CUF yatangaza 'vita' kupigania eneo la kiuchumi bahari kuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF yatangaza 'vita' kupigania eneo la kiuchumi bahari kuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Geza Ulole, Jan 7, 2012.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana-JF

  Nimejaribu kuskiiza hotuba ya Bwana Jussa (MB wa jimbo la Mji Mkongwe-Visiwani) na katika yoote aliyosema nimegundua kuna mapungufu yafuatayo haswa kwenye swala la mafuta! Sheria za kimataifa zinasema pwani inakuwa mali ya nchi kavu mpaka nautical miles 200 sasa tujiulize ukichukulia Pemba ambayo inasemekana pwani yake ya Mashariki ina mkondo wa mafuta kama anavyodai, ipo katika umbali gani toka pwani? Hebu tufikirie katika mazingira yaa Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili, Je hivi visiwa viwili vya Unguja na Pemba, je haviko ndani ya 200 nm za pwani ya Tanganyika (yaani overlapping the Tanganyika territorial waters)?

  Wakati mwingine wanasiasa wanapenda siasa za kutia ujinga ulio na hamasa na ushawishi kwa wananchi wakiwa wanajua fika kwamba kuna masuala yenye utata na majibu yake ni mazungumzo na makubaliano kupitia wataalam maana haya masuala si mageni katika ulimwengu huu na hayajaanza leo na hapa nchini mwetu pekee! Japokuwa huyu Mh amemtukana Mh Sitta (mwenye umri kama wa babake) ila ukweli unabaki palepale kama leo hii visiwa vinajitenga bado tutagawana (formula ikitengenezwa na wataalam ikizingatia pia ratio division ya resources inayotokana na vitu kama urefu wa pwani baina ya nchi zijazo mbili yaani Tanganyika na Zanzibar) na hivi visiwa mafuta yale yatakayogunduliwa iwe ya kikombe cha chai au cha kahawa ya muuza kashata au upawa wa muuza mafuta ya kupikia maana swala hili si rahisi namna ile kama linavyoelezwa na Bw Jussa bali ni suala zito na lenye kizungumkuti mkuu (a very contentious issue)! Namuomba Bwana Jussa apitie shared transboundary resources kama zile kati ya UK na Norway aone jinsi wataalam walivyokaa na kuandika formula ya kushiriki katika kula matunda ya mafuta yale! Asijidanganye ati yale ni mafuta ya Zanzibar (Waunguja na Wapemba) pekee bali yale ni mafuta ya hata Tanganyika (Wabara) maana visiwa hivi viwili vipo ndani ya nautical miles 200 zinazoongelewa na International laws of the Sea under special economic zones.

  Namshauri huyu jamaa aache kuwatia ujinga ama ujuha ama sintofahamu Wazanzibari wenzie na zile siasa za "chao ni chetu ila chetu si chao" maana mwisho wa siku itikadi hizi za kiradikali zitaleta vurugu toka kwa Watu wa Zanzibar kwa kutotambua ukweli ni upi baada ya kujazwa upuuzi wa propaganda! Ni haya tu ningependa wana JF tujue na tuwe macho na siasa za chokochoko na zenye kuleta jazba, ushabiki na uzandiki usio na punje ya akili bali ujuha mtupu!


  MY TAKE
  Naona hii habari inahusiana na hii topic tunaona hapa mama Tibaijuka ameenda kuomba mile 150 za ziada hii itafanya mile 350 toka pwani ya Tanzania kuwa chini ya Mamlaka ya JMT! Natumai Jussa anaona haya! Na ningependa ajibu kitu humu ndani kama ana hoja za maana tumjibu


  17th January 12
  Tanzania kuwasilisha ombi UN kuongezewa eneo la bahari
  Muhibu Said
  Tanzania imetangaza kuwasilisha maombi Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), jijini New York, nchini Marekani, kudai umiliki wa eneo la ziada nje ya maili 200 za Ukanda wa Kiuchumi Baharini (EEZ) katika Bahari Kuu ya Hindi, ili iweze kulifanyia utafiti zaidi kuhusu rasilimali zilizoko chini ya bahari kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.

  Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, rasilimali hizo ni pamoja na mafuta, gesi na madini.

  Eneo hilo linatokana na ongezeko lingine tena maili 150 na hivyo kufanya jumla ya mpaka hadi maili 350, ambazo ni sawa na kilomita 560 kutoka kwenye ‘baseline'.

  Waziri Tibaijuka alisema maombi hayo yanatarajiwa kupelekwa na jopo la wataalamu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na wajumbe wawili kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, litaongozwa na Waziri Tibaijuka.

  Alisema wanatarajia kuwasilisha andiko la utafiti wa kisayansi la kudai eneo hilo katika Shirika la UN Linaloshughilikia Mikataba Sheria za Baharini (UNCLOS) kesho na kwamba, baadaye Aprili, mwaka huu, watakwenda tena UN kutetea andiko hilo.

  Alisema baada ya kutetea andiko hilo huko UN, Kamisheni ya Masuala ya Baharini itafanya uamuzi kuhusu maombi yao na kwamba, anaamini hatua waliyoifikia watafanikiwa.

  Waziri Tibaijuka alisema kazi ya kukamilisha andiko hilo iliyoanza mwaka 2007 na kugharimu zaidi ya Sh. bilioni 5.2, imesimamiwa na wizara yake na tafiti zimefanyika kwa kutumia wataalamu kutoka sekta za ardhi, maji, mawasiliano, sayansi na teknolojia, sheria na wataalamu wa masuala ya baharini kutoka vyuo vikuu.

  NIPASHE
  http://www.ippmedia.com/frontend/functions/print_article.php?l=37564


  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Tibaijuka: Rep is mistaken [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 25 January 2012 22:51 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] digg

  [​IMG]Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development Anna Tibaijuka explains to journalists in Dar es Salaam yesterday Tanzania's move to seek extension of Exclusive Economic Zone. Right is the director of survey and mapping, Dr Selasie Mayunga. PHOTO | FIDELIS FELIX

  By Bernard Lugongo
  The Citizen Reporter
  Dar es Salaam. The minister for Lands, Housing and Human Settlements Development, Prof Anna Tibaijuka, has hit back at the private motion by Mji Mkongwe Representative Ismail Jussa, opposing the Union Government move on extension of Exclusive Economic Zone (EEZ).

  Tabling his motion on certificate of emergency, Mr Jussa told the House of Representatives that Zanzibaris were unhappy with the way the Union Government had handled the issues that needed a consensus between both Zanzibar and Union governments. He asked Island authorities to be bold in defending what they consider to be Zanzibar's interest.

  Upon her return from the United States where she presented application to the United Nations, seeking extension of the Extended Continental Shelf (ECS), which lies 150 miles beyond the current 200 miles of EEZ, Prof Tibaijuka yesterday said Mr Jussa's claims were "inappropriate".

  She said it was not correct that Zanzibar Government of National Unity did not participate in the exercise, but the fact was that leaders from the Isles took part and did effective job in a whole process. Also the UN Law on Marine Contract Acts, which was ratified in 1985, recognises the Union Government, which the Zanzibar Government is part of it.

  She said the Law was about UN member countries, and the Tanzania Mainland and Isles is one country.
  Under this context, implementation of the UN Law on Marine Contract Act was done on behalf of the United Republic of Tanzania, and Zanzibar being part of it.

  Exclusive Economic Zone was sketched out in 1982 and forwarded to the UN as part of United Republic of Tanzania. She argued that the identified marine zones should not be associated with issues of division of resources available within the area.

  "The issue of resources remains to be internal matter and not recognised by the UN," she said.
  She was responding to remarks by Mr Jussa, who argued in his motion that the Zanzibar House of Representatives had decided that marine and oil issues should be the preserve of Zanzibar and the Union government had no business making the application.

  Prof Tibaijuka added that her ministry was not responsible to division of resources within the country; therefore it was right to associate the issue of division of resources available in the ocean to the request for EEZ.

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  http://www.thecitizen.co.tz/news/-/19231-tibaijuka-rep-is-mistaken
   
 2. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  Jibu...ni kwa sababu na yeye ni mjinga!!!

  Mwaka Juzi Baraza la wawakilishi lilipata kumualika mtaalamu mmoja wa oil exploration baada ya kukamilika kwa zoezi la kutafiti upatikanaji wa nishati ya mafuta katika pwani ya zanzibar...mtaalamu aliwaambia wazanzibari pasi na kuuma maneno kuwa, 'mafuta yapo lakini si ya kuweza kuchimbwa commercially', maana yake nini, mafuta yaliyopo ni kidogo na ikiwa yatachimbwa basi hayatokuwa na faida kwa kuwa gharama za uchimbaji zingekuwa kubwa kuliko faida tegemewa.

