CWT, toeni Tamko udhalilishaji unaofanywa na viongozi "vihiyo" hadhi ya walimu!!

road master

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
2,064
3,011
Chama cha walimu Tanzania imefika mahali kiamke na kuwa "active" sasa!! Kuna ujinga mwingi sana unafanyika dhidi ya wanachama wake lakin hakuna tamko wala kauli ya kukemea inayotolewa!! Mimi sio mwalimu ila nafikiri kuna tatizo ndani ya CWT.

Haiwezekani mwalimu anakatwa sehemu ya mshahara wake lakini pindi anapokutwa na dhihaka kutoka kwa viongozi wapumbavu wasio na weledi na utu chama kisitoe tamko na kulaani udhalilishaji dhidi ya mwanachama husika.

Mfano ni huko mtwara!! Mkurugenzi mkumvua cheo mwalimu mkuu kisa hajachangia pesa kwenye harambee iliyoitishwa na mbunge. Tena mbele ya wananchi? Halafu wananchi wakashangilia!! Hii ni mbaya sana!! Viongoz wapumbavu wasio na busara aliyotuachia magufuli ndio hao!! Nilijisikia vibaya sana kwa kweli.

Yaani hata kama mwalimu alishindwa kujiongeza hata kutoa ahadi hewa lakini hakupaswa kudhalilishwa hivi mbele ya kadamnasi!
 
Walimu, Walimu Tuna Hali Ngumu
Tutazua Kitimtim Mpaka Rais Ajue
 
Kuna viongozi wanahisi Wana madaraka yote na watakaa milele kwenye hivyo vitu

Ikitokea yeye tu kuondolewa anaanza lalamika(kutia huruma kwa watu) Ili Hali yeye hataki watendea wenzake yaliyo mema.
 
Back
Top Bottom