CUF yatumia UKAWA kufanya mkutano wake - Tabora

May 20, 2014
31
0
Chama cha CUF kimepita mtaani kikitangaza kuwa kutakuwa na mkutano wa UKAWW leo Jumapili saa 10.

Nimefika mapema nikakuta bendera za CUF na maneno haki yakitawala pale.

Naomba nisaidiwe kama ni sahihi kutumia UKAWA kuitisha mkutano.

Sina nia mbaya ila nataka kujua makumbaliano ya UKAWA yanaruhusu kuitisha mkutano wa chama kutumia kupitia UKAWA.

Nawasilisha waungwana.

Tuchangie kwa maneno ya busara.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,679
2,000
Sioni tatizo. Hata wana-CCM ambao ni au wangependa kuwa members wa Ukawa ruksa kuitisha mikutano kwa mwamvuli wa Ukawa. La msingi malengo yao yaoane na yale ya Ukawa.

"... Kisha wakamwambia, Bwana, tuliona wengine wakihubiri lakini hawafuatani nasi tukawakataza. Akawaambia, msiwakataze, maana asiye kinyume chetu yu upande wetu ...".

Mkuu, la msingi, ni nia, malengo, na kinachohubiriwa; ingeleta mashiko kutuambia tuliwasikia CUF Tabora wakihutubia mkutano wenye amudhui kinyume na Ukawa kuliko kutuambia wameitisha mkutano kwa jina la Ukawa. Waache waendelee, ni ndugu na Ukawa.
 
Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,005
2,000
Uzi huu, ni sura tofauti tu ya ajenda yenu ileile ya kuleta fitina ili kuubomoa UKAWA. Mbinu zenu zote hizi, haziwezi kufanikiwa. Umoja huu umeshuka kutoka kwa Mungu, hakuna mtu yeyote CUF, CHADEMA, NCCR wala CCM ambaye kabla ya kuanza kwa Bunge Maalum la Katiba, Jumanne 18.2.2014; angeweza kuwaza kwamba CUF,CHADEMA,NCCR wanaweza kuwa na umoja wa kiasi hiki, ukizingatia kwamba vyama hivi vilikuwa na mikwaruzano mingi kati yao. Ni kazi ya Mungu mwenyewe, ili kuwakomboa Watanzania kutoka katika ukoloni mamboleo wa CCM. Kazi ikitoka kwa Mungu, hakuna anayeweza kuivunja! Hivyo Interahamwe jiandaeni tu kisaikolojia, kuyapokea mambo ambayo UKAWA itawalazimisha kuyakubali hivi karibuni, mpende, msipende!
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
chama cha cuf kimepita mtaani kikitangaza kuwa kutakuwa na mkutano wa ukawa leo jumapil saa 10. lakini nimefika mapema nikakuta bendera za cuf na maneno haki yakitawala pale,naomba nisaidiwe kama ni sahih kutumia ukawa kuitisha mkutano.sina nia mbaya ila nataka kujua makumbaliano ya ukawa yanaruhusu kuitisha mkutano wa chama kutumia kupitia ukawa.nawasilisha waungwana.tuchangie kwa maneno ya busara.

CUF nayo ni sehemu ya UKAWA. Katika makubaliano hakuna kipengele kilichosema ni lazima kusanyiko liwe na vyama vyote. Kama walioitisha mkutano ni kati ya wanaUKAWA na kama wanachoongelea ni ndani ya wanachofanya UKAWA then ni halali kabisa.

Vinginevyo huwezi kusema Juma anaenda sokoni, halafu ghafla ulalamike miguu ya Juma inatingishika!
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Cha msingi maudhui yawe yaleyale ya Ukawa! Hapo tabora ukawa waende zaidi vijijini kutoe elimu ya uraia, huko ndiko ccm iliko taga.
 
Hakikwanza

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
4,019
2,000
Sioni tatizo. Hata wana-CCM ambao ni au wangependa kuwa members wa Ukawa ruksa kuitisha mikutano kwa mwamvuli wa Ukawa. La msingi malengo yao yaoane na yale ya Ukawa.

"... Kisha wakamwambia, Bwana, tuliona wengine wakihubiri lakini hawafuatani nasi tukawakataza. Akawaambia, msiwakataze, maana asiye kinyume chetu yu upande wetu ...".

Mkuu, la msingi, ni nia, malengo, na kinachohubiriwa; ingeleta mashiko kutuambia tuliwasikia CUF Tabora wakihutubia mkutano wenye amudhui kinyume na Ukawa kuliko kutuambia wameitisha mkutano kwa jina la Ukawa. Waache waendelee, ni ndugu na Ukawa.

Jibu murua kabisa
 
Centrehalf

JF-Expert Member
Jun 9, 2013
509

excellent 100/100
 
bujash

JF-Expert Member
Aug 9, 2013
3,468

umemaliza kila kitu na ubarikiwe sana mkuu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom