CV za MaCEO wa Serikali

Kifo

Member
Feb 13, 2008
20
4
WanaJF,
samahanini kwa kuwa kimya sana. Nimerudi leo kutoka likizo ya kijijini kwetu. Leo nina jambo moja naomba tuchambue na kupanga CV za maCEO waserikali ili tupate angalau asusa zao. Mie nitatoa muongozo
1. Dr Dau (NSSF) - huyu ndio mfuko mkubwa wa Manji na ndio mmojawapo anayempa jeuri manji,ni mdini mpaka basi....nilikosa kazi hapo kisa mimi ni mkristo
2. Erio (PPF) - jamaa ni mshabiki mkubwa wa mpira (simba na man utd) zaidi ya hapo sina jipya lake
3. Tillya (TRA)- tatizo anaAmrishwa sana na hapewi nafasi ya kufanya maamuzi
4. Mahingila (BRELA) - jamaa anaongoza kuandikisha makampuni hewa kwa shinikizo na maagizo ya mafisadi wakuu
5. Kamuzora (Bima) - huyu jamaa ndio hafai kabisa,nchi haijui anafanya nini. Elimu yake ni ndogo sana ukilinganisha na kazi anayofanya. Inasemakana aliwekwa na Karamagi na Kamala. Ameshaharibu insurance industry kabisa!
6. Prof. Nkoma (TCRA) - Huyu naye hana msaada kabisa kwani anawatajirisha voda na wenzake bila kujali maslahi ya watz
7. Mlinga (PPRA) - huyu jamaa anajitahidi lakini hana meno na sasa wanaendesha semina nyingi sana bila dira.Ubadhirifu
8.Maimu (RITA)- Aisee huyu ni fisadi mkubwa sana na ndiye aliyeanznisha maexpert wa IT uchwara pale utumishi wakawa wanakula bila kufanya kazi na juzi alikuwa awe CEO wavitambulisho vya taifa yeye na kyaruzi
9. Benno (BOT) - mhhh
10. Kimei (CRDB) - tender zote pale CRDB anashinda mke wake
11. Snaga(LAPF)- alimkimbia Dau kwa udini na kukosa dira.

Wadau naomba mnipe details zaidi za watu hawa ambao wengi ni mafisadi kama sio wa hela ni uongozi,tuwachambue na ikiwezekana tuwe na database yao ili tuwe tunamaliza kazi mapema
 
WanaJF,
samahanin

Hii style duh!! anyway mi nilichokielewa ni kwamba unaomba samahani kwa kuhitaji kupata CV za viongozi waandamizi wa serikali! Kwa nini uombe msamaha lakini? No harm or offence intended mkuu...

wenye msaada toeni hapa..
 
Kifo,
mie nimekuelewa vizuri inaelekea unataka cv zao kwa kucheki maovu hasa ili yajulikane manake umeanza kwa kutoa maovu kidogo. Kaka/dada mie nina usongo na huyo Kamuzora. Hivi insurance industry inafanya nini kwa taifa hili?? Kwa taarifa yako huyo jamaa hana shule kabisa na inasemekana alishaikosa hiyo kazi kwani kwa mujibu wa tangazo la kazi ilihitaji mtu mwenye Masters na yeye hana hata diploma zaidi ya certificate ya insurance. Hivi wizara ya fedha walifumba machooo??Au ana urafiki na Mkullo??? Who is carrying him?? Jamani watu wa Insurance Industry tupeni uhondo tumechoka kuonewa ktk isnurance!!hatujui wala umuhim wake
 
1. Dr Dau (NSSF) - huyu ndio mfuko mkubwa wa Manji na ndio mmojawapo anayempa jeuri manji,ni mdini mpaka basi....nilikosa kazi hapo kisa mimi ni mkristo
tuhuma za huyu mzee si ngeni machoni kwa watanzania.inawezekana ulikosa kazi kwa kukosa sifa,una uhakika kama ulipita interview??.
2. Erio (PPF) - jamaa ni mshabiki mkubwa wa mpira (simba na man utd) zaidi ya hapo sina jipya lake
huyu kaoa kwa kina Mzee Ben.

8.Maimu (RITA)- Aisee huyu ni fisadi mkubwa sana na ndiye aliyeanznisha maexpert wa IT uchwara pale utumishi wakawa wanakula bila kufanya kazi na juzi alikuwa awe CEO wavitambulisho vya taifa yeye na kyaruzi

Maimu ndiyo CEO wa Nationa ID Agency so far mpaka sasa,suala la kuanzisha Ma IT Exert Uchwara pale Utumishi linaweza likawa lina ukweli.tupe majina ya hao Ma IT Expert Uchwara wa hapo ili tupime na kuangalia CV zao..
11. Snaga(LAPF)- alimkimbia Dau kwa udini na kukosa dira.
tunalifayia Uchunguzi suala la Udini la Dr. Dau,najua ni mjahidina ila suala la ukabira ni jipya kwangu..we will know then
 
Haya wakuu;kwa hakika sasa tunataka malaika ndio waongoze mashirika yetu ya umma!
 
Haya wakuu;kwa hakika sasa tunataka malaika ndio waongoze mashirika yetu ya umma!

Kimsingi hii mada ni nzuri, tunatakiwa tujue watu wanaoongoza mashirika nyeti kama haya wanasifa zipi ili watanzania wajue wanaongozwa na watu gani. Napendekeza kwa mtu mwenye cv za hawa watu atoe ktk pande zote mbili mazuri na mabaya yake. Unajua Tanzania tumefika hapa tulipo leo kwa sababu ya kutotaka kufahamu kwa undani wanaotuongoza wanatabia gani, wanaleta ufanisi, au hasara tupu. Tukiwafahamu walivyo tutapiga kelele juu yao kama huyu wa insurance kama kweli sifa zinatakiwa awe na Masters au zaidi harafu yeye ana certificate tu hili linahitaji kupigiwa kelele kwa sababu ya wezekana ubovu wa sector ya insurance inaletwa na huyu jamaa. kumbukeni Tanzania sasa tuko ktk wakati mzuri sana tumeanza na mawaziri sasa tunashuka chini na tutafika mpaka kwa wakurugenzi wa wilaya mahari ambapo naamini kunamadudu kupita kiasi. Tusiwe wavivu kusikia na kuchangia bila haya nani angejua Chenge anamiliki bilion 15? Yawezekana baadhi ya wakuu wetu wa mashirika wanapesa kama hizo au hata zaidi?

Kwa kutilia umhimu wa hoja hii ningependa kuongezea watu wafuatao ktk kujua list yao

UDSM -VC
SUA -VC
MHINBILI
MKEMIA MKUU
JAJI MKUU
MKUU WA MJESHI
MABALOZI WETU NCHI ZA NJE
 

Wadau naomba mnipe details zaidi za watu hawa ambao wengi ni mafisadi kama sio wa hela ni uongozi,tuwachambue na ikiwezekana tuwe na database yao ili tuwe tunamaliza kazi mapema

Mada ulianzisha ni nzuri sana lakini iko too simplistic na sie wengine humu JF hatupendi mambo ambayo yakekaa kirahisi rahisi namna hii

Hujaleta ushahidi wowote wa maana kusupport hoja zako. Mfano wa NSSF umeshindwa kuleta hoja ya kuonyesha udini wa Dr Dau ni upi na wapi na umeathiri vipi shirika tangu aingie pale. The same applies na allegations dhidi ya hao jamaa wengine. Hivyo its fair to conclude kuwa:

1209071123.jpg
 
Nashukuru nami niweza kusoma na kuwa mfanyakazi ktk sekta zote,i mean serikalini na binafsi. WanaJF sijawahi kuona sehemu iliyona wafanyakazi vilaza kama serikali na kubebana. Huyu aliyeanzisha swala la CV za maCEO kwa kweli anastahili pongezi 'tunahitaji kuwa cv zao' ila mambo kama ya mataka anayofanya yasiendeleee kwa kuwa JF itakuwa tayari na habari zake zote,kifo hongera!! Mie ninamfahamu sana huyo Kamuzora wa bima,sina ubishi yeye ndio tatizo katika kuua bima.Kwa nini, ni hivi
1.Ameshindwa hata kwa nukta moja kuihamasisha serikali itoe kipaumbele kwenye bima,
2.Soko la bima linamilikiwa na wageni (wakenya),anawasaidia na kuhakikisha wanafanikiwa ilihali ofisi kama yake kenya (Idara ya Bima Kenya) haina kazi kama yake
3. Hili la elimu,mimi nalijua kuwa kweli elimu yake ni ndogo na ndio sababu hata mkataba wake ulileta utata kwani kampuni iliyopewa kufanya kazi ya usahili ililazimishwa na vigogo kubadilisha job specification ili afiti otherwise asingekuwepo.
4. Huyu jamaa ana ukabila sana na kuna kipindi mie nikiwa ikulu tulipokea malalamiko mengi kuhusu yeye na bahati nzuri mengi yalikuwa yanachanwa na mtu wa masijala ikulu ambaye wana uhusiano.
5.Ukabila huu ulipelekea yeye kuchunguzwa na bodi yake lakini cha ajabu mchunguzi alikuwa advocate mmoja ambaye alikuwa supervised ktk masters na chairman wa bodi hiyo na hivyo transparency ilkuwa zero. Nasikia ana wahaya wenzake kuanzia walinzi mpaka Bwna Fedha....aibu Bima haitakaa inufaishe watanzania
 
Tukupe Details Halafu Uandae Makala Ya Gazeti Lako ? Kwanini Usifanye Kazi Mwenyewe Kwa Jasho Lako ?

