Sio mpenzi sana wa kuanzisha uzi ila nimelazimika kuandika uzi siku ya Leo.Sababu zilizonisukuma kuandika uzi ni kuhusu chalii mmoja hapa kapagawa baada ya kupigiwa simu na kuambiwa aripoti makao makuu kitengo cha cyber kusaidia upepelezi na kuhojiwa,..jamaa anachokumbuka Mara ya mwisho ali-like post ya Mange mwanzo nilidhani ni matapeli ila hali inaonyesha ni kweli japo jamaa anasema alitoa like tu na hakuna mahala alicomment au kupost ,ila itakua alienda further japo sijui
Siku chache nyuma kuna MTU huku mtaani alimtuhumu rais kuwa ana mkono kwenye tukio la Lissu kilichotokea jamaa kachukuliwa na watu wasiojulikana huku mashuhuda wakishuhudia na watu wamemtafuta vituo vyote vya polisi wamemkosa hawajui atakua wapi na imepita mawiki haijulikani yupo hai,kwenye viroba au kafa.
Hii ni mifano michache ila nina mifano 2 mingine ambayo ni worse haifai kuzungumza ya watu kupotea baada ya kushindwa kuzuia midomo yao.
Ndugu zanguni wana JF ,wananchi nawapendeni sana chungeni midomo yenu na tumieni facebook na Instagram vizuri majamaa wapo active ,msi comment na kupost vitu vya kuwashwa washwa kwenye mitandao ya fb na Instagram kwa manufaa yako na familia yako na pia chunga mdomo wako kwenye hadhira ya watu hata kama unawashwa washwa .
Kama watu wanachukuliwa na kupotea hovyo halafu hawaonekani vituoni wanakwenda wapi ? Watu 2 wamepotea kwa kuisema hovyo régime na mashuhuda wameona wakichukuliwa lkn cha kushanga vituo vyote wametafutwa wamekosekana halafu juzi tunaona watu wamefungwa vitambaa vyeusi na wamefungwa kwenye viroba na kudumbukizwa baharini na taarifa hazitolewi mpaka wavuvi walipoamua kutoa taarifa kwenye media ..
Kama hawapo vituoni wanakuwaga wapi ???
Kama hupendi udikteta bora ubaki JF tu
Mkurugenzi hii akili umetoa wapi?watakuwa wamezamia meli kuelekea mamtoni
kitaaMkurugenzi hii akili umetoa wapi?
we acha tu.Haya mambo mzee kipara anayajua lakini anakausha... yetu macho kifo kila mtu kitamkuta