Culture Music Group na Bi Kidude: Mabalozi wetu ambao serikali haiwajali

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,546
847
Kusema ukweli mimi ni mbovu mbovu sana wa ORIGINAL TAARAB vikundi kama CULTURE,MALINDI,IKHWAN SAAFA au KIDUMBAK na wala si mpenzi wa MIPASHO kama Melody na TOT ambao

kusema kweli roho yangu imefajirika mno kupata hii link na hawa jamaa wanatuwakilisha vizuri sana kwa kweli. Of course CD yao niliiona VIRGIN STORE ni £15 na wazungu wananunua

Je kuna mtu anajua kwa nini hawa na BI KIDUDE hawajatambuliwa vilivyo na serikali kwa contribution yao katika kuendeleza utamaduni wetu?

hebu bonyeza hii link:

[mp3]http://content.digitalwell.washington.edu/isilon/1/8/8b/8b3e2d30-95b4-45e1-bccd-32e6e756b81b.mp3[/mp3]

Culture%20Musical%20Club2.jpg


Culture%20Musical%20Club1.jpg

yaani hapa ninamiss chai ya rangi iliyopikwa na karafuu tu

daym naanza kuwa home sick now. Its sad kwenye ziara yao ya Ulaya hawaji London na kusema kweli nini niko radhi kulipa hata £40 kwenda kwenye onyesho lao

anywa Ijumaa njema waheshimiwa

Culture%20Musical%20Club3.jpg


Culture%20Musical%20Club4.jpg


ZIFF-2002,-Herb-Fenstein-04.jpg


Culture%20Musical%20Club5.jpg


hivi kumbe bi ZUHURA kahamia CULTURE? Tangu lini?

This is a good move kwa kweli
 
Over a year ago.. niliona ni vizuri kama Serikali ingempatia Bi. Kidude Nishani ya Shaaban Roberts.. lakini kama ilivyo kawaida hadi watu wafe ndiyo "tuwaenzi" inapokuja...
 
Over a year ago.. niliona ni vizuri kama Serikali ingempatia Bi. Kidude Nishani ya Shaaban Roberts.. lakini kama ilivyo kawaida hadi watu wafe ndiyo "tuwaenzi" inapokuja...

yeah its sad, halafu hivi unajua kama CULTURE CLUB has been around since 1950's?

wazungu wanalipa top dollar kuwaona hawa jamaa....

halafu hiyo video yao ambayo wako SEATTLE ni priceless

MKJJ hebu ifanyie ufundi ieke kule kwenye website yao

yaani mimi hapa nilipo nasikiliza hivi vitu kuku na type na roho yangu imetulia tuliiiii

Unjaua kwa muziki kama huu unaweza kumchukua wife mkaenda kuwatazama bila wasi wasi wa kuwepo kwa nyimbo za matusi kama kwenye MIPASHO ndio maana nikasema hii ni TAARAB original

ama kweli muziki ni dawa!


http://www.seattlechannel.org/videos/video.asp?ID=4057
 
Over a year ago.. niliona ni vizuri kama Serikali ingempatia Bi. Kidude Nishani ya Shaaban Roberts.. lakini kama ilivyo kawaida hadi watu wafe ndiyo "tuwaenzi" inapokuja...

Nakubaliana na wewe kwa ujumla, kuwa Bi Kidude anatisha. Huku nje ya nchi huyu mwanamama ni maarufu sana na kila mara huwa nikiwaambia watu natokea Tanzania huwa wananiuliza sana habari za Bi Kidude.
Ni vyema kama serikali ingemtuza akiwa angali hai. COSOTA wangemfikiria kwa suala hili.
 
Naungana na waTZ wengine kuwa hawa ndo mabalozi wetu nje ya nchi, pia wanahitaji kupewa tuzo ya taifa.

Nawafanisha na hawa wa Cuba wajulikanao kama;
Buena Vista Social Club, na weshaingizia CUBA mamilioni.

Tatizo letu Watz ni kuwa kama hakuna ulaji hakuna hata kiongozi atakayewatazama mara mbili.
 
COSOTA ndio akina nani ?
Spoila, COCOTA ni Chama Cha Hakimiliki Tanzania (Copyright Society of Tanzania). Kazi yao ni kusimamia haki na kazi za wasanii Tanzania, ili kulinda haki zao. Pia wana kazi ya kunyoosha mambo katika sanaa mbali mbali (kufungia kazi za sanaa zisizofuata maadili)pamoja na kulipa mirahaba (loyalty) ya kazi za wasanii pale zinapotumika.

Mfano, wao inatakiwa walinde kazi za wasanii mbali mbali dhidi ya wanaonakili bila ruhusa, kutumia kazi ya msanii bila ruhusa na kudhibiti migongano ya kimaslahi dhidi ya wasanii (kuibiana kazi za sanaa). Wasanii kwa maana ya hapa ni kama vile wachonga vinyago, wapiga ngoma za asili, wanamuziki, wachoraji wa vikaragosi, waandikaji wa mabango nk. Pia kazi za watunzi wa vitabu, washairi na filamu nao hulindwa na taasisi hii.

Ila bado kwa nchi yetu taasisi hii haijaonyesha makali yake hasa, ingawa baadhi ya wamiliki wa kazi za sanaa wameshaanza kupata mafao yao ya mirahaba, kutokana na matumizi mbali mbali ya kazi zao. Bado hawajafanikiwa kudhibiti wizi wa kazi za sanaa.

Nadhani kwa ufafanuzi huu mdogo utaelewa maana ya COSOTA.

Kwa habari zaidi pitia tovuti yao katika (http://www.cosota-tz.org/frameset-t5.html)
 
Nimetune Clouds FM, Kipindi ni leo tena.

Nimetune hiki kipindi ili kumsikiliza huyu mwanamama mwenye umri wa miaka 103 ambaye bado anafanya muziki licha ya kuwa na umri mkubwa namna hii.

Alichonifurahisha Bi Kidude ni kuongea ukweli kuwa yeye ni mlevi wa konyagi na pia anavuta sigara.

Amesema bangi hajawahi kuvuta maishani mwake mwote.

Wasanii wetu wa kizazi kipya, bangi kwao ndio kifungua kinywa chao.
 
Msanii Bi Kidude, bado yupo jukwaani?

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=iHVm41pYJCk&feature=related[/ame]


[ame]http://www.youtube.com/watch?v=1dxDpWq5H8Y[/ame]
 
Bi Kidude
Its time the curtains fall and leave the legend behind and you will be respected.
 
Wana Jamii Forum,

Bi Kidude, tales of a living legend, ni kitabu kilichoandikwa na Ali Saleh na wenzake. Kitabu hiki kilichojaa picha za bi Kidude, kinazungumzia maisha yake, kama anavyoyaeleza yeye mwenyewe, na jinsi anavyoelezea mila, desturi na tamaduni za wazanzibari. Kwa wale wanaotambua kazi zake na mchango wake katika kukuza sanaa nchini basi ni vema mkakipata kitabu hiki.

JMU
 
anaweza akadondokea huko jukwaani ..naona kama ni muda muafaka kwake kupumzika
 
anaweza akadondokea huko jukwaani ..naona kama ni muda muafaka kwake kupumzika

Haya unayoyasema wewe, alishauriwa hivyo tangu miaka 30 iliyopita tena wakamwambia aache sigara ingemuua ndani ya miaka mitano tu. Mpaka sasa anadunda na fegi anapiga mtindo mmoja. Na mwaka huu anagombea urais. Kura yangu anayo.
 
Haya unayoyasema wewe, alishauriwa hivyo tangu miaka 30 iliyopita tena wakamwambia aache sigara ingemuua ndani ya miaka mitano tu. Mpaka sasa anadunda na fegi anapiga mtindo mmoja. Na mwaka huu anagombea urais. Kura yangu anayo.

hahahah heheheh umenifurahisha mpendwa
siku njema
 
Haya unayoyasema wewe, alishauriwa hivyo tangu miaka 30 iliyopita tena wakamwambia aache sigara ingemuua ndani ya miaka mitano tu. Mpaka sasa anadunda na fegi anapiga mtindo mmoja. Na mwaka huu anagombea urais. Kura yangu anayo.


Na VALUE-a brand whisky-kama kawa
 
Back
Top Bottom