Mtoto wa Mkulima
JF-Expert Member
- Apr 12, 2007
- 683
- 122
Jamani kuna mkasa umenipata nimeona niuweke hapa ili kama kuna watu wa TRA wausome na waache wizi.
Jamaa yangu amenunua gari zake mbili zilizotumika. Gari alizonunua ni Escudo gharama zilikuwa ni USD 4500 sasa kilichotokea alipoenda TRA jamaa wakamwambia kodi ni USD 4500. Tulipouliza wakasema sisi tumeangalia kwenye website gari kama hii ni USD 7000
import duty 1050
penalty 1050
VAT 1260
inspection 38.4
import declaration form 10
shipping line 60
port charges 67.2
handling 52
VAT ya port charges na Handling 23.54
Zote hizo ni dola si %
Kwanza kuna VAT mara mbili na sijui gharama zote hizo wanachukulia kwa % ngapi
Kuuliza vigezo wanavyotumia ni eti wanaenda online wanatafuta gari kama hiyo ya mwaka huo huo wanaangalia inauzwa bei gani eti
ndo maana invoice zetu hawaziweki maanani ila nimechukia sana mkuu. Huu wizi kabisa
Mdogo wangu niliwahi kumnunulia sale jamaa waliipiga kodi gharama ikazidi 120% ya CIF
Huu wizi kabisa mimi roho inauma sana maana hawa jamaa wanashindwa kukusanya kodi ya Madini na rasilimali zetu halafu wanakuja kuibia wananchi? Mimi sasa hivi mizigo napitishia Mombasa lakini roho inauma kwanini nisichangie hii pesa kwa nnchi yangu? Hii naamini ni watu wengi sana wanafanya hivyo na TRA wanapoteza pesa nyingi sana kwa hii kutaka cheap money.
Mimi nachotaka kusema Raisi wetu wala asihangaike kwenda nnje kutafuta wawekezaji, ni mfanya biashara gani atawekeza kwa mazingira kama haya? Nadhani badala ya kuhangaika na kupoteza pesa za walipa kodi bure angehangaika kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara. Bandari kama Dar bado inapotential nyingi sana za kukuza uchumi. Jamaa zangu wa Zambia huwa wanapeleka mzigo kupita Durban wanasema Dar kuna ukiritimba mwingi sana japo ni karibu.
Nimegundua sera ya kuzunguka kuwaalika wawekezaji haiwezi kufanikiwa kwa mtindo huu ni bora warekebishe mazingira ya nndani kwanza. Hakika ni vigumu kwa mwekezaji serious kuja kuwekeza kwa mazingira kama haya ya kwetu. Ila nawaomba watu wa TRA wawe wanatumia haki na akili badala ya mfumo huu wa sasa hivi ni wizi wa wazi kabisa.
IMENIUMA SANA WAZEE NDIO MAANA NIMEIWEKA HAPA ILI NANYI MJIONEE.