CWT Mmethubutu kugoma, Mmeshindwa kesi na Hamsongi mbele katika Mgomo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CWT Mmethubutu kugoma, Mmeshindwa kesi na Hamsongi mbele katika Mgomo!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Emashilla, Aug 3, 2012.

 1. Emashilla

  Emashilla Senior Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MIGOMO KISHA MAHAKAMA ZIKASEMA NI BATILI BADO KUAHIRISHA HAKI SIO SULUHISHO LA MADAI YA WANYONGE

  Hatuwezi kuwalipa Madaktari iweje tuwalipe hawa wana wa wito kama hawataki tunazowapa wanaweza kufanya wanalotaka au tuwafukuze katika zoezi la sensa. Lakini tunawajali na kuwapenda walimu na madaktari. Hivi walimu wanadai mazingira magumu wana mazingira magumu yapi? tuisheni tayari tumepiga marufuku, Sensa tumewapa wao, uchaguzi mdogo na mkubwa bado huwa wanapewa jamani walimu mnataka posho gani hii ya mazingira magumu? Bima ya afya mnapata ingawa mtachangia kidogp kununua dawa kwa marafiki zenu madokta waliogoma kama ninyi lakini tuliwashinda na sasa huduma zinaendelea vizuri na ninyi walimu tumewashinda kwa kishindo kama sera zetu za kishindo rudini shuleni mkawalipe wanafunzi kwa utoro wenu kwa mgomo batili.
  Kweli mimi ninawashangaa Viongozi wa chama cha walimu Tanzania-CWT! Nilitaka kuwaunga mkono, lakini nimepata wazo jipya. Walimu mnapata shikamoo na Good morning Sir/Madam nyingi sana kuliko mtu yeyote kwa siku. Bado hamridhiki tu? Mikopo katika mabenki kwa riba kubwa inawahusu. Mnadai nyongeza ya mishahara na maposho hivi mnataka nini tena jamani? au niwatume huko wauzaji wa bidhaa ili wawakopeshe; niwakate kwenye hizo fedha zenu za kila mwezi?
  Lakini kwa nini jamani walimu wangu! Vumilieni. Wenzenu huku gharama za maisha ni kubwa mno. Sasa tunataka gari zuri na posho ya shilingi 200,000/= kwa masaa machahe tu kila siku. Sisi tukigoma sijui nani atawatungia sheria za kuzuia migomo? Kumbukeni hata maneno ya Mungu yanasema aliyenacho ndiye ataongezewa, lakini asiyenacho atanyang'anywa hicho kidogo alichonacho. Walimu wangu Malipo yenu ni WITO na KUWAJALI WANAFUNZI. Watu mpendwao ndio mtakaoendelea kulipwa kidogo. Mgomo huu kama vile umefika mwisho! Je! mazoezi haya ya Mgomo yatafuatiwa na ule wa TUCTA au Wahadhiri au wanavyuo kudai mikopo toka bodi ya mikopo ya elimu ya juu?

  Mwalimu Pole! Nilikuona ukilia baada ya hukumu ya mahakama divisheni ya kazi.Machozi yako si bure.

  Mungu yupo Upande wenu Walimu wa Tanzania.
   
 2. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kwanza kabisa,
  naomba kumezamaneno yangu yote,
  nilisema walimu hawawezi kugoma,
  wamegoma Shame on me!
   
 3. Emashilla

  Emashilla Senior Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maneno yako ni magumu tafadhali punguza ukali wa maneno yako magumu.Huenda kwenu yupo mwalimu fulani na umemuumiza kwa post yako! Tuwahurumie!
   
 4. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Nakubalina na wewe,
  sikuwa hivi mwanzoni,
  Nimejifunza kwa Ndungai,
  Naibu spika wa Bunge,
  Nilidhani lugha ngumu,
  ndo std ya mazungumzo siku hizi.

   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Walimu wazidi kuitilia ngumu Serikali


  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]MUKOBA ASEMA WATAGOMA HATA BAADA YA LIKIZO, ASKOFU RUWA’ICHI ASEMA TUNAKOELEKEA SIKO
  Waandishi wetu, Dar, mikoani
  CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimetoa tamko kikisema hata kama shule zitafungwa wiki hii, mgomo utaendelea baada ya kufunguliwa endapo Serikali itakuwa haijatimiza madai yao.Tayari mgomo huo umesababisha athari kubwa katika mfumo wa utoaji elimu nchini kuanzia msingi na sekondari na jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema Dar es Salaam kwamba mgomo huo hautaathiriwa na kufungwa kwa shule.

  “Mgomo huu hauna ukomo, ni Serikali tu ndiyo itakayoamua uishe au uendelee. Tukipewa nyongeza tunazotaka utaisha lakini tusipopewa utaendelea milele,” alisema Mukoba. Jana ilikuwa ni siku ya tatu tangu kuanza kwa mgomo huo.

  Alisema mgomo huo ni wa mafanikio makubwa, kwa sababu unahusisha asilimia 95 ya walimu... “Walimu wachache wanaoendelea kwenda shuleni ni waoga, wanafiki wenye kujipendekeza ili wapate vyeo na wanasaliti wenzao wanaodai haki zao,” alisema.

