"D0WANS ni genge la mafisadi" asema Sitta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"D0WANS ni genge la mafisadi" asema Sitta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Good Guy, Jan 9, 2011.

 1. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mh.Sitta alitoa maoni yake alipoulizwa na wananchi kuhusu hukumu ya mahakama ya kimataifa ya ICC iliyolitaka shirika la umeme Tanesco kulipa Dowans sh. Bil.185 kutokana na kuvunja mkataba na Dowans 2008 bila ya kufuata utaratibu. Sitta alisema jana "Kuna kila dalili za genge linalohujumu nchi kuandaa mpango wa kutafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015." Ikumbukwe kuwa Shirika hilo la uma liliibuka na mapendekeza ya kununua genereta za kampuni hizo zinazoendeshwa kwa gesi,mapendekezo ambayo bunge la Sitta liliyakataa kwa maelezo kuwa yanakiuka sheria ya manunuzi ya umma,msimamo uliomfanya mkuu wa zamani wa Tanesco Dk Idris Rashid kukubali kwa shingo upande akilaumu wanasiasa kwa kukwamisha masuala ya kitaalam na kusema asilaumiwe kwa matatizo ya umeme baadae. Sitta alizidi kudokeza kuwa "Kuna dalili za genge la watu wenye fedha chafu kujaribu kuandaa mpango wa kuhujumu nchi,hakuna uhalali wowote wa kulipa Dowans sh bil185.Kihasi hicho cha fedha si haki hata kidogo."Sitta ambae aliweka bayana dhamira yake ya kuendelea kupambana na ufisadi mara baada ya kuapishwa kuwa waziri aliendelea kusema."Ni genge ambalo halina huruma na nchi na umaskini wa watanzania na kama likiachiwa lijiimarishe,watanzania wasubiri matatizo makubwa zaidi kutokea mbele.Genge hili limekuwa likiwafanya watanzania kuwa ni wajinga wasioweza kufikiri,ni sababu limeishika nchi,linafikiri siku zote litafanya mambo hovyohovyo na kuangaliwa.Sijui linawatafuta nini watanzania wazalendo?"Mh Sitta alimaliza kwa kusema. "Hii nataka uninukuu vizuri kwamba sasa ni dhahiri kuna genge linalotaka kufanya mchezo mchezo mchafu ambao sisi serikalini tutajitahidi kuuzuia. Watu hawapaswi kuitwisha mzigo Tanesco kwani uamuzi huo uliangalia maslahi ya taifa kuliko baadhi wanavyojaribu kupotosha. Sitta akadokeza "Baadhi ya watuumiwa wa ufisadi nchini wamekuwa wakikwepa kufungua kesi zao mahakama za ndani kwa hofu ya kuumbuka.Dowans ilifungua kesi hiyo ICC ambayo makao yake makuu yako Paris Ufaransa.VIMESEMA VYANZO VYA HABARI.
   
 2. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Go Sitta go.
   
 3. m

  mpingomkavu Member

  #3
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli umenena SITTA, whats the way forward, siyo kila siku unasema kwa kulalamika waeleze watanzania nini cha kufanya? kama kuingia barabarani tuingie ila watoto wabaki majumbani tukifa wote wao wabaki kuwa taifa la kesho
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kaza kamba Mheshimiwa Sitta, bila ya wazee kama ninyi kwenye kabineti hawa vijana wa kina Ngereja watatuflisi.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wanahitajika wazee wengi wenye courage ya hivi...KUsema hivyo tu inatosha sana kuwapa moyo wafuatiliaji maarufu wa maskandali haya, ili waweze kutujuza zaidi...Kubenea Saeed, mnaungwa mkono, kuna watu wengi nyuma yenu.
   
 6. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  BIG UP 6, we are all behind you! GOD Bless Tanzania.
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Bora wapo watu wachache ndani ya serikali wanaokiri kuwa hili dowans ni mtaji wa wahuni. Inabidi waungwe mkono.
   
 8. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Sasa ikiwezekana Sitta ujiuzulu ili kutia msisitizo......hapotutakuelewa..
  Mwakyembe yeye kiimyaaa kalainishwa na kau naibu waziri...kumbe nae mdhaifu namna hii!!!??? Yaani Mwakyembe kelele zote zile kimya!! kweli paradiso watenda wachache mno!
   
 9. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Come on Sitta we need some more info's help us!
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu Sitta has played his part already. Akiwa waziri anayatakiwa kuwa na collective responsibility, amesema wazi kuwa kuna wanyang'anyi nchi hii ambao wanawafanya watanzaia wajinga, amesema sisi tumuitikie.........
   
 11. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tulianzishe kama vp!
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee mbona menoanayo si ang'ate tu?
   
 13. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Anawalia tymin'
   
Loading...