Cybercrime Alert: Vijana watukutu, kuwavalisha barakoa bibi na bwana katika nembo ya taifa (Tanzania Coat of Arms) pia ni kosa la kimtandao. Usijaribu

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Bado sijaona mtanzania aliyefanya kitendo hiki lakini ninatoa tu tahadhari kwa ndugu zangu hawa wa Graphics Designing pamoja na wale wazee wa Photoshop.

Kucheza na nembo za taifa sio jambo nzuri kupitia sanaa ya picha. Barakoa zilivuma sana korona iliposhamiri na kwa mataifa ya kibeberu hakuna sheria za maana kama hizi zinazolinda alama za taifa. Ni viongozi wanaojiamini tu kama Rais Magufuli ndio wanaona umuhimu wa kuwa na sheria za kizalendo kama hizi za kukataza uhalifu mitandaoni.

20 May 2020: Mchekeshaji Idris Sultan anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar na anahojiwa katika Kitengo cha Makosa ya Mtandaoni.

Anashikiliwa baada ya kuwasili Kituoni hapo kufuatia wito wa Polisi na inadaiwa atahamishiwa Polisi Makao Makuu. Oktoba 2019, alikamatwa kwa kuhariri picha ya Rais Magufuli.

ANGALIZO: Kuwavalisha barakoa (Face Coverings) wale bibi na bwana waliopo katika nembo ya taifa (The coat of arms of Tanzania) pia ni kosa la kimtandao.

download.jpg

Yule askari sanamu (Askari Monument) wa pale mtaa wa Samora sijui anaweza akavalishwa hizo barakoa au la? Ngoja wataalam watakuja kufafanua hili zaidi.

Usije ukajaribu upuuzi huu kijana. Baadae usije ukasema kuwa mtanzania mwenzako sikukutaarifu mapema.

Maisha haya yamekuwa ni magumu kwa sasa, kwanini ulipishwe fines kwa mambo ya kizembe kama haya? Pesa unayo wewe au njaa kali tu kama mimi Infantry Soldier?

Zile nenda rudi za wanasheria plus muda utakaoupoteza Polisi na mahakamani ukisema uutumie katika mambo ya maana unaweza ukawa upo mbali kiasi gani?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Infantry Soldier 〜 A True Patriot 〜
 
Hizi ndizo zile 'Sheria kandamizi' ambazo Dr wa degree Saba alizikimbiza bungeni kwa hila ya kudhibiti na kunyima watu Uhuru wa maoni.

Tukiendelea hivi tusitegemee kujikomboa kifikra!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom