mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,480
- 6,833
Cyber espionage ni moja ya njia za kijasusi zinazohusisha ukusanyaji wa taarifa kupitia computer na mtandao kwa ujumla. Ujasusi huu huwezeshwa kupitia programu au virus ambao huwekwa kwenye computer au mfumo wa computer na kuwezesha ukusanyaji wa taarifa kutokea mbali. Katika ulimwengu wa sasa Cyber security ni mchangamoto kubwa sana, matukio ya udukuzi kwa ajili ya ujasusi yamekuwa yakiropotiwa sana. Kama tutakumbuka ni majuzi tu aliyekuwa wakala wa NASA, Edward Swoden alitoa siri kuwa viongozi wengi wengi wa mataifa MARAFIKI wa USA walikuwa wamedukuliwa, jambo hili lilizua mizozo hasa kwa kansela wa Ujerumani bibi Merkel kwa mshangao mkubwa iwe hata MARAFIKI walikuwa wanadukuliwa taarifa zao? Lakini huo ndio ujasusi haijalishi ni RAFIKI kwa sasa au adui kwa sababu huwezi jua baadae kama mtabaki kuwa marafiki au la, kwa hiyo URAFIKI hauzuii UJASUSI kuendelea, kwa nchi nyingine ni sera na sio umauzi wa Rais. Ndio maana huwezi kumlaumu Obama kwa programu ile ya PRISM iliyohusisha udukuzi hadi kwa MARAFIKI zake.
Nije kwenye mifano ya aina hii ya Ujasusi
1. Mwaka 2012 wataalamu wa masula ya usalama Ulaya, walisema kuwa computer kadhaa katika ukanda wa mashariki( nchinza kiarabu, pamoja ma Iran) zilikuwa na virus ambao walikiwa wakifanya kazi ya kutuma taarifa za kimiamala ya fedha na kuathiri mfumo wa udhibiti katika sekta ya viwanda.
2. Katika kitabu cha Dan Raviv kinachoitwa INSIDE ISRAEL SECRETE WARS, anaelezea jinsi mashirika ya kijasusi ya CIA na MOSSAD yalivyokuwa yakihujumu mfumo wa uendeshaji wa mitambo katika kituo cha ukuzaji wa Nyuklia nchi Irankwa kutumia virus waliowekwa kwenye mfumo wa computer. Virus hao walijulikana kwa jina la Stuxnet. Virus hao pia wameripotiwa katika Wizara na sehemu nyingime nyeti zinahusiana na sekta ya mafuta.
Ni wazi teknolojia imechukua nafasi kubwa sana katika suala la ujasusi miaka hii, jinsi ulivyo na teknolojia ndivyo unakuwa na faida japo suala la ukusanyaji wa taarifa kwa kutumia watu( Human Intelligence) linabaki kuwa la umuhimu.
Kwa nchi majirani, washindani ( kibiashara) n.k kujasusiana ni kitu cha kawaida katika harakati za kutafuta ushawishi mkubwa eneo husika au duniani kwa ujumla.
Nadhani hii ni changamoto kwetu, tuzidi kujiboresha ili tuendane na mahitaji ya ulimwengu wa sasa na harakati zetu kuhakikisha tunabaki kuwa BOSI kwenye jumuiya yetu lakini pia jinsi ya kujikinga na kuzuia ( counter espionage)na aina hii ya ujasusi unaoshamiri. Ili kuweza ku counter maana yake uwe na wataalam wenye ujuzi wa ngazi inayoendana na mahitaji na wakati tulio nao.
Copied & Pasted
Karibuni kwa michango zaidi