CV za Wabunge: Hii inawezekana au mie sielewi mifumo ya Elimu ya Tanzania?

Zinedine

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
1,187
694
Huu ni mfano wa taarifa zisizoeleweka katika website ya Bunge ambapo mbunge huyu (Mheshimiwa) anaonyesha alijiunga na masomo ya shahada ya uzamili MBA mwaka 1988 mara tu alipomaliza High School 1987. Je jambo linalowezekana katika mfumo wetu wa elimu Tanzania au? Aidha ieleweke kwamba sina nia ya ku-question elimu ya Mheshimiwa huyu isipokuwa nia yangu ni kuelewa juu ya uwezekano huo na wahusika wa website ya Bunge wapitie website yao na kuondoa sintofahamu zilizopo kwenye website yao ambazo zinaonyesha makosa mengi ya taarifa za waheshimiwa.
Member of Parliament CV

GENERAL
SalutationHonourable
First Name: Sinkamba
Middle Name:Josephat
Last Name:Kandege
Member Type:Constituency Member
Constituent:Kalambo
Political Party:CCM
Office Location:Box 134, Sumbawanga
Office Phone: +255 784 271944/+255 754 271944
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail: jkandege@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 6 June 1964
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start DateEnd DateLevel
Arusha Institute of AccountancyCPA20002003DIPLOMA
Dar Es Salaam School of AccountancyMBA19881990MASTERS DEGREE
Usagara Secondary SchoolA-Level Education19851987HIGH SCHOOL
Ifunda Secondary SchoolO-Level Education19811984SECONDARY
Mwimbi Primary SchoolPrimary Education19741980PRIMARY
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From To
The Parliament of TanzaniaMember - Kalambo Constituency20102015
Agriculture and Food SecurityZonal Accountant19962010
Biashara Consumer Services (BCS)Accountant19951995
Ministry of Science and TechnologyAccountant19941995
Ministry of LabourAccountant19931994
Ministry of Labour (VETA)Accountant19911993
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/LocationPositionFromTo
Chama Cha Mapinduzi, CCMMember - National Executive Committee2008
Chama Cha Mapinduzi, CCMMember - District General Council-
Chama Cha Mapinduzi, CCMMember - Regional Parent Association

Source: Parliament of Tanzania
 
CPA ya Diploma level ?????
Huwa najiuliza suala la CV hata kama limekosewa ina maana ilishindikana kufanya masahihisho kwa kipindi chote cha miaka mitatu au nane walichokaa bungeni.Hizi CV za ujanja ujanja...
 
Makosa madogo madogo tu hayo, nadhani ofisi ya katibu wa bunge imehusika nayo.
 
CPA diploma ndio iko vp?elimu yangu ni ndogo nieleweshen tafadhal!
 
Sasa hii nayo kali, MBA baada tu ya Form Six, there after CPA-Diploma, inatisha kwa kweli.
 
Kama angekuwa amesomea UFUNDI MCHUNDO (FTC-Full Techinician Certificate) zamani na kwenda kusoma URUSI tungeweza kumuelewa maana nchi kama URUSI huwa zinaangalia na course contents ya ulichokisoma huko ulikotoka lakini katika proffessional course na lakini sio FORM SIX .Mfano angalia Elimu ya Principal wa Arusha Techincal College Eng. Dr. R. J. Masika



PhD (Structural Eng) (Hungary), MSc. Eng (Hungary), FTC (Civil Eng.) (DT

C), C.Eng (T).



Dr. R. J. Masika is a Consulting and Licensed Engineer and the Principal of Arusha Technical College.

Huyu Mheshimiwa ni kichwa kizuri tu.
 
Mnashangaa nini sasa,kwani mliambiwa bongo lazima ukae darasani ili upate cheti?au kwa vile nyie mko nje ya "mfumo"?au kwa vile nyie hamna hela ya kununua nanihii pale nanihii!yaangalie,umbea tuuuu!
 
They say the best times of one's life are the college and bachelor years. College years for the obvious reasons; lots of activity, freedom, and access to nearly everything. You can get away with anything, including pulling off the sign post of a bar and grill from the roadside and hanging it from your hostel window. You grow up, make friends, get into fights, and learn the things that matter in life.

Bachelorhood is breaking-out time. Life takes shape as you shake off the carelessness of your college days and train your sights on money and the need to stabilise. While Alexander the Great went about trying to conquer the world, a young bachelor, since there is no more world to conquer and needs more time to conquer the office, will have to find an alternative. The reason is simple; a man ought to conquer some place... or something.
 
Sitaki kumtetea, lakini hii kitu inawezekana kama alipitia mlolongo ufuatao (though bado nina mashaka kidogo) kama alimaliza Form 6 kama inavyoonekana kwenye hiyo CV yake, inawezekana alikua akifanya mitihani ya Board ya Uhasibu NBAA, yawezekana aliaanzia na ATEC ii ya wakati huo (kama alikua na principles 2 za A-level) then aka endelea na P-i hadi P iv kwa hiyo miaka ya 90 hadi 2002 kabla mzee Reginald Mengi hajaachia uenyekiti wa hiyo Board, P-iv ya wakati huo ndio ilikua CPA yenyewe, so inawezekana, kumbukeni pia, CPA ndio cheti cha juu kabisa kwa Uhasibu hapa nchini, miaka hiyo pia uchakachuaji haukuwepo sana kwenye ile Board, so i think the man with his CV is correct. Labda watu wa NBAA, najua wapo humu pia, wanaweza kututhibitishia kama kweli bwn mkubwa huyu anamiliki hicho cheti.
 
Mkuu,
Huu mfano wako una makosa. Hii ya Eastern aeurope ilikuwa hata kwa mtu wa A-level. Unasoma miaka 6 kusotea hiyo masters ambayo ina maana inaunganisha pamoja first degree na Masters. Kwahiyo japo unaona kama huyo Dr karuka kutoka certificate mpaka Masters ukweli ni kwamba hiyo ni program ya miaka mitano mpaka sita.

Hata UK kwa vijana wenye uwezo na wanaotaka unaweza kupiga masters tokea certificate ila inakuchukua mwaka mmoja zaidi ya wanaosoma bachelor.

Huyu mheshimiwa anaonyesha alikuwa anasoma masters muda ambao alitakiwa kuwa JKT. Haiwezekani; hapo ofisi ya bunge wamekosea au yeye kachakachua.

Kama angekuwa amesomea UFUNDI MCHUNDO (FTC-Full Techinician Certificate) zamani na kwenda kusoma URUSI tungeweza kumuelewa maana nchi kama URUSI huwa zinaangalia na course contents ya ulichokisoma huko ulikotoka lakini katika proffessional course na lakini sio FORM SIX .Mfano angalia Elimu ya Principal wa Arusha Techincal College Eng. Dr. R. J. Masika



PhD (Structural Eng) (Hungary), MSc. Eng (Hungary), FTC (Civil Eng.) (DT

C), C.Eng (T).



Dr. R. J. Masika is a Consulting and Licensed Engineer and the Principal of Arusha Technical College.

Huyu Mheshimiwa ni kichwa kizuri tu.
 
Zinedine kwa nini uwabebeshe mzingo ofisi ya Bunge, wao wanabandika walichopewa na Wabunge. Wabunge ni watu wakubwa, Waheshimiwa na watu wanaotakiwa kuwajibika. Ni wao kila mtu kwa nafasi yake kuangalia taarifa zilizoko kwenye website ya Bunge ambazo ni za wazi kwa watu wote (dunia nzima) kuzihakiki na kurekebishe ili ziwe kweli.
 
Kama ina makosa mwenyewe angeomba yarekebishwe, kama hakufanya hivyo, basi hivyo ndivyo ilivyo!
 
Weka cv yako

Nem: Zinedine M. Zidane
Marito statasi: Married with 4 childish
Education: Lupaso Primary School (std v)
Wakk experence: Tandale kwa Tumbo, Mchuuzi maarufu wa mchele wa Mbeya
Date of Basi: 23-09-1965

Una jengine mkuu, CV yangu hiyo hapo nimeweka.
 
Mimi post yangu nimeweka tahadhari kuwa lengo, si kujua elimu yake ila kuuliza je hili linawezekana kwa mfumo wa elimu wa tanzania. La kama hapana ni typing error, basi wataalam wa website ya bunge wapitie na ku-edit, au nayo kupitia website yao inataka dokezo la 'sitting allowance' hivyo mpaka zipelekwe na hazina. Website (WWW) si kitu kidogo jamani, ni habari ambayo umeruhusu dunia nzima iangaliwe na itumike, mwekezaji au mtu yeyote anayetaka kwenda nchi husika kwa lengo la kwa mfano kuwekeza huwa anaangalia mfumo mzima wa nchi, (Serikali, elimu, afya, rasilimali watu, uwezo wa kununua, mfumo wa mahakama, bunge na wabunge na aina zake na sifa zao). Hivyo tuwe makini jamani japo kidogo
 
Wabunge wa ccm wengi ni makanjanja. Ona wanavyoshindana kuitana Dr, Kuna ukweli wowote kuwa Daresalaam School of Acountancy ilikuwa inatoa hata degree 1 tu miaka hio?????

Hili ndilo linalotusumbua katika elimu yetu watanzania. Forgery nyingi mno.

Yaani Dip yenyewe kapata 2000-2003 halafu masters 1988. Hii balaa. Waliokuwa wakubwa enzi hizo watupe ukweli kuhusu cheti kilichokuwa kinatolewa pale DSA na AIA miaka inayoonekana hapo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom