Cyber crime

blackstone

Senior Member
Aug 11, 2015
147
128
Wakuu ni jinsi gani ya kutambua mtu mnayewasiliana nae kwa email hususani toka nje ya nchi mfano uingereza anataka kukufanyia wizi au utapeli wa mtandao.Mwenye mfano toa!maana kuna jamaa yangu leo kanisimulia amepata rafiki wa kizungu wamekuwa wakiwasiliana zaidi ya siku tatu zimepita sasa ivi anataka amtumie zawadi ya vifaa vyakiteknolojia na zawadi nyingine.hii ipo kweli maana mimi sijamuelewa kabisa!!
 
Njia ya kujua ni hapo atakapokutaka umtumie hela ya kusafirisha hivyo vitu
 
Huyo ni tapeli mkuu Mimi pia ninawasiliana na mtu kama huyo kaniambia ametuma vifaa vya kiteknolojia ikiwemo laptop,simu ya apple na vingine kadhaa pamoja na cash.
Nikamwambia anitumie namba yake anayotumia huko uingereza ili nimkamate kupitia code number kadai hayuko online kwa Sabuni yuko Safari Vietnam.
Tapeli wangu kajitambulisha anaitwa dr Natasha Philip.
Kwa kifupi ni tapeli mwisho atataka utume gharama za kusafirisha hivyo vitu ukimtumia japo buku umeliwa.
Take care
 
  • Thanks
Reactions: PNC

duuh mkuu tushashtuka hawa watu ni matapeli ni hivyo hivyo anapatikana facebook anakuomba urafiki mwenyewe ukukubali anakutumia sms inbox kwamba yuko bize anajiita Dr Meeran Goodness mkiendelea kuwasiliana atajifanya yuko bize mara anataka kukupa zawadi ya laptop mbili iphone camera jiepusheni asee ataanza kukuomba fee ya kusafirisha zawadi toka Senegal jiepusheni wakuu.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
wazungu wamekuwa wanatutapeli kirahisi sababu tunaamini wao hawana shida na wamejitoshekeza hii inapelekea tuamini kwamba wazungu wanajua kila kitu na hawana shida!dada zetu,viongozi wa afrika kusainishwa mikataba feki hadi raia wa kawaida tunatapeliwa kindezi na hawa wazungu!mtu ukiishi na wazungu ndio utajua tabia zao vizuri
 
hivi kwani ukiwasiliana na mtu kwa email toka nchi nyingine hakuna njia ya kujua email uliyotumiwa imetoka nchi gani Chief-Mkwawa msaada hapa.
 
huwa mara nyingi tamaa ndio inafanya watu watapeliwe, sasa mtu anakujua siku tatu tu then akutumie vitu?
 
hivi kwani ukiwasiliana na mtu kwa email toka nchi nyingine hakuna njia ya kujua email uliyotumiwa imetoka nchi gani Chief-Mkwawa msaada hapa.
itategemea na email provider na feature anazotoa, kama anaruhusu utaona kama haruhusu huoni.

mfano kama email ya gmail ndio hio hio hutumika youtube, google plus na maeneo mengi unaweza kuangalia activities zake na kujua alipo huyo mtu
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom