CWT kupinga uanzishwaji wa bodi ya kitaalamu ya walimu.

Amaizing Mimi

JF-Expert Member
Feb 2, 2019
477
1,065
Bila shaka mpo salama wanajukwaa.

Hivi karibuni katibu wa Chama cha Walimu wilayani kwetu amezunguka kwenye shule za hapa wilayani.amekuwa akipinga uanzishwaji wa bodi ya walimu, nijuavyo mimi CWT ndio inaongoza kumnyonya mwalimu.

Kuna lipi la muhimu kwa mwalimu hadi cwt ijifanye inamtetea mwalimu ilhali wao ndio wanyonyaji wakubwa? CWT itakuwa na nguvu gani baada ya bodi kuanzishwa?

Bodi watakata elfu hamsini kwa mwaka kwa mwalimu wakati CWT inakata walimu kwa asilimia(kuna walimu wanakatwa hadi laki nne kwa mwaka).

kwanini CWT inapinga uanzishwaji wa bodi ilhali inaonekana kuwa na makato madogo kuliko cwt?Au bodi ikianzishwa cwt itafutwa?
 
Japo sio mwalimu lakini uanzishwaji wa bodi utaongeza heshima kwa walimu. Kwanini mainjinia wana bodi nie msiwe nayo? Madokta, wanasheria nao wana bodi vipi nyie?

Nnachoona hapo na cwt wanatetea ulaji wao maana wanajua bodi ikianzishwa ugali wao utapungua kama sio kutoweka kabisa.
 
Heshima ni pesa hizo tatataka nyingine ni takataka tu zisizo msaidia mwalimu wala kuinua ufaulu kwa mwanafunzi. Walimu walipwe vizuri na sio kuongezewa mizigo lukuki.
 
Heshima ni pesa hizo tatataka nyingine ni takataka tu zisizo msaidia mwalimu wala kuinua ufaulu kwa mwanafunzi. Walimu walipwe vizuri na sio kuongezewa mizigo lukuki.
Sasa makato ya 50k kwa mwaka au kukatwa kila mwezi mfano 10k kipi bora?
 
Wakimaliza hapo ianzishwe Proffesional body ya ku certify wanasiasa.
 
Sasa makato ya 50k kwa mwaka au kukatwa kila mwezi mfano 10k kipi bora?
Vyote utakatwa kwasababu uwepo wa bodi hauhalalishi 10k kuondolewa. Pia kuna ishu nyimgi sana humo kuhuisha leseni mwalimu kujigharamia gjarama za semina n.k
 
Back
Top Bottom