CV za Mawaziri Baadhi Hizi hapa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
Na Neville Meena
Jana Rais Jakaya Kikwete alitangaza baraza la mawaziri ambalo linajumuisha mawaziri 29 na naibu mawaziri 15 hivyo jumla yao kuwa 44. Katika safuhii tunakuletea wasifu wa baadhi ya mawaziri ambao wamo katika baraza hilo litakaloapishwa Jumamosi ya wiki hii, Ikulu jijini Dar es Salaam.


1. Jina: Mathias Meinrad Chikawe Malome
Nafasi: Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais – Utawala Bora
Kuzaliwa: 30 May 1951
Jimbo la Ubunge: Nachingwea - CCM (2005-2010) na amechaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa 2010
Nafasi nyingine:
Waziri wa Katiba na Sheria (2006-2008)
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria (2005-2006)

Elimu:
Stashahada wa Uzamili ya Sheria za Kimataifa na Maendeleo (Uholanzi) (1981 -1982)
Stashahada wa Uzamili katika Utawala (Uingereza – 1977 – 1978)
Shahada ya Sheria - LL.B (Hons) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1972 – 1975)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

2. Jina: Stephen Masato Wasira
Nafasi: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu
Kuzaliwa: 1945
Jimbo la Ubunge: Bunda – CCM (2005 – 2010) na amechaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa 2010

Nafasi nyingine
• Waziri: Kilimo na Mifugo (1989 – 1990), Maji (Januari 2006 - Octoba 2006), Kilimo, Chakula na Ushirika (Octoba 2006 - Februari 2008), Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) (Februari 2008 - Mei 2008) na Kilimo, Chakula na Ushirika (Mei 2008 – Novemba 2010).
• Mbunge: Mwibara (1970 – 1975), Bunda (1985 – 1990),(1995 -1996) na (2005 – 2010)
• Naibu Waziri: Wizara ya Kilimo (1972 – 1975), Serikali za Mitaa (1987 – 1989),
• Mkuu wa Mkoa: Mara (1975 – 1982), Pwani (1990 – 1991),
• Waziri mwambata: Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC, Marekani (1982 – 1985)

Elimu
• Shahada ya Uchumi (BA in Economics) Chuo Kikuu cha Washington, DC (Marekani)
• Shahada ya Sayansi ya Siasa (Chuo Kikuu cha Washington, DC (Marekani)
• Shahada za Uzamiri katika Utawala (Masters in Public Administration),Chuo Kikuu cha Washington, DC Marekani.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

3. Jina: Hawa Abdulrahman Ghasia
Nafasi: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Manejimenti ya Utumishi wa Umma Kuzaliwa: 10 Januari 1966
Jimbo la Ubunge: Mtwara Vijijini (2005 – 2010) na amechaguliwa katika uchaguzi mkuu wa 2010.

Nafasi nyingine:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Manejimenti ya Utumishi wa Umma (2006 – 2010)

Elimu:
Shahada ya Uzamiri ya Maendeleo Vijijini (M.A. Rural Development) Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) (2001-2003)
Stashahada ya juu ya Uchumi (1992 1995) Chuo Kikuu cha Mzumbe

Historia ya Ajira
Mkurugenzi Msaidizi na nafasi mbalimbali katika – Halmashauri ya Wilaya ya Masasi (1992 – 2005).
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

4. Jina: Bernard Membe
Nafasi: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Jimbo la Ubunge: Mtama
Kuzaliwa: 9 Novemba 1953
Nafasi nyingine alizowahi kushika:
Waziri: Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (2007- 2010)
Naibu Waziri: Nishati na Madini (2006 - 2007) na Mambo ya Ndani (Januari 2006 – Oktoba 2006)

Historia ya Ajira
1992 - 2000 Mshauri katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ofisi ya Rais – Mchambuzi wa masuala ya ulinzi na usalama
Elimu:
Shahada ya Uzamili ya Uhusiano wa Kimataifa – Chuo Kikuu cha dar es Salaam (1981-1984)
Shahada ya kwanza (BA) (1977 - 1990)
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&



5. Jina: William Vangimembe Lukuvi
Nafasi: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Kuzaliwa: 15 Agosti 1955
Jimbo la Ubunge: Ismani (2005-2010) na amechaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Elimu:
Stashahada ya Sayansi ya siasa, Urusi (Diploma in Political Science – USSR - (1982 – 1983).
Cheti cha Ualimu, Chuo cha Ualimu Tabora (1975)
Cheti cha masuala ya Usalama, (Iringa Training in Defence and Security - 1980)
Mafunzo ya Uongozi (Urusi) - 1985

Nafasi nyingine alizowahi kupata
Mkuu wa Mkoa: Dar es Salaam na Dodoma
Waziri: Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, 2000 – 2005)
Naibu Waziri: Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana (1995 – 2000)
Mkuu wa Wilaya: Bukoba (1994 - 1995)
Chama cha Mapinduzi: Nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM (1984 – 1993).
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++


6. Jina: Mary Michael Nagu
Nafasi: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Jimbo la Ubunge: Hanang 2005- 2010 na amechaguliwa tena kuongoza jimbo hilo katika uchaguzi mkuuwa mwaka huu.
Kuzaliwa: 11 Mei, 1952

Nafasi alizowahi kushika:
Waziri: Viwanda, Biashara na Masoko (2008 – 2010), Katiba na Sheria (2006 – 2008), Ofisi ya Rais – Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto

Elimu:
Udaktari wa falsafa (PhD), Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Washington (2002 -2004)
Masomo ya Utawala (Commonwealth Diploma in General Management (1987)
Stashahada ya Uongozi – Japan (1982 – 1984)
Shahada ya Uzamiri ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (MA Economics) (1979 )
Stashahada ya elimu ya biashara (Milan) 1979
Diploma in Business Education – Milan
1976 1987
Shahada ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1973-1976)

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++


7. Jina: George Huruma Mkuchika
Nafasi: Waziri wan chi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa)
Kuzaliwa: 6 Octoba,1948
Jimbo la Ubunge: Newala (2005 – 2010) na amechaguliwa tena katika uchaguzi wa mwaka huu.

Nafasi nyinginea alizowahi kushika:
Waziri: Habari, Utamaduni na Michezo (2008 – 2010)
Mkuu wa Mkoa (1998 – 2005)
Mkuu wa Wilaya (1983 – 1998)
Kamanda Vita vya Kagera (1970)
Naibu Katibu Mkuu (CCM Tanzania Bara) 2008 - sasa
Pia amewahi kushika nyadhifa nyingine mbalimbali ndani ya CCM (1968 – 2008).

Elimu:
Shahada ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1970 – 1973) Shule ya Sekondari Ilboru (A-Level Education)

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

8. Jina: Mustapha Haidi Mkulo
Nafasi: Waziri wa Fedha na Uchumi
Kuzaliwa: 26 Septemba 1946
Jimbo la Ubunge: Kilosa (2005 – 2010) na pia ameweza kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Nafasi nyinginea alizowahi kushika:
Waziri: Fedha na Uchumi (2008 – 2010)
Naibu Waziri: Fedha (Anayesimamia Sera, 2006 -2008)
Mkurugenzi Mkuu: Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF, 1987 -2000)
Elimu:
Shahada ya Uzamili ya Mashirika ya Maendeleo ya Taifa (MBA) Chuo Kikuu cha Almeda (1985- 1987).

Historia ya Ajira
Mkurugenzi wa Uendeshaji, Shiria la Maendeleo la Taifa (1985)
Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha (1982-1985)
Mkurugenzi wa Mipango na Fedha, NDC (1980-1982)
Mdhibiti wa Fedha NDC (1978-1980).

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

9. Jina: Shamsi Vuai Nahodha
Nafasi: Waziri wa Mambo ya Ndani
Kuzaliwa: 20 Novemba, 1962
Jimbo la Ubunge: Mbunge wa Kuteuliwa

Nafasi nyinginea alizowahi kushika:
Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (2000 – 2010)

Elimu:
Shahada ya kwanza ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(1984 – 1987).
Cheti cha masomo ya lugha, taasisi ya Kiswahili na Lugha za kigeni Zanzibar (1980 – 1984)
Stashahada ya Uzamili katika uhusiano wa kimataifa, Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam (1995 – 1996).
Shahada ya Sheria (LLB), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1999).

Historia ya Ajira
Mkurugenzi wa vipindi vya elimu (televisheni Zanzibar, 1988 – 1991)
Mhariri na Afisa Uhusiano katika Idara ya Habari Maelezo (Zanzibar)

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Jina: Emmanuel John Nchimbi
Nafasi: Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo
Tarehe ya Kuzaliwa: 24 Desemba, 1971
Jimbo la Ubunge: Songea Mjini (2005-2010) na ametetea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu

Nafasi nyinginea alizowahi kushika:
Naibu Waziri: Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (2008 – 2010), Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana (2006-2008) na Habari, Utamaduni na Michezo (Januari 2006 – Oktoba 2006).
Mkuu wa Wilaya: 2003 -2005
Afisa Tawala, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC, 1998 – 2003)

Elimu:
CommonWealth Open University PhD (Management) 2001 2003 PHD
Shahada ya uzamili katika masuala ya fedha na benki (MBA), Chuo Kikuu Mzumbe, (2001 -2003)
Stashahada ya Juu ya Uongozi, Chuo cha Uongozi wa Maendeleo Mzumbe (IDM) (1994- 1997).


Jina: Celina Ompeshi Kombani
Nafasi: Waziri wa Katiba na Sheria
Jimbo la Ubunge: Ulanga Mashariki (2005-2010) na ametetea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Tarehe ya Kuzaliwa: 19 Juni 1959

Nafasi nyingine alizowahi kushika
Waziri: Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) (2008 – 2010).
Naibu Waziri: Ofisi ya Waziri Mkuu – Tamisemi (2006 – 2008)

Elimu:
Stashahada , Chuo cha Uongozi wa Maendeleo Mzumbe (IDM) (1985)
Shahada ya Uzamili ya Uongozi (IDM) (1992-1994)

Historia ya Ajira
Afisa Tawala Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
Meneja wa Kiwanda cha Maturubai Morogoro (Morogoro Canvas Mill)( 1994- 1995)
 
Elimu kusoma sana sio kigezo bora cha uongozi,hawa wasomi mbona wanaliingiza Taifa majangani.

Cha muhimu ni kiongozi bora mzalendo.
 
Viongozi wanapaswa kusoma sana uchumi nimeona kozi muhimu kama MBA kasoma mmoja tu naungana na sumaye viongozi wa leo wasome MBA wazijue capacity charges wajue partnership wajue taxes wajue inflation wajue madhara ya kutorosha feza na kutakatisha fedha wailewe bajet waelewe mikataba waelewe company law nchi yetu inapigwa sababu hiyo ndo mana warioba anataka watu watoke nje ya bunge mfano unamchukua utoh waziri mkuu, Asad wa fedha, Kimei MIPANGO NA UCHUMI
 
Naona wengi waliwekeza hela nyingi kusoma nje ya nchi na sasa hela zao zimerudi na faida juu ila kiutendaji ni kama vile wana cheti cha chekechea tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom