CV ya Naibu Waziri wa Elimu Philip Mulugo: Je inatosheleza kusimamia majukumu aliyopewa?

Status
Not open for further replies.
Mkuu WildCard.

Ndiyo ushangae Mzee wa Kiraracha kaacha mark yake wizara ya mambo ya ndani hakuwa na degree/PhD.Wapo mawaziri wengi wenye shule za kutisha jiulize wamefanya nini !.


Mrema aliwahi kuwa NAIBU WAZIRI MKUU na Waziri wa Mambo ya ndani akiwa na darasa la nane tu na ukuruta wa UwT basi.
 
Watu huwa tunasema kuendelea kuongozwa na CCM ni janga tunapuuzwa!!!

Ubaya ni kuwa bado wataendelea kutubuluza mpaka tupate akili ya kina tunisia na misri!!
 
Wadau naomba tuiangalie CV ya huyu Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi tuone kama ina kidhi majukumu mazito :

First Name: Philipo
Middle Name: Augustino
Last Name: Mulugo
Member Type: Constituency Member
Constituent: Songwe


EDUCATION
Rukwa Primary School, Chunga Primary Education 1982 1989 PRIMARY
Mbeya Secondary School O-Level Education 1990 1993 SECONDARY
Songea Boys' High School A-Level Education 1994 1996 HIGH SCHOOL
Open University of Tanzania BA (Economics Education ) 2002 2008 GRADUATE
CERTIFICATIONS

EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
The Parliament of Tanzania Member - Songwe Constituency 2010 2015
Southern Highland Secondary School School Managing Director 2008 2010
Southern Highland Secondary School Administrative & Personnel Officer 2005 2010
Southern Highland Secondary School Teacher 2000 2004
POLITICAL
Chama Cha Mapinduzi, CCM Member - National Executive Committee 2008
Chama Cha Mapinduzi, CCM Secretary General - Mbeya Region (Parents) 2008
Chama Cha Mapinduzi, CCM Member - Chunya District Political Committee 2007
UKITAKA JIBU LA KWANINI KATEULIWA ULIZA WAWILI HAWA Dr (wa kupewa tu!) MERRY MWANJELWA NA MR. PRESDAA Dr(wa kupewa tu!) JK a.k.a Mr. NICE.
 
Asante mkuu kwa kulileta hili humu jamvini personally nimeshawahi kufanya kazi na huyu jamaa nini afanye kwa nyimbo lkwenye suala la elimu na IT, jamani huyu jamaa ni kilaza sijapata ona, hajui hata windows unaweza ukainstall hapa tz coz wakati anaandaa bajeti alikuwa anaweka software costs, mbali na hayo na kilichonifanya nimmwage ni kwamba alikuwa anataka kuwaridhisha wapiga kula wake eti awe mbunge wa maisha hata kama anachowapelekea hakitawasaidia watu wake.

Akaniomba nihakikishe kila tutakachokifanya kifike kwa media na picha nyingi na lazima kupikwe pilau kupumbaza watu, kila anachokipresent huyu jamaa kimeandaliwa na mtu mwingine hajui hata kutumia microsoft word, trust my words. imenishangaza sana hivi KJ alitumia kigezo gani kumchagua?achana na hilo huyu jamaa hawezi kuflow in English for more than 5mins.

acha nipitie some of his hard copy documents nizimwage humu muone ni kilaza kiasi gani.

Ntarudi
 
sasa unafikiri angemteua nani kwa mkoa wa mbeya? wananchi ndio wabunge waliowachagua na jk anachagua mule nyie wananchi mliowachagua, mulugo anaziba nafasi ya lucas siame jamani ambae alikuwa waziri na alishindwa uchaguzi na chadema na ndio maana akina gideon cheyo wa ileje alikaa muda mwingi kwenye uwaziri kwa ajiri ya ratio hata kibona nae wa ileje na ndio maana ilibidi mwakyusa awedroped ili mwakyembe aingie na pia chunya ni jimbo halijawahi toa waziri hivi vitu vinakwenda kwa ratio!! sasa hapo wa kulaumiwa ni wanachi wa songwe kumpa ubunge mulugo wangempa mtu mwenye madegree sio?

hoja hapa zungumza kuwa mulugo hakustahili wizara ya elimu na alistahili wizara ipi? maana uwaziri ni stahili yake kutoka miongoni mwa wabunge wa ccm wa mkoa wa mbeya

nadhani umenielewa


Hakuna kipengele kwenye katiba kinacho mbana Rais kuchagua cabinet membees kwa uwiano. Huo ni woga tu wa wanasiasa. Siwezi kusema Rais angemchaguavnani badala ya Mulugo, nafikiri wote tunawajua wabunge wa Mbeya. Ila kama hayupo anayeweza nafuu JK angetuachia wale wawili tu Mwakyembe na Mwandosya. Hii ni kejeli kumuweka mtu mwenye profile ya Mulugo na integrity ya wasiswasi
 
Tatizo hasa nini?
  1. Elimu yake ?
  2. Namna alivyopata Unaibu Waziri?
  3. Utendaji wake wa Kazi kama N/Waziri?
 
Mrema aliwahi kuwa NAIBU WAZIRI MKUU na Waziri wa Mambo ya ndani akiwa na darasa la nane tu na ukuruta wa UwT basi.

Darasa la nane la mkoloni lilikuwa bora kuliko darasa na 12 au wakati mwingine hata la 14 la sasa
 
Ahasante kwa kutujuza! Yaani Mwalimu wa shule ya Sekondari BINAFSI, asiyepata mafunzo yeyote ya UALIMU, anapanda ngazi hadi kufikia UNAIBU WAZIRI WA ELIMU!!!! Tunaipeleka wapi ELIMU katika nchi hii jamani? Lakini usishangae wana JF kibao watajitokeza na kumsifia kuwa jamaa ni KICHWA!!! We haya we!

Maajabu kama haya utayaona Tanzania tu
Hata Ualimu hajasomea lakini JK kampa aongoze wizara
 
Waziri ni "political post" na si "technical post" ninavyofahamu (I stand to be corrected)

Pale wizarani kuna PS, huyo ndo anapaswa kuwa mtaalamu. Waziri ni kisiasa zaidi, hata kama hana background ya wizara anayosimamia. Sasa kama huyu ana bahati ya kuwa "mwalimu" na background ya admin, anatosheleza.

huko sahii lakini tuangalie haya mambo,PS yuko pale kwasababu ya meritocracy na waziri yupo kwa spoil and patronclientile sasa hapo utaweza kupata jibu kuwa kwa utawala kama huu wa Tz unafuata mfumo gani katika maamuzi.
 
yaani hapo kaz ipo iyo mnayosema southen ni shule yake yeye mwenyewe mulugo
cv mbovu
jamaa kuna kpnd shule yake ilifungiwa kwa wizi wa mitihani ya 4m 4 leo ndo amepewa unaibu wazr kweli....
 
Maajabu kama haya utayaona Tanzania tu
Hata Ualimu hajasomea lakini JK kampa aongoze wizara
jamani jamani ukiwa mwl ndo unawezo wakuongoza wizara yako?hebu acheni hizo,kuna maprof wa elimu wamepewa kazi ya kuongoza na wamefeli
 
Kama ni kweli alirudia darasa la saba.........je hilo jina analotumia ni lake kweli?........hapo bado hatujaenda kwenye masuala ya umri........just curious
 
Mkuu sasa wewe unataka kuwatukana watanzania hasa wapiga kura wa majimbo iliyoyataja! Lema alipambanishwa na PhD wananchi wakamchagua yeye wakamuacha PhD kwa hiyo hayo ni matakwa ya wananchi wa Arusha. Na wao wana akili na wanajua kuwa huyo Lema ni.STD VII na yule mwingine ni PhD lakini ndio matakwa yao. Nenda Rorya waulize akina Prof. Monyo nini kiliwapata kwa mbunge mmoja jina lake sijui Ayilo. Nasikia jamaa ni std saba lakini aliwagaragaza maprofesa! Tukubali tu na kuyaheshimu matakwa ya wapiga kura.

Kimbunga bana
 
Waziri ni "political post" na si "technical post" ninavyofahamu (I stand to be corrected)

Pale wizarani kuna PS, huyo ndo anapaswa kuwa mtaalamu. Waziri ni kisiasa zaidi, hata kama hana background ya wizara anayosimamia. Sasa kama huyu ana bahati ya kuwa "mwalimu" na background ya admin, anatosheleza.

Mmmmmmmmmmm. Lakini pale ambapo Waziri ana elimu ya jambo analoongoza huwa ni afadhali zaidi. Mara nyingi Mawaziri wa Fedha kwa nchi nyingi ni wanauchumi waliobiobea. Hebu kumbuka waizara hiyohiyo na Waziri Mungai, alichokifanya kinalaaniwa mpaka leo. Anafuta michezo, michepuo yote mashuleni, mpaka mchepuo wa kilimo akafuta. Ndio hao hao. Mlugo angekuwa makini na Waziri wake, wale vijana waliofutiwa mtihani wangerudia mtihani mwingine ndani ya mwezi mmoja hata kama ni huo huo. Wangepatikana wazuri na wasiojua
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom