CWT, TAMISEMI, Hazina na Utumishi husikeni hapa

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,049
2,000
Niende moja Kwa moja kwenye hoja.

Mh. Rais wa JMT Madame SSH amakuwa akitoa maelekezo Kwa wizara na idara za serikali ya jinsi ya kutatua kero zinazowakabili wafanyakazi wa Serikali.

Moja ambalo alishalielekeza na kuliidhinishia fedha za malipo ni like kundi la wafanyakazi waliopanda madaraja mwaka 2017 na 2021 na wanadai salary arrears za miaka miwili yaani baada ya kurekebishiwa mshahara mwaka 2019.

Jambo la kusikitisha ni kuwa Kila jambo hili linapoibuliwa utumishi na HAZINA wanatupa mpira TAMISEMI ambao wanadai kuwa wanahakiki na ama wamepeka utumishi na utumishi wantupa mpira HAZINA na HAZINA wanakaa kimywa.

Utendaji wa mtindo huu serikalini hauna afya na unaidhalilisha serikali na kupelekea serikali kupuuzwa Kwa kudaiwa fedha ndogo na kushindwa kuzilipa Kwa wakati.

Hivi wanaoidai Serikali wakifungua shtaka la kudai riba ya fedha hizo halali watakuwa wameikosea adabu?

Nianasihi mawaziri wa TAMISEMI, fedha na utumishi hebu waondoleeni kero hii watumishi Hawa ambao wengi wao ni walimu.

Na CWT iamke kuwatetea walimu badala ya kuchukua michango yao Kila mwezi bila kufanya kazi!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom