMI;Kwani wewe ni nani?

YEYE;Wewe nitajie tu,then nitakwambia

MIMI;Siwezi kutoa details zangu ilhali sijui naongea na nani

YEYE;Unamfahamu fulani (anataja jina la yule msichana)

MIMI;Ndiyo namfahamu,kwani vipi?

YEYE;Huyu ni mke wangu,aliniaga anaenda semina,lakini cha ajabu amerudi hapa na sms zako za mapenzi mkizungumzia MP,imekuwaje??

kiukweli nimejikuta napandwa na hasira dhidi ya dada huyu,nimejiuliza kwanini hakuniambia ukweli tuuu,mwenye mke anaonekana haamini kabisa kuwa mkewe sina uhusiano naye wa kimapenzi kutokana na sms alizoziona,mbaya zaidi ni kwamba muda mfupi baadaye jamaa kanipigia simu akiwa anampiga mkewe,namsikia anavyolia na jamaa anamwambia mke wake "nakuua leo,"

Mpaka muda huu sijui ni nini kimeendelea huko,nimekosa amani kabisaa,hata usingizi sipati hata kidogo,ndugu zangu nifanye nini ili nirudi kuwa NORMAL???
 
Wanaawake mnaambiwa tulia na mumeo, unatanga tanga nini..haya unachat chat unatuma sms zenye mashaka na unajua waz ur wife of somebody, ..sasa linabumburuka huko uko hatihati kukatwa mapanga mana mume.uliempata pengine nae majanga.
Pole mkuu hata mimi nsingeweza kulala kwa amani
 
Huyo mwanamke Muuwaji sana.....Kikubwa Akishakupa mrejesho jinsi alivyopata kichapo kama akiwa hair FUTA NAMBA YAKE NA IKIWEZEKANA MCHANE MAKAVU JAMAA YAKE....KUNA MWANAMKE MIMI ALITAKA KUNIPONZA,KASEMA ANAKAA KWA MAMA YAKE MDOGO KUMBE YUPO KWA MUMEWE.....KWENDA KUULIZIA MZIKI WAKE ULIKUWA NOMA
 
1. Toa taarifa kituo cha polisi na uchukue na RB kabisa. Hakuna sababu yoyote inampa ridhaa mwanandoa kumpiga mwenzi wake. Hiyo RB itakusaidia ikiwa mume wake atanuia kukudhuru.
2. Kama una ukaribu na kaka yake uliyesoma naye, unaweza ukampa taarifa pia.
3. Unaweza ukapuuza hayo mawili ya Juu kama nafsi yako itakataa, uvute shuka na ufute kumbukumbu kabisa kama ulishawahi kufahamiana na huyo dada.
 
Rafiki,hawa wanawake wana matatizo kupita kiasi ndugu,yaani usije muamini mwanamke hata kidogo labda mama yako ambae na yeye atakua na migogolo na baba yako,usijaribu pia kuingia kwenye nyumba ya mwanamke anaekwambia anaishi akiwa single,ni hatari kuliko hatari ya kuanguka na gari barabarani.hua wakipata msukosuko kwenye mahusiano kidogo anakimbilia kwa mwanaume mwingine kupunguza stress na anakua nae kwa kudanganya,ni waongo kumzidi hata shetani,andika msg ndefu za kumuelewesha huyo jamaa then ukimaliza kumpa ukweli block namba hyo,na akitumia namba nyingine kukutisha na kukufanya ukose amani nenda katoe taarifa police na hata yeye muweke wazi kabisa kama haelewi na ana kutisha unaenda kumshitaki kwisha
 
Hahahahaaa nakushauri achana na wanawake kwa sasa,yonyesha huna bahati ya wanawake,kila asogeae karibu yako anakuletea janga lake,pole bwana ila huyo achana nae
 
1. Toa taarifa kituo cha polisi na uchukue na RB kabisa. Hakuna sababu yoyote inampa ridhaa mwanandoa kumpiga mwenzi wake. Hiyo RB itakusaidia ikiwa mume wake atanuia kukudhuru.
2. Kama una ukaribu na kaka yake uliyesoma naye, unaweza ukampa taarifa pia.
3. Unaweza ukapuuza hayo mawili ya Juu kama nafsi yako itakataa, uvute shuka na ufute kumbukumbu kabisa kama ulishawahi kufahamiana na huyo dada.
Ahsante kwa ushauri wako mkuu,nimeufanyia kazi asubuhi na mapema kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom