Naomba msaada wako Rais wangu wa CWT.
Tunaomba mtuondolee Katibu Wenu wa Wilaya, amekuwa ni kuwatisha wakuu wa idara husika na MKurugezi baadaye anapote kabisa.
- Mie na walimu wenzangu wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro tuliopata likizo ya Juni mwaka huu hatujalipwa nauli ya likizo mpaka sasa, licha ya kuambiwa nauli hizo zilitoka na kuliwa. Katibu wa CWT wilaya analijuwa hili. Nisaidieni nipate pesa zangu.
- Nilipewa barua ya kupanda daraja baadae nikaambiwa imefutwa serikali haina fedha, Katibu wenu wa wilaya Mr. Maneno mengi analijuwa hili.
- Walibandika majina kwenye mbao za matangazo tunaositahili malipo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhamisho, matibabu, nk. lakini kila baada ya miezi sita au mwaka Katibu wenu wa Wilaya amekuwa anatuandikisha madeni upya.
- Tulihudhuria mafunzo ya sayansi (INSERT) mwezi Septemba mpaka leo hatujalipwa. Tukifuatilia tunaambiwa wakuu wakuu wa shule hawajalipa toka sehemu ya ada. Ukiuliza wakuu wetu wa shule wanadai ada wanatumia kununua chaki,kulipa walimu wanaojitolea kufundisha masomo ya sayansi na vitabu. Wanadai hawajapata fedha ya ruzuku toka serikali kwa mwezi wa Julai, Agosti, Septemba, Oktoba na Novemba. Licha ya kupata taarifa kuwa fedha toka TAMISEMI zimeshatumwa.
Tunaomba mtuondolee Katibu Wenu wa Wilaya, amekuwa ni kuwatisha wakuu wa idara husika na MKurugezi baadaye anapote kabisa.