Cyril Ramaphosa, Jacob Zuma na Tanzania!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,169
23,860
Imebidi nikae chini nifikiri juu ya yanayojiri kutoka huko bondeni Afrika Kusini na mustakabali wa uhusiano wetu na hawa wenzetu wa Sauzi.

Nimewalinganisha Cyril Ramaphosa na Jacob Zuma katika kuongza Afrika Kusini na kuwalinganisha uongozi wao na Tanzania kwa ujumla.

Tulikotoka si ndwele lakini lazima tugange yajayo.
Kati ya viongozi wawili wa Sauzi niliowataja ingalau Jacob Zuma anajua kuwa kuwepo kwake pale alipokuwa Rais ni kwa juhudi za waafrika wenzake, wakiwemo waTanzania.
Mugabe aliwahi kusema mzigo mzito Zaidi katika kuikomboa afrika Kusini ulibebwa na Tanzania.
Wapigania uhuru walijengewa makambi, wakapewa passports za Tanzania na kiujumla waliishi kama vile vijana wetu wanavyoishi katika makambi ya JKT au Zaidi, tena kwa miaka au miongo kadhaa.

Zuma aliishi Tanzania.
Ramaphosa hakuwahi kuishi nje ya Afrika Kusini, na namkumbuka miaka ya 70's na 80's alikuwa kijana simple wa kupiga makelele majukwaani.
Mimi namkumbuka vizuri na madevu yake kama Bushiri.

Kuna tetesi kuwa Ramaphosa alifadhiliwa vizuri na makaburu kufika hapo alipo ili asimamie matakwa yao.
Hatushangai leo from a simple guy kawa ni Tajiri mkubwa mwenye makampuni ya biashara.

Mtazamo wa Ramaphosa unalingana sana na mtu aliyefadhiliwa na makaburu.

Kuna clip imeiona wakati wa kampeni yake ya Urais naye ali wahi kulitaja tatizo la wahamiaji walioingia Sauzi kama tatizo la wasauzi.
Mimi sina maneno na kuwachukulia hatua wahamiaji haramu maana hata Tanzania tunao.
Lakini hili la kuwachoma moto, kuwapiga na kuchoma biashara za wahamiaji, wengine ambao ni wahamiaji halali, that's a political crime.

Serikali ya Ramaphosa ingweza kuwa kusanya hao wahamiaji haramu na, kma tunavyofanya Tanzania, na kuwapeleka makwao kistaarabu.

Lakini Ramaphosa si Mtanzania wala si mtu ana uhusiano wa kindugu na watanzania na waafrika wengine, yeye ni mSauzi first.

Serikali yetu ya 60's ili wafadhili waafrika wa Afrika Kusini walipokuwa wanateswa na serikali ya kaburu.
Leo wameshika serikali, na serikali hiyo inakamata Ndege za serikali iliyowakomboa.
Wananchi waafrika wenzao Sauzi wanapigwa au kuteswa na kuuwawa, mpaka unajiuliza , hivi ni hawa binadamu tulikuwa tunakesha JKT na kuimba

"kaburu matata hiya….hiya... Kaburu matata hiya …….hiya...…"
" Kruger naye ….. tutamkata……...Kruger naye tutamkata……."

Was all that in vain?
Mwalimu na Mandea must be turning in their graves.


Kweli tenda wema uende zako!!!!
 
Ramaphosa kwa kweli siyo jembe la ukombozi wa mwafrika.

..Wasouth huwa wanabishana kundi lipi ndilo lililowezesha kupatikana utawala wa walio wengi.

..kuna wanaodai waliokwenda ukimbizini ndiyo waliotoa mchango mkubwa zaidi. Katika kundi hilo wapo wakina Thabo Mbeki, Jacob Zuma,.etc.

..pia lipo kundi linalodai waliobaki nyumbani waliteseka zaidi, na ndio waliopambana mpaka Makaburu wakalegea na kuruhusu utawala wa walio wengi. Kundi hilo lina watu kama Winnie Mandela, Ciryl Ramaphosa, etc etc.
 
Cha muhimu ni kwamba
1. sisi wananchi tuache kuchagua viongozi vilaza
2. Viongozi wanaopata ridhaa ya uongozi wanalazimika kuhakikisha wanaboresha maisha ya raia wa nchi zao ili kuepusha ukimbizi husio wa lazima.
3. Kila taifa la Afrika litambue kwamba lina wajibu wa kuimarisha uchumi wake kwa kupitia rasimali watu na vitu vya ndani ya nchi zao kwa kuvitumia maximally kabla ya kuanza kuruhusu wageni kuja kufanya shughuli ambao wazawa wanaweza kuzifanya.
 
