CWT badilisheni utaratibu; tumechoka kofia na tisheti

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,208
2,808
Nadiclare interest kwanza...
Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi (aka fom foo feliya). Nina mwaka wa tatu kazini sasa

Twende kwenye hoja yangu...
Imezoeleka kwamba kila mwaka walimu tunapatiwa tshirt na kapelo kutoka CWT (chama cha walimu Tanzania).

Nimejaribu kuuliza sana hili jambo kwanini iwe ni hivyo tu kila mwaka ila sijapatiwa majibu ya maana. Binafsi huwa napokea (nachukua) hivyo vitu kwajili tu ya kupunguza au kufidia hasara ninayoipata kupitia 2% lakini siyo kwamba nafurahia

Hatukatai kwamba utaratibu wa kutoa tshirt na kapelo unatumika sehemu nyingi ila tunachotaka mfanye mabadiliko.

Kwani mkiamua mwaka mwingine kutoa hata viatu au masweta au mashati hayavaliki? Au mkaamua kuwatolea dada zetu khanga wavae kwani kuna shida gani? Kila mwaka ni kapelo na kifom siksi kisicho hata na ubora ni udhalilishaji huo.

Ccm wamejiongeza siku hizi wenzenu wana mpaka kanzu akina tito wanavaa, wana khanga zisizo na idadi mtaani na vitu kedekede kwani nyinyi mnakwama wapi mbona wote ni vyama?

Kibaya kabisa mnatupa mavazi ambayo hata kazini tukiingia nayo tunaforoshwa sasa sijui mnakusudia tukayavae wapi?

Tisheti na kapelo kwangu zimekosa mvuto nikiwa nimepokea mara mbili tu sasa najiuliza vipi hawa wenzangu waliopokea zaidi ya mara kumi?

Yaani tisheti na kapelo hizo...
1.Mbaya kimwonekano (nimefuatilia labda zile za kijivu tu ndo nzuri zilikuwa za 2014 kama sikosei)

2.hazina ubora hata kidogo

3.hakuna vipimo ni kukadiriana tu (tena kama sisi wa maporini ndo kabisaa ikikufika wameshachagua chagua huko)

4.hazina tija kazini (labda kwenye meimosi kwa hao walio mijini- lakini sisi wengine hata hatuoni umuhimu wake maana ukikutwa umevaa kazini kesi yako ni kubwa kuliko aliyemvua raisi nguo hadharani)

5.zina unyonyaji ndani yake (nakatwa 2% ya mshahara kwa mwezi lakini napewa kitisheti kamoja na kikapelo kimoja kwa mwaka)

6.zinakuwa kama kulazimishwa (kukatwa hela ni lazima sawa tumekubali lakini sasa kwanini nisiwekewe options hapo kwenye kufaidi matunda ya kile nilichokatwA)
 
Ngoja wadau waangalie namna ya kuweka riba kwenye hayo makato ya 2%, muda si mrefu wataanza kupeleka gawio kwa kiranja mkuu🤣
 
Unataka Ubora gani, kikawaida hizo unavaa kwenye tukio baada ya hapo hazina kazi, tatizo mnataka ndo ziwe za kutokea, Umasikini ni mbaya mno jamani, Hawatengenezi hizo Tshirt na Kofia ziwe za kudumu ni za One day event, nyie ndo mnalazimisha ziwe za kutokea kwa sababu ya Umasikini
 
Punguza ukali wa maneno mkuu..
 
Unataka Ubora gani, kikawaida hizo unavaa kwenye tukio baada ya hapo hazina kazi, tatizo mnataka ndo ziwe za kutokea, Umasikini ni mbaya mno jamani, Hawatengenezi hizo Tshirt na Kofia ziwe za kudumu ni za One day event, nyie ndo mnalazimisha ziwe za kutokea kwa sababu ya Umasikini
ila kweli
 
Back
Top Bottom