Cyprian Musiba: Rais hataki miaka 7 ila sisi tunataka, Bunge lifanye mabadiliko ya Katiba

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mkurugenzi Mkuu wa CZ Information & Media Consultant LTD, Cyprian Majura Nyamagambile amesema kuwa Rais hataki kuongoza miaka saba lakini wao wanataka kwakuwa wana haki ya kutoa maoni yao kama wananchi.



Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amelitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya mabadiliko ya vipengele vya Katiba ili iweze kumuwezesha rais kutawala kwa muda wa miaka saba.

“Rais Dkt. Magufuli alishasema hataki miaka saba. hata juzi karudia tena kwamba hataki lakini sisi tunataka miaka saba, na tunaliomba bunge libadili Katiba,”amesema Nyamagambile

Hata hivyo, ameongeza kuwa Rais Magufuli ni wa mfano wa kuigwa Afrika kwa yale anayoyafanya kwani wengi wameshindwa lakini yeye ameweza.
 
Hawa watu wana familia kweli.?
Yani mke na watoto.?
Mimi kabla sijafanya upuuzi huwa mke wangu ananishangaa kwasbabu kunipinga hawezi,kwakuwa nina akili timamu akinishangaa tu naachana na hicho kitu..

Au wenzetu wameoa ma zombie.??

Inaingiaje akilini mtu anang'ang'aniza kitu kama hiki namna hii.??

Kama wanashida hiyo kweli si wapeleke hayo mambo kwenye vikao vya Ccm kwanza wakakubaliane kisha watoke na kauli moja kama Chama..

Ili sisi wananchi tujue Chama cha mapinduzi kimeamua hiki na kile..
 
Back
Top Bottom