CUF yawanasa live CCM wakinunua vipande vya kupigia kura BUBUBU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF yawanasa live CCM wakinunua vipande vya kupigia kura BUBUBU

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Duble Chris, Sep 15, 2012.

 1. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  • Wamkamata muuzaji.
  • Mgombea (Bhaa), walinzi wake na dereva watimua mbio

  Jana tarehe 14/9/2012 ikiwa zimebaki siku mbili kabla ya siku ya upigaji kura kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu, CCM wanaonekana kutegemea rafu na michezo michafu kama mtaji wa kutafutia ushindi.

  Kikosi Maalum cha Operation na mipango ya Uchaguzi wa Bububu cha CUF kilipokea taarifa jana kiasi cha saa 2 usiku kutoka kwa mmoja ya wanafamilia ambae baba yake mzazi alikataa katakata kumuuzia Mgombea wa CCM (Bhaa) kipande chake cha kupigia kura kwa thamani ya shilingi laki moja.

  Baada ya kupokea taarifa hizo, kikosi hicho Maalum kilianza operation yake ya kumsaka kila kipembe mgombea wa CCM na wenzake ambao kwa usiri na ustadi mkubwa walikuwa kazini kununua vipande vya kupigia kura. Mara taarifa kuhusu sehemu ambayo zoezi la kununua vipande vya kupigia kura linaendelea ilipatikana.

  Gari la CUF lenye kikosi hicho Maalum lilivamia kwa ghafla eneo la tukio kiasi cha saa 5 na dakika kadhaa usiku na kumfuma mgombea wa CCM, mlinzi wake na dereva wakiwa wote wamesimama pembeni ya gari lao wakiendelea kupatana mpiga kura kura (jina linahifadhiwa) ili kununua kipande chake.

  "Vamia, kamata wote, haraka haraka, piga picha piga picha, watie katika gari!!" Kauli ya kamanda wa kikosi hicho maalum ilisikika. Kishindo hicho cha ghafla kiliwashtua wote waliokuwa wakiuziana vipande vya kupigia kura na kupatwa na mfadhaiko mkubwa wakiwa hawaamini kinachotokea.

  Mgombea wa CCM, mlinzi wake na dereva kwa haraka mno walijilenga katika gari , wakawasha na kukimbia huku wakimuacha mteja wao peke yake akifadhaika na kujikuta mikononi mwa wana operation wa CUF. Haya yakitendeka mpiga picha maalum wa operation hii akiendelea na kazi yake. Kijana huyo aliingizwa katika gari la CUF na kuelekea kituo cha Polisi. Hata hivyo baada ya kusikiliza maelezo ya mpiga kura huyo, wana operation wa CUF walimsamehe na kumpa onyo kali.

  CCM wamefadhaika na hawana imani wala matumaini ya kuweza kuutumia mchezo wao wa wizi wa kupigisha kura kumi kumi na kuleta watu kutoka maeneo mengine kuja kupiga kura. CUF wameapa kumkata kichwa mtu yeyote atakaethubutu kusogea kituoni kwa ajili ya kupiga kura na ilhali si mpiga kura wa jimbo hilo.

  Jambo hili limewatia hofu wapiga kura hewa waliopangwa kwa kazi hii wakiwemo wale waliotumika kusaidia kuiba jimbo hilo katika uchaguzi wa 2010. Vijana hao kutoka nje ya Bububu wanaohofia kupoteza maisha yao wamekataa kata kata kusogea kituoni kwa ajili ya kusaidia wizi wa jimbo hilo.

  Baada ya kufeli kwa mikakati iliyozoeleka CCM sasa wameamua kuupa nguvu kubwa mpango wa kununua vipande vya kupigia kura. Kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa kwa ajili kufanikisha ununuzi wa vipande vya kupigia kura kwa bei ya shilingi laki moja kwa kipande kimoja. Uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu unatarajiwa kufanyika kesho Jumapili tarehe 16/09/2012, huku kampeni za CUF zikifungwa rasmi leo na Mwenyekiti wa CUF Taifa Mhe Profesa Ibrahim Haruna Lipumba.


  [​IMG][​IMG]

  CHANZO:
  Mzalendo.net
   
 2. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hahahahaha! MAGAMBA bhaaaana!
   
 3. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Magamba na CUF, tunajua walishafunga ndoa kitambo, sasa kuna shida gani?
   
 4. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  wakuu hii imekaaje tena ya kukata watu vichwa naomba tuijadili nayo. Hivi huko wenzetu hawana sheria ????
   
 5. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Sijui nitumie lugha gani ili nieleweke bila BAN. Ukweli ni kwamba ukiona mke wako anagombea sahani la pilau na wewe kisha anagundua mbinu zako za kutaka kumzidi vinyango za nyama ujue kakuchoka na hana jinsi la sivyo angekupa taraka... Ukizingatia ndoa yenu ni matokeo ya shinikizo kutoka kwa walezi wako na wa mkeo kwani wazazi Mzazi wako amekufa na wa mkeo yu hai.
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Pumba tupu, hakuna mchele.
   
 7. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,454
  Trophy Points: 280
  Zomba kwani vipi, ina maana kati ya CUF na CCM wewe uko upande gani? LOL
   
 8. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,454
  Trophy Points: 280
  Saafi sana CUF! Yaani hapo mmeandelea kuwaumbua hawa mumiani wa siasa za Tanzania.

  Ila kwa nini msijitoe kwenye ile nanihi.... yenu? Si mnawaona walivyo mafidhuli lakini?
   
 9. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,454
  Trophy Points: 280
  Huo mfano ni mzuri na sahihi (relevant) katika context ya siasa za Tanzania.
   
 10. K

  Kibagata JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Tendwa msajili wa vyama FUTA CCM kwa rafu hizo maake kinahatarisha amani visiwani Zanzibar. maake wameanza kutishiana kukata vicbwa hi hatari kwa msitakabari wa Taifa.
   
 11. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  CUF na CCM ni mtu na nduguye hakuna ushindani hapo! Wao wa Unguja sisi Wabara....teh..teh! kila mcheza kwao.....
   
 12. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unaogopa kukatwa kichwa AU unaogopa kuwa sasa watu wanajua kuwa chama chako ni cha kukata watu vichwa?
   
 13. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  hii ndio dawa ya ccm iliyobaki wakiiba chinja finish job! hata huyu raia aliyeshikwa akiuza kipande angekatwa hata vidole viwili ili ajifunze!!
   
 14. C

  CUF Ngangari JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi kwanini CHADEMA hawakushiriki uchaguzi wa bububu, au kwa kuwa huko hakuna makanisa? jussa alisema kweli.
   
 15. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  kaka zomba nataka niwahi nyumbani nikaangalie ile filamu ambayo inawafanya muwe vichaa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Hivi mke anaweza kumkamata mume kwa sababu mume anadokoa mboga jikoni ??
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Umeipenda na unarudia kuiangalia au ndio mara ya kwanza kwenda kuiangalia?
   
 18. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #18
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  mara ya kwanza nimeipata kwa rafiki yangu
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nikaribishe na mie nije tuone pamoja.
   
 20. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kaka zomba utanivunjia TV yangu bure na uwezo wa kununua nyingine sina. nitakutolea copy nikutumie mkuu uangalie ukiwa kwako
   
Loading...