  Rais huyo wa walimu alidai kuwa walimu hao wanaoendelea na kazi ndiyo wanaosababisha vurugu kwenye baadhi ya shule kwa sababu wao wamewaagiza walimu kubaki majumbani.

  “Tunawaagiza walimu waendelee kubaki majumbani kwani wanaweza kusingiziwa na mwajiri kwamba wanawachochea wanafunzi kuandamana na kuharibu vifaa vya shule,” alisema.
  Mukoba alisema mgomo huo ni halali na iwapo walimu waliogoma wataadhibiwa, chama kitafuata taratibu za kisheria kuwatetea wanachama wake.

  Vitisho vya wakuu wa mikoa na wilaya
  Rais huyo ametaka viongozi wa CWT na walimu waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka, waachiliwe mara moja na kufutiwa mashtaka.

  Mukoba alidai kwamba kuna viongozi na walimu ambao wamekamatwa katika Wilaya za Tarime, Rungwe, Kyela na Babati na kwamba kwenye Mikoa ya Pwani, Morogoro na Ruvuma, viongozi wa CWT wametishwa na wakuu wa mikoa na kamati za ulinzi na usalama za mikoa.

  “Wakuu wa mikoa na wilaya waache kutumia madaraka yao kuwatisha walimu kwa kuwa wao siyo waajiri na mgogoro huu unawahusu walimu na waajiri wao,” alisema Mukoba.
  Alisema vitisho vya dola havitasaidia kitu katika mgogoro huo bali, kutimiza madai ya walimu.

  Ruwa’ichi: Tuendako siko
  Katika hatua nyingine, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Mwanza, Thadaeus Ruwa'ichi ameonya kuwa taifa ambalo linachezea elimu halitathaminika popote huku akisema madai ya walimu ni ya msingi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, muda mfupi baada ya kumaliza ibada ya misa takatifu ya maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya Shule ya Msingi Nyakahoja ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki, alisema hakuna taifa ambalo litathaminika duniani kwa kushindwa kuweka elimu kuwa kipaumbele.

  Alisema kwa sasa Tanzania imekuwa ni nchi ya migogoro hali ambayo inaonyesha kuwapo kwa tatizo ambalo limetokana na kuzembea mahali fulani na kuonya kwamba isipowekwa sawa italeta tabu baadaye.
  “Ni hatari taifa likishindwa kutimiza malengo ya kuwatendea haki watoto na familia... Sijapata kusikia popote watoto ambao wamefaulu kwenda sekondari wakati hawajui kusoma wala kuandika, hii ni aibu kwa taifa na fedheha kubwa,” alisema Askofu Ruwa'ichi.

  Akizungumzia msimamo wa kanisa kuhusu mgomo huo wa walimu, alisema Serikali ni lazima ijifunze mazungumzo na maelewano na hayo lazima yazingatie haki na wajibu.

  “Wanachogomea walimu ni masilahi, wanayo haki ya kupata masilahi mazuri yanayowawezesha kumudu maisha. Siyo vyema kuwaona wanapogoma kama ni wakorofi, hapana. Kama tumeona sawa wanasiasa wapate maslahi bora lakini walimu wanatizamwa tu, huku ni kuchezea elimu.”

  “Sisi wakati tunasoma, mwalimu alikuwa mtu wa kuheshimika, lakini sasa tunathubutu kusema kwamba mtu anapofeli mahali kwingine kote tunaona aende kuwa mwalimu. Hili ni lazima tulibadili.”
  Alisema ni vigumu kupata mhandisi bora, askofu mzuri na hata daktari bora iwapo waliofaulu vyema hawatachaguliwa kusomea na kuwa walimu.

  Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye aliwaomba walimu kutumia njia za kisheria kudai madai yao badala ya kugoma kufundisha watoto kwa vile wanaoathirika ni wanafunzi.

  Alisema mgomo huo umeanza wakati mbaya kwa vile kuna wanafunzi ambao wanajiandaa kumaliza elimu ya msingi, jambo ambalo linaweza kuharibu maisha yao ya baadaye na kuwa na athari kubwa kwa jamii.
  Aliwasihi walimu kuangalia majaliwa ya wanafunzi ambao wanatarajia kuhitimu elimu yao ya msingi, kwa kufikiria upya njia ya kudai madai yao kisheria.

  Dar hali bado tete
  Mkoani Dar es Salaam, hali bado ni mbaya kwani walimu katika shule nyingi bado wameendelea na mgomo.
  Katika Manispaa ya Ilala baadhi ya shule za msingi na sekondari zilizoathirika na mgomo huo, za Mnazi Mmoja yenye wanafunzi wa msingi na sekondari, Lumumba na Kidongo Chekundu, Kata ya Jangwani, madarasa yake yalikuwa yamefungwa.

  Waandishi wetu walishuhudia baadhi ya madarasa katika Shule ya Msingi Lumumba yakiwa yamegeuzwa vituo vya kuandikisha Vitambulisho vya Taifa.

