CUF Zanzibar yamtaka Prof. Lipumba kujiondoa ili kukinusuru chama hicho

G-Mdadisi

Member
Feb 15, 2018
66
125
WANACHAMA na viongozi wa chama cha Wananchi CUF Zanzibar wamemtaka kiongozi wa chama hicho Prof. IBRAHIM LIPUMBA kuwaachia chama Chao ili kukinusuru na hali mbaya inayokikabili kutokana na kile walichokiita 'Usaliti wa Lipumba kwa chama hicho'.

Wamesema kutokana na mwenendo wa vitendo vyake vyenye kila dalili za kukihujumu chama chao kwa makusudi imefika wakati anatakiwa kuondoka ndani ya chama kwa namna yoyote ile ili chama kiendelee na utekelezaji wa agenda zake za kutetea masrahi ya wananchi kwa mujibu wa katiba.

Bullycheka

JF-Expert Member
Dec 15, 2016
558
500
Cuf ni mali ya lipumba Kama wao wamechoka tunawakaribisha Act -wazalendo
Miongoni mwa wanasiasa feki huyu professor Pumba ni moja wapo, sijui huo usomi wake aliupataje huwa anajidhalilisha sana ,tena ni mlaini kununuliwa hata rejareja. Kadri siku ziendavyo mtazidi kumjua sie tulishamuona hata kabla ya walio nae wengine hawajazaliwa, miaka ile ya 1990 enzi za James Mapalala huyu hakuwa MTU wa kuamini hata one second!!!
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
172,379
2,000
WANACHAMA na viongozi wa chama cha Wananchi CUF Zanzibar wamemtaka kiongozi wa chama hicho Prof. IBRAHIM LIPUMBA kuwaachia chama Chao ili kukinusuru na hali mbaya inayokikabili kutokana na kile walichokiita 'Usaliti wa Lipumba kwa chama hicho'.

Wamesema kutokana na mwenendo wa vitendo vyake vyenye kila dalili za kukihujumu chama chao kwa makusudi imefika wakati anatakiwa kuondoka ndani ya chama kwa namna yoyote ile ili chama kiendelee na utekelezaji wa agenda zake za kutetea masrahi ya wananchi kwa mujibu wa katiba.

Analindwa na wasiojulikana..na kwa malengo maalum...HATOKI
 
Babu Ochu

Senior Member
May 30, 2021
147
500
Lipumba alitumiwa sana kuihujumu CUF na Marehemu Self,kwa ahadi kedekede toka kwa "mtawala" na washauri wake
Rejea sarakasi za mahakama,na msajili dhidi ya Maalimu,na mwishowe akaishia kupata ile ruzuku .Ruzuku sasa imeisha na genge lake likiongozwa na Abdul Kambaya na David Maphone wameanza kumkimbia
Chama kimebaki jina tuu
 
careenjibebe

JF-Expert Member
May 28, 2020
1,222
2,000
WANACHAMA na viongozi wa chama cha Wananchi CUF Zanzibar wamemtaka kiongozi wa chama hicho Prof. IBRAHIM LIPUMBA kuwaachia chama Chao ili kukinusuru na hali mbaya inayokikabili kutokana na kile walichokiita 'Usaliti wa Lipumba kwa chama hicho'.

Wamesema kutokana na mwenendo wa vitendo vyake vyenye kila dalili za kukihujumu chama chao kwa makusudi imefika wakati anatakiwa kuondoka ndani ya chama kwa namna yoyote ile ili chama kiendelee na utekelezaji wa agenda zake za kutetea masrahi ya wananchi kwa mujibu wa katiba.

Juzi nilikua tanga nikaambiwa ile redio mwambao ambayo cuf wanaimiliki na alikua akiisimamia kambaya kwasasa ipo chini ya mama nuru na kwamba kambaya si lolote si chochote tena ndani ya cuf heehee nasikia chama sahivi hakina hela kila mtu kaenda njia yake kabak lipumba na sakaya tu yaan upinzani wa nchi hii jaman? Sasa huko zanzibar napo kuna cuf gan hata wajitutumue kumuondoa mwenye nyumba??

Nasikia ACT napo pamegawanyika vibaya mnoo kuna bara na kuna zanzibar kuna ACT chadema na ACT cuf..
Chadema nao ndo hao kila mtu analake sahiv...
Tusubir tu kipindi cha uchaguz kuibuke chama kipya chenye nguvu mpya
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom