CV ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CV ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rosemarie, May 25, 2012.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Wakuu naomba sana mwenye CV ya mkuu huyu Dickson Maimu,kila wakati huyu akitokea kwenye Tv ninakuwa na mashaka sana na uwezo wake,kipindi cha nyuma alikuwa anatokea akiwa amevaa cheni shingoni na mapete kibao na mkufu mkononi,kwa kweli inanitia mashaka sana kama kweli ni mtu anayefaa kwa kazi hii,,vile vile kuongea kwake ni kama mtu wa kawaida wa kijiweni nashindwa nimweke kwenye kundi gani kiuwezo,naomba kujua kama kweli ni mtu aliye tayari kufanya kazi hiyo ya muhimu kabisa ya kuwapatia watanzania vitambulisho vya taifa kwa mara ya kwanza kabisa
   
 2. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kaka ni muhuni tu, alifanya sherehe kubwa na kuchinja baada ya appointmentakijua ni ulaji na sio kazi kubwa inayomkabiri.
  mengine tunaangalia na kunyamaza ili tuone kutatkea nini mbele. CV sina, mwonekano wake unamfanya watu wawe na doubt lakini inaonekana anashauriwa maana siku hizi macheni na mapete ameyapunguza.
   
 3. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  alikuwa chakula!
   
 4. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Achana na Mambo ya CV mkuu, Sometime doesn't work.CV ya Chami ilikuwa nzuri Then!
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Cha nani tena?
   
 6. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,754
  Trophy Points: 280
  may be mat.ka ye si ndio mlaji mzuri?
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sasa kuvaa cheni na mapete kuna uhusiano gani na uwezo wake au CV yake?
   
 8. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  naomba ufafanue zaidi,hivi watanzania wanajua yule jamaa kazi anayofanya ni ya muhimu sana?
   
 9. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  jama yupo smart sana ,semeni wazi kama nyie ni mapolisi au jeshi mlioaathirika kwa kugushi vyeti.Kama cheni mbona MKAPA raisi anakubwa zaidi au JOHN MALECELA WAZIRI MKUU MSTAAFU MZEE WA MVUMI
   
 10. P

  Pwito Senior Member

  #10
  May 25, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Si umeona walikoipeleka nchi na hayo maurembo yao.
   
 11. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Tuwe makini sasa jamani hii mambo ya kuweka premises za kuanza na negation sio kitu nzuri bana as appearance sometimes may deceive......cha maana iwekwe CV hapa na kazi alokuwa nayo hapo Home Affairs before sio oooonh mapete.......aaanh mikufu.......sijui muonekano wake hauna mvuto..... kwani tupo kamati ya maonesho??????

  Kama ni uvaaji hauendani na wadhifa just opine and quit
  If ni reliability versus tasks sawa.......just enquire
  Qualifications versus rsponsibilities......get a comparative framework

  Sio blah blah tuuuuuuuuuuuu

  May be we can advice for the fact that it is high time for the GoT to establish a website from which we can get particulars concerning high ranking Public civil servants to get rid of day to day complaints from the majority
   
 12. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #12
  May 27, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya VItambulisho vya Taifa- NIDA ,anatarajiwa kupigwaa chini wakati wowote kuanzia sasa....kwa kosa kubwa la kihaini la kuvunja sheria ya usalama wa Taifa,Taratibu za usalama wa Taifa zinakataza mtu ,taaisis au jumuia yeyote kutoa utambuzi wa Afisa au maafisa au watumishi wa idara za usalama ,na vyombo vyao...,Aidha ni marufuku kutoa taarifa yeyote itakayoonesha uwezo wa taasisi au chombo cha usalama .....ikiwemo majeshi.

  Taarifa zilizotolewa na NIDA zimeonesha udhaifu mkubwa wa kiuweledi .....,wa kutoa taarifa za undani juu ya uwezo wa maafisa na askari wa majeshi yetu,katika Hali ya kawaida ....NDugu Mwaimu ...alikuwa na uwezo kabisa wa kuandika barua ya Siri kwenda kwa Amiri jeshi mkuu au mkuu wa majeshi kueleza juu ya kile alichokibaini.......ili aweze kujibiwa....na Kushauriwa cha kufanya......,Kiukweli hakuna anayekataa kazi Yake ila ni utaratibu mbovu alioutumia kutokea taarifa..hizo nyeti kana kwamba alikuwa amekagua .....sekta ya umma ...ie walimu, madaktari ,etc...

  Katika Hali ya kawaida ya usalama inaelezwa kuwa Askari 250 wa jeshi la wananchi waliogundulika kuwa na majina mawili mawili...au yanayotofautiana na vyeti ....wengi wao wanatoka kitengo Nyeti cha Millitary Intelligence .....ambao karibu wote huwa na ...majina feki,,passport na VItambulisho zaidi ya kimoja...au hata passport za mataifa mengine....kadiri ya mikakati ya kijeshi.......Ni kosa la kihaini kutambua maaskari wa aina hii maana unaweza kuwasababishia Maafa na kuvuruga mipango Yao...,Pia imebainika kuwa ni maaskari wa kitengo hichi ambao wengine kwa sababu maalum ...wana VItambulisho vya idara Nyingine za kiraia ie ..TAnapa,wizara...na hata mashirika ya umma....au wizara ya nje.

  Pia ndani ya jeshi la Polisi...Kati ya Hao askari polisi 700 ....wapo wa kitengo cha DCI...plain clothed police....,kitengo cha madawa ya kulevya...,Iterpol etc...ambao nao inaelezwa sio ajabu kukutana wanatumia majina tofauti na ya kwenye vyeti....kutokana na unyeti wa kazi Zao....

  Haya ndio yanayofikia watu wa usalama kuona kuwa Ndugu Mwaim,hata Kama alikuwa na nia njema ....Kama Afisa wa serikali ...anayejuwa undani wake tayari amevunja sheria za usalama wa Taifa....kwa kushindwa kuwasiliana na vyombo husika katika Hali ya Usiri........stahili.
   
 13. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,650
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  Mkuu philemon,

  Maelezo yako yanajenga dhana potofu ambayo inaweza kutumika kutetea uhalifu wa kugushi kwa kivuli cha mwavuli wa usalama wa taifa.
  Vitambulisho vya kitaifa ndiyo msingi wa usalama wa taifa lenyewe hivyo taarifa zinazohitajika hapo ni zile za msingi na halisi zisizochakachuliwa kwa namna yoyote ile. Haikubaliki na ni ajabu kwa mtu yeyote mwenye akili timamu na uzalendo kwa nchi yake kukubaliana na dhana hii.
  Utambulisho fake unaoweza kutumiwa na wanausalama kwa shughuli maalum hauna uhusiano wowote na wala hautarekodiwa katika kumbukumbu zinazohifadhiwa na mamlaka ya vitambulisho vya kitaifa!
  Watanzania walio wengi wenye ufahamu wa kawaida tunajua kabisa kwamba vyeti vya kugushi vipo vingi na utamaduni huo unaendelea kwa sababu ya mawazo ya kipuuzi tu ya kutukuza vyeti katika usaili na hata kuteuwa au kupandisha vyeo wakati wenye vyeti hivyo hawana kitu kichwani. Hali hii ina uhusiano wa moja kwa moja na umasikini wa kitaifa unaotokana na maamuzi ya kijinga.
  Ili tuendelee lazima tuwe wakweli, tusahihishe makosa yaliyofanyika kwa njia za busara badala ya kutafuta visingizio vya kijingajinga tu kuhalalisha upuuzi!
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,602
  Trophy Points: 280
  Huyo Mwaimu kwani ametokea wapi?4i wamemuweka wenyewe hao hao wenye vitambulisho vingi??au hujui wewe alikotokea??utaishia hivyo hivyo na utasubiri sana!!!!
   
 15. C

  Cupid 50mg Member

  #15
  May 28, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napita tu na sitarudi.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Watanzania na Waafrika tuachane na kasumba ya kufikiri vyeti vingi vya kubandika ukutani ndivyo vinavyofanya kazi bila kuangaliwa uwezo wa mtu. Si kila aliyesoma ameelimika, na si kila aliyeelimika ana uwezo wa kuongoza. Kuongoza ni bongo la mtu. Mababu zetu walikuwa machifu wakubwa ambao hawakujua kusoma na kuandika, lakini waliweza kufanya organization nzuri na hata kupigana na wakoloni na kuwashinda, CV zao na bongo lao na uwezo wao.

  Kasumba hii ndiyo inayoturudisha nyuma kimaendelea kwa kufikira kusoma ndiko kuendelea. Wenye kujua zaidi siku hizi wanasomelea kile anachotaka kufanyia kazi kwani wengi wanasoma bila malengo ili mradi awe na sifa ya kwamba amemaliza chuo kikuu au phd na kuishia kutangatanga bila kazi, nini tatizo kusoma bila malengo.

  Nimeshuhudia nchi za ulaya na Marekani wengine huchukua mafunzo ya muda mfupi (short course) na baada ya hapa huajiriwa moja kwa moja kwa vile wamechukulia mafunzo katika taaluma inayohotajika kazini na mara wanaanza kutia pesa mfukoni mwao. Lakini wale wanaohitimu vyo vikuu wengi wanahangaika kupata kazi kwani elimu yao ni ya jumla jumla ambayo makampuni yakiwaajiri inabidi yaanze kuwafunza kazi tofauti na aliyechukua kozi mfupi maalum kwa ajili ya kazi hiyo. Ingawa kuna baadhi ya kazi zinahitaji kiwango fulani cha degree, lakini si hoja ya kuashiria uwezo wa kuongoza katika madara.

  Tuachane na ukiritimba wa kufikira CV ndizo zinafanya kazi kumbe ni kasumba tu ya Watanzania na Waafrika.
   
 17. p

  poison Member

  #17
  May 28, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Candid well said , nawashangaaga sana wakati mwingine wanazungumzia mbona alipata division one sijui honors so backwards, Nilipokuja Marekani nilionyesha ma vyeti yangu ya bongo walaa hawakuyaangalia waliniweka kwenye panel ya watu sita waliobobea interview siku nzima, wala kuomba sijui copy ya vyeti hawataki wewe andika tuu uongo wako kwenye CV/Resume watakuubua tuu na kazi ni at will, wanakufukuza saa yeyote na wewe unatoa notice wakati wowote , mimi nina kadiploma kangu ka bongo na vi short kozi kibao nacheza na wenye masters na niko top kwenye field lakini na uhakika nikirudi bongo hata computer operetar wataninyima so backwards
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Waambie uzoefu wako labda watafunguka na kuelewa, kwano wao ni kutundika mavbyeti ukutani kwao ndio uwezo. Nchi zilizoendelea wanachoangalia uwezo wako na wala si elimu yako. Utashangaa wewe na madigree yako unatolewa nje na mtu mwenye certificate tu, why ana elimu na ujuzi unaohitajika katika field yake, si elimu ya jumla jumla tu ya chuo Kikiuu.
   
 19. p

  poison Member

  #19
  May 28, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nilishajaribu walikuja Diaspora duu wanakwambia wanataka masters, huyo Dickson Maimu mwenyewe wanaojaribu kumsema huku alikua Treasury enzi hizo eighties , Mainframe Developer unacheza na Dump Terminals tuu, command line tuu hakuna GUI kama siku hizi ukitaka hata kusave file unaandika sentensi nzima ya Code, one of Smart guys ameandika systems nyingi tuu ndio hako ka vitambulisho, he can manage na kama ni kushika spanner kwenye Editor anaweza vilevile hamdanganyi mtu
   
 20. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mkuuu tafuta degree please.....


  Post kubwa kama huyo Maimu lazma uwe na elimu kubwa, hakuna longolongo hapo..... Hata hapo USA mtu kama Paneta ni shule kubwa, Prof...zz

  Hivi ugomv wa wasio na elimu na wenye elimu utaisha lini?? Haaaaaaaa
   
Loading...