Hizo Tuhusu Dhidi Ya Dau Ni Kubwa Na Unajaribu Kuchafua Jina La Dau Kwa Makusudi Tunakuomba Ufute Kauli Hyo La Sivyo Sema Ni Jinsi Gani Amehusika Kaitka Kukatakiwa Kwako Kazi
 
Huyu aliyeanzisha swala la CV za maCEO kwa kweli anastahili pongezi 'tunahitaji kuwa cv zao'
jamani kwani Curriculum Vitae (CV) is a summary of ones educational and academic background
sana mbona mnoyotaka sio CV ila vibweka/majungu nashuri ubadilishe title ya hii thread na iwe ubovu/vibweka/majungu ya maCEO ......
 
Tukupe Details Halafu Uandae Makala Ya Gazeti Lako ? Kwanini Usifanye Kazi Mwenyewe Kwa Jasho Lako ?

Hizo Tuhusu Dhidi Ya Dau Ni Kubwa Na Unajaribu Kuchafua Jina La Dau Kwa Makusudi Tunakuomba Ufute Kauli Hyo La Sivyo Sema Ni Jinsi Gani Amehusika Kaitka Kukatakiwa Kwako Kazi

Thats not fair ku-conclude hivyo, inamaana kila mtu anayechangia/kuanzisha thread na kuomba more lights over the issue anataka ''kuandaa makala''?


Nakubaliana na wewe kimsingi kuwa tuhuma dhidi ya Dau ni kubwa, lakini ambacho ungetakia kusema/kumwomba afanye mwanzilishi wa hii thread ni kile ambacho GT hapo nyuma kasema kuwa atupe data kamili, for instance kwa issue ya Dau ambayo yeye mwenywe ni victim then we expect him/her to give us more thorough data ni jinsi gani alikuwa victim wa discrimination!

Ku-concl. moja kwa moja kuwa jamaa nalenga ''kumchafua Dau'', i think it sound more ''subjective coclusion'' to me!..
 
Thats not fair ku-conclude hivyo, inamaana kila mtu anayechangia/kuanzisha thread na kuomba more lights over the issue anataka ''kuandaa makala''?


Nakubaliana na wewe kimsingi kuwa tuhuma dhidi ya Dau ni kubwa, lakini ambacho ungetakia kusema/kumwomba afanye mwanzilishi wa hii thread ni kile ambacho GT hapo nyuma kasema kuwa atupe data kamili, for instance kwa issue ya Dau ambayo yeye mwenywe ni victim then we expect him/her to give us more thorough data ni jinsi gani alikuwa victim wa discrimination!

Ku-concl. moja kwa moja kuwa jamaa nalenga ''kumchafua Dau'', i think it sound more ''subjective coclusion'' to me!..

Si wakati wa kuendekeza Uswahiba.
Serikali imeonywa kutowachagua wenyeviti na wakurugenzi wa bodi za mashirika ya umma kwa misingi ya uswahiba, kulipa fadhila, dini na kabila, bali ifanye hivyo kulingana na uwezo wa wahusika hao.

Baadhi ya wabunge, watendaji na wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma walipokuwa kwenye kikao cha wabunge wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma, wenyeviti na watendaji wakuu wa mashirika ya umma.

Ni wakati muafaka sasa baada ya Rais Jakaya kuwapa madaraka marafiki zake wa karibu kwa nia nzuri tu lakini mastokeo waliboronga kumtia aibu kiongozi wetu huyo baada ya kuibuka ufisadi katika sehemu mbalimbali na kufanya wahusika kuachia ngazi.

Peter Serukamba, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), alisema umefika wakati kwa Serikali kuangalia watu wa kuwapa nafasi ya kuendesha mashirika ya umma na kuachana tabia ya kutoa madaraka kwa watu wasiostahili.

Alisema watu wasiostahili wanapopewa madaraka huwa chanzo cha shirika au taasisi za serikali kutofanya vizuri, hali inayosababisha taifa kupata hasara kubwa pamoja na kupoteza ajira kwa baadhi ya watumishi.

Elisa Mollel, Mbunge wa (CCM) Arumeru Magharibi, alisema ufanisi katika mashirika hayo unategemea zaidi kuchagua kiongozi mwenye taaluma katika sekta husika pamoja na uzoefu alionao kwenye uongozi.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, alisema ni vema watendaji wa mashirika na taasisi za serikali wakawa makini katika utiaji saini mikataba ili kuepuka mambo ya ufisadi ambayo yameligharimu taifa fedha nyingi.

Alisema kila kukicha taarifa za ufisadi ndizo zinazopewa nafasi katika vyombo vya habari na watendaji wamekuwa wakitumia muda mwingi kushughulika na mambo hayo, jambo linalofanya muda wa kushughulikia maendeleo kuwa mdogo.

“Muda mwingi tunautumia katika kupiga kelele kuhusu ufisadi, sasa ni wakati kwa wenzetu kufanya kazi kwa umakini ili tuweze kwenda mbele na kutimiza malengo yetu,” alisema Zitto.

Source Tanzania Daima.
 
Sasa kama kuna mtu anyeona kuwa kifo alikosea na asem,this is a big concern jamani. Tukumbuke kuwa CV ni elimu na kazi ambazo ushawahi kuzifanya.. Nimesoma kuwa mkurgenzi wa Bima ni mkabila sana na kuwa mwenyekiti wake wa bodi alimsaidia kufanikisha hilo,je hauoni ufisadi huo achilia mbali elimu yake kuwa ndogo hata wabunge wa chama tawala wanajua hilooo!!Tuwe makini na maslahi ya watz jamani. Kuna viongozi kibao wanafanya ufisadi hasa katka manunuzi . Kuna habari ya ofisa mmoja naifatilia kwa mkaguzi wa hesabu wa nje ambaye alikagua hapo siku si nyingi kuhusu manunuzi ya hapo nitawaletea.
 
mwanangu mie naona ni mambo ya kiswahili kwamba wewe ukikosa kazi basi umebaguliwa,,,unauhakika gani kama watahiniwa wengine uliwazidi vigezo?? maana hadi hapa mie nimehsaona uwezo wako ni mchafu na mdooooogo sana so ulistahili kukosa hata Uhudum ofisini kwa dau maana jamaa is very smart...sory aise
 
UMEMSAHAU MMOJA BAINA YA mapepe WALIOSAHAULIKA! gues who?

MREMA - CEO (TANROADS): huyu utendaji wake hauna tofauti na Mrema wa TLP(siku saba mbele) huyu labda Magufuli arudi ndo atamcontrol!
 
mwanangu mie naona ni mambo ya kiswahili kwamba wewe ukikosa kazi basi umebaguliwa,,,unauhakika gani kama watahiniwa wengine uliwazidi vigezo?? maana hadi hapa mie nimehsaona uwezo wako ni mchafu na mdooooogo sana so ulistahili kukosa hata Uhudum ofisini kwa dau maana jamaa is very smart...sory aise

Good analysis indeed!
Kifo thread yako na ife and so your all propaganda. I am very certain uli deserve kukosa kazi..you are too shallow to make arguments na kutetea.

Upenzi wa mprira..na utendaji wa mtu wa kazi wapi kwa wapi? hii inaonyesha kama mada yako ni dhaifi, lemavu na isiyo na mashiko yoyote ya kuteegmea.
My conclusion! haya ni majungu na it is a shame kupewa nafasi kuandika humu..mods..threads kama hizi zina undermine credibility ya JF na nashauri ifitiliwe mbali.

Naomba kuwasilisha.
Kigwele wa Kingwele.
 
mm hapo mkuu nimekuelewa unataka CV chafu za hawa viongozi wa mashirika ya umma.Naomba wana JF toeni CV zao ambao mpo kwenye vitengo kati ya vivyo alivyo taja tuwamulike hawa.
 
Naomba mwongozo Mwenyekiti>>
Huyu Kifo ametoa baadhi ya CV kama na wewe boss wako anaudhaifu wa kifasadi anika hapa naona Kifo yeye ni Yanga alafu ni Arsenal kwa hiyo alinyimwa masurufu au kuna jamaa ake ambaye yupo na huyo boss ofisi moja hamtendei haki kwa vile ni Yanga au timu nyingine.Kwa hiyo ni wazo zuri na sio kuifutilia mbali hoja.
 
Back
Top Bottom