Inawezekana kuwa historia ya harakati za ukombozi imeishafifia na bila shaka imebakia mioyoni mwa wakongwe wachache sana ambao wengi wao wameisha kustaafu, si rahisi kushawishi idumu. Kama ilivyo kwa vijana wa Tanzania kwa sasa ndivyo ilivyo kwa vijana wa sasa wa RSA... ni wachache wanaopenda kijihusisha nayo kwa kuwa kila karne huja na vitabu vyake.

Mwaka nilioingia chuoni ughaibuni, nilikuta wasauzi wanamibia na wamalawi waliokuwa na Pasi za kusafiria za kitanzania maana wakati huo Tanzania ilikuwa ndio Baba na Mama wa nchi za kiafrika kusini mwa jangwa la Sahara. Mawi ya kale hayanuki, kwa hiyo tujipange upya bila kutegemea kulipwa fadhira.
 
Ramaphosa ni bilionea aliefaidika ni mpango wa mandela kuwapa weusi nguvu za uchumi
Alikuwa katibu mkuu wa vyama vya wafanyakazi,anawatishia wazungu migomo anavuta mpunga
 
Serikali ya Tz na Watanzania tunatakiwa kutubu KWA Mungu KWA kosa La kuruhusu kodi zetu na ardhi yetu kutumika kuwasaidia mashetani weusi wa Afrika Kusini kutimiza malengo yao maovu ya kuuondoa utawala hàlali wa Makaburu ambao tulidhani eti ni " utawala wa kibaguzi"
 
South Africa hatukuwasaidia ili waje watulipe fadhila ya kugombania nao vikazi vya hovyo hovyo
Naona leo wasauzi wamepiga mabomu huko misikitini,wanataka kuwawahisha wajomba kule kwny bikra 72.
 
Unajaribu kuandika kitu unachanganya na porojo na uwezo mdogo wa kuelewa
mwisho unaandika porojo tupu

Ni lazima kabisa mjue kuwa serikali ya Africa Kusini HAIHUSIKI na kuzuiwa
kwa ndege ya Tanzania...Africa Kusini mahakama ni HURU..haiingiliwi na serikali

Ndege yetu ilizuiwa na mahakama na ikaachiliwa na mahakama

Kuhusu Tanzania kubeba mzigo wa kuisaidia South Africa..ni lazima
useme tumesaidia kwa kiwango gani msaada wetu ulikuwa na impact kubwa?
tusingewasaidia wasingepata uhuru? nani wengine wakiwasaidia?
unajua nafasi ya Zambia?

je wakimbizi waliokuja Tanzania walikuwa wangapi? waliokwenda nchi zingine je?
sisi tuligharamia kiasi gani kwa bajeti yao nzima ya kupigania uhuru?
je kina Ramaphosa na wananchi wao wanatambua yote hayo?au ni sisi tu tunaojua hilo? kuna mengi mno hayako clear zaidi ya kuongea porojo na ku mix na ukweli
 
Badala mpiganie haki na demokrasia Tanzania mmeng'ang'ana na South Afrika,
Tuombe CIA watusaidie kuua hawa madikteta wetu, maana inaonyesha wenyewe tumeshindwa kuwaondoa.
 
Unajaribu kuandika kitu unachanganya na porojo na uwezo mdogo wa kuelewa
mwisho unaandika porojo tupu

Ni lazima kabisa mjue kuwa serikali ya Africa Kusini HAIHUSIKI na kuzuiwa
kwa ndege ya Tanzania...Africa Kusini mahakama ni HURU..haiingiliwi na serikali

Ndege yetu ilizuiwa na mahakama na ikaachiliwa na mahakama

Kuhusu Tanzania kubeba mzigo wa kuisaidia South Africa..ni lazima
useme tumesaidia kwa kiwango gani msaada wetu ulikuwa na impact kubwa?
tusingewasaidia wasingepata uhuru? nani wengine wakiwasaidia?
unajua nafasi ya Zambia?

je wakimbizi waliokuja Tanzania walikuwa wangapi? waliokwenda nchi zingine je?
sisi tuligharamia kiasi gani kwa bajeti yao nzima ya kupigania uhuru?
je kina Ramaphosa na wananchi wao wanatambua yote hayo?au ni sisi tu tunaojua hilo? kuna mengi mno hayako clear zaidi ya kuongea porojo na ku mix na ukweli
Wazambia pia wanauwawa huko bondeni.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom