CUF yawasha moto Z’bar

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482

Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, kimesema hatima ya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili iko mikononi mwa Wazanzibari wenyewe hivyo wasikubali kudanganywa.

Katibu Mkuu wa CUF Taifa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara ambao uliandaliwa na chama hicho, Kaskazini Unguja.

Alisema mamlaka ya Zanzibar ni jambo muhimu ambalo halipaswi kupuuzwa na Wazanzibari hivyo kia mmoja anapaswa kuipigania haki hiyo.

Kwa upande wake,aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe samaki, Bw.Mansour Yussuf Himid(CCM), aliwataka vijana visiwani humo kuongeza mapambano ili kudai mamlaka hayo bila kurudi nyuma.

Alisema ili mapambano hayo yaweze kufanikiwa, vijana wote visiwani humo bila kujali tofauti za vyama vyao wanapaswa kuwa kitu kimoja katika mapambano hayo.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano,Bw.Nassor Moyo, aliwataka Wazanzibari wasikubali kudanganywa kwani wakati Zanzibar inatafuta uhuru wake, haikutegemea kupata usaidizi kutoka kwa Tanganyika.

"Vijana piganieni uhuru wenu... sisi hatukupigania uhuru wetu kwa kutege mea kusaidiwa na Tanganyika,uchumi wetu ulikuwa karafuu na mbata," alisema Bw. Moyo.

Aliongeza kuwa, wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, zilikubaliana mambo 11 na kuyaweka katika kikapu kimoja sasa kite ndo cha Zanzibar kudai mamlaka kamili iweze kujiendesha yenyewe ni jambo muhimu lisilopaswa kuhojiwa.

Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar,Bw. Edi Riyami,alisema uraia wa Zanzibar hauwezi kujadiliwa na wako tayari kufa lakini wapate uraia wao.

"Uraia wa Zanzibar hauwezi kujadiliwa, tuko tayari tufe lakini tupate uraia wetu, tulitoka mbalihadi kufikia hapa tulipo sasa leo hii kwa nini uraiawetu ujadiliwe," alisema Bw. Riyami.

Katika mkutano huo, wanachama 459 kutoka vyama vingine vya siasa Wilaya ya Kaskazini A, walijiunga na CUF.

Kabla ya mkutano huo, Maalim Seif aliweka mawe ya msingi matawi ya chama hicho yaliyopo Kinyasini, Kiganja, Chaani Kubwa na kupandisha bendera za chama hicho.

Pia Maalim Seif aliweka jiwe la msingi ili kuanza ujenzi wa Ofisi ya Kikundi cha Ushirika wa Ketwa Chaani na kukabidhi sh. 300,000 kwa kikundi hicho, kuahidi mabati ya kuezekea na kutoa mabati 51 kwa madrasa ya watuwazima iliyopo Kinyasini, wilayani humo.
Chanzo: Majira
 
Na sisi wengine wa bara tunapenda mjitenge hatuwataki mnatunyonya tu na tuongeazea mzigo.
 
Mke akikuchoka mwache aende zake
Mke mwenyewe ushamlala wee for 50 years, amezeeka, masikini, malaya, mbea, ana gubu, mdini, gaidi
Chama Cha Mizigo kina-bore
Let Z'bar Go!
 
Wazanzibar waachwe waende, tumechoka tabia ya kisiwa kutawala bara, kina nahodha na shein wamepewa vyeo kwenye serikali ya muungano kwa kupunguza msuguano wa wagombea urais uzanzibar!
 
Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, kimesema hatima ya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili iko mikononi mwa Wazanzibari wenyewe hivyo wasikubali kudanganywa.

Katibu Mkuu wa CUF Taifa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara ambao uliandaliwa na chama hicho, Kaskazini Unguja.

Alisema mamlaka ya Zanzibar ni jambo muhimu ambalo halipaswi kupuuzwa na Wazanzibari hivyo kia mmoja anapaswa kuipigania haki hiyo.

Kwa upande wake,aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe samaki, Bw.Mansour Yussuf Himid(CCM), aliwataka vijana visiwani humo kuongeza mapambano ili kudai mamlaka hayo bila kurudi nyuma.

Alisema ili mapambano hayo yaweze kufanikiwa, vijana wote visiwani humo bila kujali tofauti za vyama vyao wanapaswa kuwa kitu kimoja katika mapambano hayo.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano,Bw.Nassor Moyo, aliwataka Wazanzibari wasikubali kudanganywa kwani wakati Zanzibar inatafuta uhuru wake, haikutegemea kupata usaidizi kutoka kwa Tanganyika.

"Vijana piganieni uhuru wenu... sisi hatukupigania uhuru wetu kwa kutege mea kusaidiwa na Tanganyika,uchumi wetu ulikuwa karafuu na mbata," alisema Bw. Moyo.

Aliongeza kuwa, wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, zilikubaliana mambo 11 na kuyaweka katika kikapu kimoja sasa kite ndo cha Zanzibar kudai mamlaka kamili iweze kujiendesha yenyewe ni jambo muhimu lisilopaswa kuhojiwa.

Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar,Bw. Edi Riyami,alisema uraia wa Zanzibar hauwezi kujadiliwa na wako tayari kufa lakini wapate uraia wao.

"Uraia wa Zanzibar hauwezi kujadiliwa, tuko tayari tufe lakini tupate uraia wetu, tulitoka mbalihadi kufikia hapa tulipo sasa leo hii kwa nini uraiawetu ujadiliwe," alisema Bw. Riyami.

Katika mkutano huo, wanachama 459 kutoka vyama vingine vya siasa Wilaya ya Kaskazini A, walijiunga na CUF.

Kabla ya mkutano huo, Maalim Seif aliweka mawe ya msingi matawi ya chama hicho yaliyopo Kinyasini, Kiganja, Chaani Kubwa na kupandisha bendera za chama hicho.

Pia Maalim Seif aliweka jiwe la msingi ili kuanza ujenzi wa Ofisi ya Kikundi cha Ushirika wa Ketwa Chaani na kukabidhi sh. 300,000 kwa kikundi hicho, kuahidi mabati ya kuezekea na kutoa mabati 51 kwa madrasa ya watuwazima iliyopo Kinyasini, wilayani humo.
Chanzo: Majira
kwa hiyo hoja ya mgombea wa mwaka 2015 kutoka Zanzibar imekufa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom