CUF yawanasa live CCM wakinunua vipande vya kupigia kura BUBUBU

Kaka zomba utanivunjia TV yangu bure na uwezo wa kununua nyingine sina. nitakutolea copy nikutumie mkuu uangalie ukiwa kwako

Njoo basi na kopi tuangalie kwangu. Utapendelea nikutayarishie nini? bisi za siagi? Gahwa na kashata? au crisps za muhogo kwa ukwaju na pilipili? ooooh, jirani yangu wanauza bajia nzuri za kunde kwa chatni ya machicha ya nazi na pilipili kichaa, labda utapendelea hiyo?
 
Njoo basi na kopi tuangalie kwangu. Utapendelea nikutayarishie nini? bisi za siagi? Gahwa na kashata? au crisps za muhogo kwa ukwaju na pilipili? ooooh, jirani yangu wanauza bajia nzuri za kunde kwa chatni ya machicha ya nazi na pilipili kichaa, labda utapendelea hiyo?
kaka zomba Gahawa na Kashata bila kusahau Pilau na ndizi mbivu na Chachandu kwa wingi juice ya miwa isikosekane
 
Last edited by a moderator:
haya magamba yashalaaniwa. Kote kote ni kuiba tu. Wake za watu, kura, madini.
 
hivi kwanini CHADEMA hawakushiriki uchaguzi wa bububu, au kwa kuwa huko hakuna makanisa? jussa alisema kweli.
Ku-deal na Waislam kama wewe na "Sheikh Ponda Mali Kifo chaja" is wastage of time! CDM wants to use every second effectively, not to waste any single minute like at Bubu-bu constituency!
 
Mahoka...serikali yailalamikia serikali, wapi na wapi! Raisi na Makamu wake wadhulumiana, msuluhishi atoke wapi?
 
Jamani tunaposema CUF mjue kuwa sisi sote ni ndugu tatizo ni CCM hamtuelewi sasa angalieni jangwani juzi mlizindua operation mnawashutumu chadema mnawaacha magamba ili mradi tu mwaondolee chadema imani kwa watu wasiokuwa na vyama waone siasa ni malumbano ama kwa uchu wa kuona chadema imewazidi mi nawambia kama hamjafunga ndoa na ccm mjiunge na chadema msiwe na uchu ama chuki kuwa chadema imewapiku LA SIVYO hapa hata mkilalama vipi kuhusu CCM sisi tunasema WALLAH hii ni vita ya BIBI NA BWANA ...WAKIGOMBANA NYUMBANI WAACHE WENYEWE MPAKA WATAELEWANA
 
Tanzania bwana ni nchi safi. Polisi wananyang'anywa kazi yao ya kulinda wanaona sawa tu!!!! Matukio haya yana maana kubwa sana kwa mustakabali wa nchi hii: Au polisi wenyewe wanajua hawafanyi kazi yao sawasawa na hivyo akijitokeza mwenye tija zaidi wanampisha kiulaini sana, au polisi wenyewe hawapende dhuluma wanayofanyiwa vyama vingine na hivyo wako upande wao wanawaachia wajilinde ndo watakuwa salama vinginevyo NAPE atawaagiza wawapore hata kura zao...!!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom