CWT imempa siku 14 , Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri awe amewalipa walimu wastaafu

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,507
Chama cha Walimu Tanzania (CWT ) wilaya ya Meatu kimempa siku 14 , mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Meatu awe amewalipa walimu wastaafu nauli na fedha za kusafirishia mizigo yao kurejea makwao kwani tayari wameshafukuzwa katika nyumba ambazo walikuwa wakiishi wakati wa utumishi wao , asipofanya hivyo ndani ya siku hizo wataipeleka mizigo yao na kuikabidhi ofisini kwake.

Aidha wamempa wiki mbili meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa shinyanga kuwapatia bima zao ambazo tayari zimeshaiva na kwani ni haki yao ya msingi.

Hayo yamesemwa na katibu wa cwt wilaya ya meatu james msimba ngíombe wakati wa hafla ya kuwaaga walimu wastaafu 20 wa mwaka 2015 na 2016 na kuwapa mkono wa kheri .

Amesema kuwa walimu wastaafu wamekuwa wakidahalilishwa na waajiri wao pale wanaposhindwa kuwapa malipo na nauli ya kufunga mizigo ya kurudi makwao ,wengi wamefukuzwa katika nyumba walizokuwa wakiishi ,hivyo wamemuomba mkurugenzi atekeleza malipo yao kabla ya walimu hao kuanza kuhesabu fedha za kujikimu za kila siku.

Akizungumza katika hafla hiyo katibu wa cwt mkoa wa simiyu said mselem amesema kuwa kustaafu sio mwisho wa maisha bali ni mwanzo wa maisha mazuri ,hivyo amewaasa kabla ya kupata hundi zao ni vema wakaiweka fedha hiyo katika akaunti na kufikiria mradi wa uzalishaji ili fedha iweze kupata mzunguko huku akiwasisitiza kuwekeza hisa katika benki ya walimu.

Chanzo: Channel 10
 
Cwt ipi? Isije kuwa ni chama cha wanawake Tanzania maana chama cha walimu Tanzania hakina uwezo wa kufanya lolote huwa wana matamko yasiyo na mafanikio na hawana msaada wowote kwa walimu... sasa kama tamko lao ni kuchukua mizigo na kuipeleka ofisini kwa mkurugenzi je hii ndo suluhu la matatizo au maigizo? Nilifikiri wataenda mahakamani kumbe wanaenda kuwadhalilisha walimu kwa kuchukua mizigo yao ambayo kwa hali yao ya maisha utakuta ni vigoda viwili, kitanda cha mbili kwa sita na kagodoro mbavu ya mbwa. POOR CWT
 
Chama cha Walimu Tanzania (CWT ) wilaya ya Meatu kimempa siku 14 , mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Meatu awe amewalipa walimu wastaafu nauli na fedha za kusafirishia mizigo yao kurejea makwao kwani tayari wameshafukuzwa katika nyumba ambazo walikuwa wakiishi wakati wa utumishi wao , asipofanya hivyo ndani ya siku hizo wataipeleka mizigo yao na kuikabidhi ofisini kwake.

Aidha wamempa wiki mbili meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa shinyanga kuwapatia bima zao ambazo tayari zimeshaiva na kwani ni haki yao ya msingi.

Hayo yamesemwa na katibu wa cwt wilaya ya meatu james msimba ngíombe wakati wa hafla ya kuwaaga walimu wastaafu 20 wa mwaka 2015 na 2016 na kuwapa mkono wa kheri .

Amesema kuwa walimu wastaafu wamekuwa wakidahalilishwa na waajiri wao pale wanaposhindwa kuwapa malipo na nauli ya kufunga mizigo ya kurudi makwao ,wengi wamefukuzwa katika nyumba walizokuwa wakiishi ,hivyo wamemuomba mkurugenzi atekeleza malipo yao kabla ya walimu hao kuanza kuhesabu fedha za kujikimu za kila siku.

Akizungumza katika hafla hiyo katibu wa cwt mkoa wa simiyu said mselem amesema kuwa kustaafu sio mwisho wa maisha bali ni mwanzo wa maisha mazuri ,hivyo amewaasa kabla ya kupata hundi zao ni vema wakaiweka fedha hiyo katika akaunti na kufikiria mradi wa uzalishaji ili fedha iweze kupata mzunguko huku akiwasisitiza kuwekeza hisa katika benki ya walimu.

Chanzo: Channel 10
Huo ni mfululizo wa matamko tu yanayosadifu hafla yenyewe ili kuwatia moyo wastaafu. CWT haina meno ya kutafuna fupa hilo hasa kwa mda huo ulionadiwa.
 
Angesema kabisa kwamba hatua ambazo atachukua kama wasipolipwa maana sioni uwezekano wa kulipwa.
 
Hii c serikali ya kufanya maamuzi kwa kushinikizwa...ukurasa huo ulishachanwa na kuchomwa moto, ukujaribu kuipa siku serikali hii unatumbuliwa tu.
 
Angesema kabisa kwamba hatua ambazo atachukua kama wasipolipwa maana sioni uwezekano wa kulipwa.
Amesema atachukua mizigo yao awapeleke ofisini kwa mkurugenzi..., ndo ujue macwt yasivyo na akili
 
Back
Top Bottom