  Baadhi ya wanafunzi katika shule hizo walidai wanakosa masomo huku wakiilaumu Serikali kwa kutochukua hatua madhubuti na mapema kutatua suala hilo.

  Walimu nchini wamegoma wakidai nyongeza ya mishahara ya asilimia 100, asilimia 50 ikiwa ni posho kwa wale wanaofundisha masomo ya sayansi, asilimia 50 kwa masomo ya sanaa na kwa walimu wanaofundisha katika mazingira magumu wanataka wawe wanapewa nyongeza ya asilimia 30 ya mshahara.
  Raymond Kamnyoge, Mashamba Badi, Zakhia Abdallah, Elizabeth Edward, Dar na Frederick Katulanda, Mwanza[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Walimu wazidi kuitilia ngumu Serikali
   
 6. Emashilla

  Emashilla Senior Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeeleweka Msalagambwe hata mimi siku moja nilitamani kutumia maneno ya Lusinde kule Arumeru lakini niligundua kuwa si lazima kuwa kama yeye. Lakini walimu wetu wana shughuli kwel kweli. Wakajipange upya maana Baba yao hana uwezo na hawezi kuthubutu kuwalipa madai yao!

  Asante kwa maoni yako mazuri!
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  walimu rudini madarasani mkafundishe madudui majibu watayapata..
   
 8. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,174
  Likes Received: 10,515
  Trophy Points: 280
  Ngumu kumeza..
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Naomba niyaondoe maneno yangu ambao niliwahi kusema WALIMU HAWAWEZI KUGOMA", nilikosea kuwadhania hivyo, sasa nimeamini kuwa kweli walimu wakiamua wanaweza. Samahani sana walimu kwa mimi kuwadhania ndivyo sivyo, I'm sorry!!!! Accept my apologies!!!
   
 10. p

  pembe JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kwa wale wataalamu wa uchumi watujuze kama serikali ingekubal kuwalipa hali ya bajeti ingekuwaje. Hali inakuwa ngumu sana kwa mwananchi anayeshindia mlo mmoja kwa siku huku akisikia kampuni zinazoiuzia TANESCO umeme zinalipwa mamilioni ya pesa kwa siku! Kuna walakini mkubwa ktk uongozi wa nchi hii! Muwezeshe mwananchi naye atainua uchumi wa nchi. Tunawawezesha wageni wanatufilisi na baadae watachukua nchi turudi enzi za kutawaliwa tena. Haki itafutwe kwa gharama yeyote ile ili mradi tunajue uwezekano upo.
   
 11. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Chezea waalimu wewe,huku tunapoenda,watoto wataanza kufundishwa kuwa( kwenye history)" mtu wa kwanza alitokana na mbwa...) acha serikali ichezee waalimu ione.
   
 12. M

  Mfukunyuzi Senior Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  2wajali walimu kwani bila wao hakuna ,wabunge madaktari, mainjinia hata huyo anaesema hana pesa za kuwalipa walimu bila walimu asingefika hapo alipo, mbona nyie mnalipana posho za vikao ambazo ni kazi yenu? Hakika hamuwatendei walimu haki hata kidogo
   
 13. Emashilla

  Emashilla Senior Member

  #13
  Aug 5, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu waalimu msife mioyo kwani nilidhani ninyi hamtoweza kugoma lakini mlichokionesha kweli kinafikisha ujumbe kuwa mwaka 2015 mtasaidia kampeni za kuimaliza CCM na kuwapa M4C kutawala nchi hii. Anzeni kuelimisha wapiga kura kwamba Nguvu ya Umma ipewe mamlaka ya kuongoza nchi kwa sababu mgawanyo wa mapato kwa sasa unapendelea kundi dogo tu. Pia, bendera yao ina jembe na nyundo maana yake ni Chama cha wakulima na Wafanyakazi isipokuwa Washika chaki ambao wao ni watekeleza WITO sio MAPATO.
   
 14. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Baada ya mgomo kubatilishwa,
  walimu wanawalisha sumu
  Wanafunzi as plan B. sijui nani wa
  kulaumiwa, Jk na watu wako mpoo!,
  kazi ipo
  Mwanafunzi:- Please madam
  gfsonwin, how many types of coffee
  do we have in Africa?
  Teacher gfsonwin: - Two
  1:Coffee Annan
  2:Coffee Olomide.
  Chezea mwalimu wewe alieleta
  uhuru TANGANYIKA.
   
 15. DANNFORD

  DANNFORD JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 335
  Likes Received: 201
  Trophy Points: 60
  "hakuna maji,umeme,nyumba,mtandao wa simu unasumbua,hakuna madawat wala vitabu darasan" mmh! bila WITO haufiki!
   
 16. DANNFORD

  DANNFORD JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 335
  Likes Received: 201
  Trophy Points: 60
  bora bomu la atomic, kuliko bomu ambalo walimu watalitega kwa mgomo balidi wa walimu. yan 1+1=11.
   
Loading...