  Lakini Wazanzibari kwa kuwa wameshadanganywa sana na wanasiasa wao wameendelea kujidanganya kuwa wana mafuta...hivi kweli kwa tafiti zote ambazo zimeshafanyika kama yangekuwepo, si yange kwisha anza kuchimbwa???

  Nnachokiona mkuu ni kuwa wanasiasa wanacheza na bongo za wapumbavu ili waendelee kuwatawala na bahati mbaya wapumbavu wameendelea kuwa hivyo basi hewala kwa wanasiasa.
   
 3. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #3
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kweli kuna tatizo kubwa sana kwenye vichwa vetu -waafrika.Ila hawa wanasiasa wa Zanzibar wanataka kuwagawa wananchi ila wapate madaraka.
   
 4. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Ni kijana sio mzeee
  ni bilionea zanzibari na oman
  ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa
  ana miliki visima kama mia vya mafuta tanzania bara na visiwani
  ana mijengo mikubwa oman nimesikia na uingereza
  ni mmoja wa vijana waanzilishi wa chama cha cuf


  huyu ni jusa ismail wa jusa

  nani anamtuma,wananchi,wafanya biashara wenzake,alqaeda,matajiri wa oman au cuf???
   
 5. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,171
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Wapemba na wajomba zao.
   
 6. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hilo ni swali la msingi sana, maana ni kwamba anatumwa si yeye maana hawezi
   
 7. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Ali shababu''
   
 8. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  hata mie nimekuwa nikijiuliza sana,nimefuatilia sana kauli zake nimetambua c bure,na hakuna mtu/kiongozi ndani ya chama ama serikali ya zanzibar ambayo nae yumo aliyesema chochote, kama ni kutumwa basi ni Seif(maalim) na Oman huko. lazima!
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,279
  Trophy Points: 280
  Yaani uwe na uswahiba na Rostam Aziz halafu uwe kapuku? wewe vipi bana!!
   
 10. T

  TUMY JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Jusa sio bilionea wala hana huo utajiri unaousema wewe wa kumiliki visima vya mafuta karibu mia tanzania bara na visiwani ni Tanzania hii tunayoifahamu kuna Tanzania nyingine.
  Sana sana Jusa anaonekana ni mtu asiye na mwelekeo na ambaye hana sera.
   
 11. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wazee musipate tabu bure Mh. Jussa anatumwa ni Wazanzibari hususan wale wazee na vijana wa CCM ambao wanauchungu na nchi yao ya Zanzibar, kwa sasa Wazee/Vijana hawa chango za uzazi zimewauma na wameshathibitisha kweli kama wakifanya masihara nchi yao itaenda arijojo lakini kutokana na jinsi wazee na vijana hawa walivyo na Usuhuba sana na jamaa zao wa Kitanganyika wamefika mahali hawawezi kujitokeza hadharani kuitetea nchi yao na badala yake wameamua kulitumilia hili JEMBE, na ndio maana huwajawasikia viongozi wa CCM wakipiga kelele sababu wao ndio wanamtuma aseme hicho anachokisema. Kwa upande wa CUF wao wanauwelewa wajibu wao kwa nchi yao tangu siku kilipoasisiwa chama chao.
   
 12. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  VATICAN, defintely!
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,279
  Trophy Points: 280
  Mambo ya wapemba hayanihusu, ni sawa na kushabikia siasa za Congo.
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Inavyoonekana si mtu wa kutumwa na mtu,
  ni mtu mwenye utashi na itikadi zaidi
  Siyo mtu wa kuburuzwa na mtu yeyote
  Ni mtu mwenye uwezo wa kifedha
   
 15. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  Jussa ni mtetezi wa nchi yake ya Zanzibar
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  kweli jusa kiboko.

  Magwanda wanamuhara.


  keep it up Jussa, mpaka kieleweke
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,279
  Trophy Points: 280
  Huyu ni Mzanzibar aliyepo ukimbizini Oman.
   
 18. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Takbiiiiiiir! Zanzibar Daima Mbeleeeeeee. Am proud to be Zanzibari.
   
 19. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Acha uzembe wa kufikiri, Jussa atawasumbua wanzanzibari wenzie(probabaly ukiwemo na wewe),
  Huku Tanganyika He is a tiny insect in the jungle..
   
 20. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yasahaulisheni matatizo yenu kwa kujikusuru na threads za Mh. Jussa hadi 2015 ifike wanaume waje wachukue waweke waaaaaa! Huku wakiwaacha nyinyi mukiandamana baadae wawaletee askari wawatawanye mupate kujificha katika maspeaker utadhani munacheza michezo ya kombolela!
   
Loading...