CV ya Naibu Waziri wa Elimu Philip Mulugo: Je inatosheleza kusimamia majukumu aliyopewa?

Status
Not open for further replies.

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
1,371
2,000
Halafu ali fanya collusion na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Songwe kwa kumchelewesha mgombea wa CDM aliyekuwa ameenda kuchukua form za kugombea uchaguzi mkuu. Kuna mtu bogus alipewa form za CDM na msimamizi wa uchaguzi halafu alipofika Paul Ntwina anayetambuliwa na CDM makao makuu akaambiwa tayari tumekwisha toa form. Then yeye akawa declared mbunge aliyepita bila kupingwa. No Mulugo is not competent at all
 

Mkiliman

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
982
500
Hili ni tatizo la mamlaka ya uteuzi, ambayo ni Rais JK...yeye huteua hata wasiokuwa na sifa za kuongoza hiyo wizara. Ukweli ni kwamba huyu Naibu Waziri hana vigezo mtambuka kuelewa upana wa kinachotakiwa kufanyika ili kuendeleza jitihada za kuelimisha watu. Fadhila siku zote haiangalii unalipaje, kinachotakiwa ni kutoa nafasi tu kwa yule unayeamini unamlipa fadhila kwa alichokutendea siku za nyuma.

Hali hii itabidi ikome wakati wa uandishi wa katiba mpya, hakuna haja ya kuwa na Rais anayeteua kwa fadhila, ushwahiba na pasipo kuthibitishwa na chombo (for checks and balances purposes) chochote cha juu. Huu utaratibu ukome kabisa, kwani huyu Rais wetu anaonekana hana busara ktk uteuzi wake, tazameni wateule wake wote ktk ubalozi, ukuu wa mikoa/wilaya n.k ni kwa marafiki na walioshindwa ktk chaguzi za ndani.

Mwisho wa upuuzi wa uteuzi wake upo karibu sana.....!!

Mungu Ibariki Tanzania.
 

Nsesi

JF-Expert Member
Nov 20, 2008
374
195
Siasa za Chunya ndani ya JF, hao wenye CV nene wamefanya nini, suala hapa ni uwezo wa mtu kuongoza.
 

Nsesi

JF-Expert Member
Nov 20, 2008
374
195
Huihui2,

Hata kama unachuki zako na huyo Mulugo sio sahihi kudanganta watu. Ntwina alijichelewesha mwenyewe kwa tamaa, alihama vyama vitatu ndani ya masaa 24!!!

lakini ni Ntwina yupi unayemtetea wewe, yule mwizi wa fedha za wafadhili kwa ajili ya shule za Songwe, ambaye aliokolewa na tabia ya kulindana ndani ya CCM! Hebu acha utani bwana, tupo wenye data zao hapa.
 

Safety last

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
4,230
2,000
Wakuu huyu waziri mkumbuke ni yatima wazazi wake wote waliliwa na mamba huko kwao mbeya akiwa mtoto mdogo.!
 

Mlengo wa Kati

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
2,731
0
Bado safari yetu Ndefu kiukweli Mlugo nafasi ya Unaibu iko juu sana kwa Uwezo wake! Ni kama vilaza hawa eti ni Wabunge Mr Sugu-Form 4 Mbunge wa Mbeya Mjini,Godbless Lema -form 4 Mbunge Arusha Mjini! Yani form 4 failure anaongoza jimbo!
 

Mokerema

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
235
0
Bila kutafuna maneno utaratibu uliowekwa na CCM kuwateua Mawaziri kwa kuzingatia makabila na balance ya mikoa pamoja na jinsia ni upuuzi mtupu na wa kufuata. Ili tujikwamue narudia wabunge wasichaguliwe kuwa Mawaziri. Tuwe na mechanism ya kuteua professionals amabo watasimamia mambo kwa udhabiti na weledi. Utaratibu huu wa mtu mmoja kuteua kila mtu is Kama anagawa birthday cake ni wa kufuta. Tanzania has everything inaweza ikawa ya kwanza Afrika kwa maendeleo tatizo miaka yote ni uongozi and tumefanya kila kitu politic. Remove politics in the main stream and we shall be home and dry. Haruna viongozi wala utawala we only have big time comedians tangu 1961! Walisema wahenga kwamba Kiongozi ni kioo cha watu anaowaongoza. Sijui kama nimetafsiri vizuri. Garbage in garbage out!:A S 465:
 

mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
2,000
Siasa za Chunya ndani ya JF, hao wenye CV nene wamefanya nini, suala hapa ni uwezo wa mtu kuongoza.

Lkn kwa Mlugo mkuu,, ni mweupe sana tu, I tell u for sure kupata kwake unaibu wa wizara ilikuwa mipango tu!
 

mopaozi

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
3,305
1,250
Yaani nilitegemea mngesema jamaa kihiyo ila kwa hy CV anaweza pewa kazi hata na Obama ya uwaziri wa elimu
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,355
2,000
Ahasante kwa kutujuza! Yaani Mwalimu wa shule ya Sekondari BINAFSI, asiyepata mafunzo yeyote ya UALIMU, anapanda ngazi hadi kufikia UNAIBU WAZIRI WA ELIMU!!!! Tunaipeleka wapi ELIMU katika nchi hii jamani? Lakini usishangae wana JF kibao watajitokeza na kumsifia kuwa jamaa ni KICHWA!!! We haya we!
Wakuu tulishaambiwa hakuna mtu iyesomea uwaziri! Si agadhali huyo naona amesoma OUT, wengine je? Waziri si lazima awe na fani inayohusiana na wizara yake. Tumesahau enzi za Prof. Sarungi (Bingwa wa upasuaji mifupa) kuwa waziri wa utamaduni na michezo!
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,355
2,000
Bado safari yetu Ndefu kiukweli Mlugo nafasi ya Unaibu iko juu sana kwa Uwezo wake! Ni kama vilaza hawa eti ni Wabunge Mr Sugu-Form 4 Mbunge wa Mbeya Mjini,Godbless Lema -form 4 Mbunge Arusha Mjini! Yani form 4 failure anaongoza jimbo!
Mkuu sasa wewe unataka kuwatukana watanzania hasa wapiga kura wa majimbo iliyoyataja! Lema alipambanishwa na PhD wananchi wakamchagua yeye wakamuacha PhD kwa hiyo hayo ni matakwa ya wananchi wa Arusha. Na wao wana akili na wanajua kuwa huyo Lema ni.STD VII na yule mwingine ni PhD lakini ndio matakwa yao. Nenda Rorya waulize akina Prof. Monyo nini kiliwapata kwa mbunge mmoja jina lake sijui Ayilo. Nasikia jamaa ni std saba lakini aliwagaragaza maprofesa! Tukubali tu na kuyaheshimu matakwa ya wapiga kura.
 

CERDIC

Member
Oct 3, 2011
16
0
The minister is a presidential appointee therefore who should be blamed by giving the Tanzanian the person whom we think does not deserve that position? these are the things you guys should strongly critisize these appointment and its not only Mulugo may be there are so many. otherwise the war of fighting the three enemies will not end with victory.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom