CUFwanasiasa gani baada ya uchaguzi wa marudio

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Ni vyema tukajadili msimamo wa CUF kutokuitambua Serikali ya Zanzibar baada ya chama (kwa shinikizo la Maalim Seif) kususia uchaguzi wa marudio:

1) CUF hawaitambui Serikali, kwa mjibu wa maazimio ya Chama.

2) Wanachama ni Wazanzibari wakazi na wasio wakazi wakipata huduma zote za serikali!

3) Katibu wa chama, ni makamu wa kwanza wa Rais mstaafu anaendelea kulipwa stahili zake na serikali asiyoitambua!!!

4) Nafasi ya chama kikuu cha upinzani katika kuipa changamoto iko wapi, au chama kibaibgia mstuni!!

5) Wanachama waliotaka uongozi wako wapi na wanaichukuliaje hali hii ya sintofahamu chamani kwao!

Ni mawazo tu, kwenu wanajamvi.
 
Mleta mada unaitazama CUF kwa jicho moja la Zanzibar unasahau Muungano. CUF ipo na itaendelea kuwapa.

Sijui ulitaka Wafanyeje sasa kama unashiriki siasa ambazo watu hawako tayari kukubaliana na matakwa ya wananchi walio wengi kwa kung'ang'ania dhana ya historia na hawako tayari kupokezana madaraka kwa amani kisa tu wao waliingia kwa kupindua.

Njia nzuri na ambayo WaTz wengi hawaitaki na hawakuizoea ni ya kuingia msituni lakini bahati nzuri kwa watawala ni kuwa nchi na wananchi hawako tayari
 
Umenena sahihi, ngoja tusubiri wanajamvi wengine. Njia ya amani na kistaarabu ni kumweka kiongozi kwa njia ya kura, ambayo ni demokrasia.
 
Umenena sahihi, ngoja tusubiri wanajamvi wengine. Njia ya amani na kistaarabu ni kumweka kiongozi kwa njia ya kura, ambayo ni demokrasia.

Kwa wana Lumumba hiyo ni ndoto kwao madaraka ni ccm kushinda na si vinginevyo Angalia hata masuala madogo madogo ya umeya ndio utaijua rangi halisi ya ccm
 
Back
Top Bottom