Mbona ana BA wandugu?Au alitakiwa awe na elimu kiasi gani?
Mbona ana BA wandugu?Au alitakiwa awe na elimu kiasi gani?
Duh nafikiri tatizo ni anayewateua. Aibu.
Siasa za Chunya ndani ya JF, hao wenye CV nene wamefanya nini, suala hapa ni uwezo wa mtu kuongoza.
Wakuu tulishaambiwa hakuna mtu iyesomea uwaziri! Si agadhali huyo naona amesoma OUT, wengine je? Waziri si lazima awe na fani inayohusiana na wizara yake. Tumesahau enzi za Prof. Sarungi (Bingwa wa upasuaji mifupa) kuwa waziri wa utamaduni na michezo!Ahasante kwa kutujuza! Yaani Mwalimu wa shule ya Sekondari BINAFSI, asiyepata mafunzo yeyote ya UALIMU, anapanda ngazi hadi kufikia UNAIBU WAZIRI WA ELIMU!!!! Tunaipeleka wapi ELIMU katika nchi hii jamani? Lakini usishangae wana JF kibao watajitokeza na kumsifia kuwa jamaa ni KICHWA!!! We haya we!
Mkuu sasa wewe unataka kuwatukana watanzania hasa wapiga kura wa majimbo iliyoyataja! Lema alipambanishwa na PhD wananchi wakamchagua yeye wakamuacha PhD kwa hiyo hayo ni matakwa ya wananchi wa Arusha. Na wao wana akili na wanajua kuwa huyo Lema ni.STD VII na yule mwingine ni PhD lakini ndio matakwa yao. Nenda Rorya waulize akina Prof. Monyo nini kiliwapata kwa mbunge mmoja jina lake sijui Ayilo. Nasikia jamaa ni std saba lakini aliwagaragaza maprofesa! Tukubali tu na kuyaheshimu matakwa ya wapiga kura.Bado safari yetu Ndefu kiukweli Mlugo nafasi ya Unaibu iko juu sana kwa Uwezo wake! Ni kama vilaza hawa eti ni Wabunge Mr Sugu-Form 4 Mbunge wa Mbeya Mjini,Godbless Lema -form 4 Mbunge Arusha Mjini! Yani form 4 failure anaongoza jimbo!