CUF yashangaa Dr.Salmin aliwafunga jela vipi Dr. Jakaya hafanyi hivyo kwa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF yashangaa Dr.Salmin aliwafunga jela vipi Dr. Jakaya hafanyi hivyo kwa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagamoyo, Mar 22, 2011.

 1. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,519
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  CUF walikuwa wanakataa kuwa wao siyo sehemu ya serikali lakini sasa wanatembea kila kona kuishindikiza serikali ya Jakaya Kikwete kuwasweka jela viongozi wa CHADEMA.

  Rashid Hamad aelezea masaibu yake ya kufungwa jela miaka mitatu kwa kutomtambua Dr. Salmin Amour mwaka 1997.
  • 1997 Salmin aliwaweka 18 wa CUF jela!
  • Vipi Jakaya Kikwete hawafungi jela wabunge wa CHADEMA!
  • CHADEMA ni kama dikteta Iddi Amin DADA!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa sababu walikuwa/ni mazuzu ndo maana wanakubali kuonewa
   
 3. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hawakujua wanasimsmia nini kwa sababu ya unafiki wao ndio maana walifungwa jela
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kweli umbumbumbu wa sheria ni kitu kibaya sana.... pole zao!!!:lol: Kwahiyo kwa sababu wao walifungwa ndo maana wakawa ma**ya wa kisasa!!:angry:
   
 5. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  kaazi kweli kweli!
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  nimekupa 5 mwanangu!
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hamad Rashid ni mwanasiasa mzuri sana anayejua kupanga karata zake. Ushauri huu anaompatia JK ni mzuri sana hasa kwa upande wa CUF ambao wamekuwa ni victim wa siasa za majungu tokea 1995 kabla ya kuamua kwa ridhaa yao kuwa if you can't beat 'em, join 'em. Na ku-surrender to the CCM oppression. Anajua kabisa kuwa JK akiwaweka ndani viongozi wa CHADEMA itakula kwake, yaani CCM itakuwa imejimaliza kuanzia ndani na nje ya nchi, hivyo kuwapatia CUF nafasi ya kung'ara na kueleza kuwa hata wao walionewa 1997.

  Katika upepo huu unaovuma kwa sasa hivi kitendo hicho kitaipatia Tanzania page kwenye vyombo vya magharibi na hivyo kufufua picha za CNN et al ambazo CUF walioneshwa wananyanyaswa miaka hivyo. Kwa wapensi wa demokrasia tusiomuone Hamad kama adui wa CHADEMA bali ni rafiki mkubwa kama ushauri wake utafuatwa na JK.
   
 8. markach

  markach Senior Member

  #8
  Mar 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mh! Upinzani wa kutafunana, sidhani kama tutafika. Ama kweli ccm ni wajanja, wanawatumia hao hao wapinzani kutafunana wenyewe kwa wenyewe
   
 9. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Chadema ni chama kisicho jua siasa ni nini! bali kinaonekana kuongozwa na watu Mbumbumbu!
  nasema hivyo sababu Wazanzibari wameamua kwa kupitia kura ya maoni kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa CUF na CCM kwa pamoja na wao CDM wanaubeza uamuzi huo wa Wananchi kwa kuwaita CUF kuwa ni CCM-B!!! hii maana yake nini? inamaana huko Uingereza chama Liberal kuunda Serikali ya Mseto na chama cha Conservative itakifanya Liberal kuwa ni Conservatibe-B?
  Au ODM ya Odinga tutaiita ni PNU-B ambayo inaongozwa na Kibaki? au chama cha Tvangirai huko Zimbabwe tutamuita ni ZANU-PF-B????

  Sasa wanazunguka kila kona kuwashawishi Wananchi waiasi Serikali! sasa waliingia kwenye uchaguzi kwa minajili ipi? Kutangaza kuwa Tanzania haitatawalika mpaka kieleweke maana yake nini?

  Mwisho nawashauri Chadema waende Bungeni kupigania maslahi ya Wananchi ndani ya Bunge na kama kazi hiyo imewashinda basi wajiuzulu kazi za Ubunge na waende Msituni kama alivyofanya Jonas Savimbi maana aliingia ktk uchaguzi na aliposhindwa hakuingia Bungeni na aliamua kuutafuta Urais kwa njia za mtutu!

  Tunawaomba CDM waache kutuyumbisha Wananchi, tunamatatizo kibao na hatutaki watuletee matatizo mengine mapya!
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tofauti CDM inaenda kwa nguvu ya Umma, wao ccm- B walikuwa viongoz wabinafsi waroho wa madaraka, wakibisha wamdanganye mkwere aweke mtu ndani waone nguvu ya umma ikoje. Hawakuona arusha?
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Guys, hii single ya CUF kuikandia CHADEMA na hivi sasa kupeleka dua kiangushwe kabisa hakika nimeipenda sana na kama sehemu ya serikali inayotawala hivi sasa madarakani basi nadhani yata-hit sana ikipelekwa kwenye kumbi za disco la siasa!!!
   
 12. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  aisee, kumbe kwnye hii nchi mambumbumbu mko wng! Pole mwaya da zubeda ila punguza jazba cz utapata kisukar na hali yko ya uchum huna hta naul ya kkfksha kw babu akpatie kikombe!
   
 13. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  mwambie kama hana nauli aniPM na yule Hamad rashid nataka niwapeleke kwa babu. Hamad bwn! Alaf eti anataka vyama vya Upinzani viwe na muungano! Wapi!!
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hebu jaribu kutazama miguu yako hiyo kama kweli haijaota tende kwa kudhubutu kudharau mwiba CHADEMA.
   
 15. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  nikimwanaglia hamad,namwona dhahiri kabisa anavoonekana kuishiwa nguvvu na kukosa raha kwa cdm kuchukua uongozi wa kambi ya upinzani bungeni nae kupigwa chini na chama chake cuf. the way i see, cuf hawatakuwa na siku nyingi to go. mfano ufanyike uchaguzi right now,bara hawapati viti zaidi ya kupokwa na hivyo viwili
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kwani cuf ni wapinzani? wao ni wing nyingine ya ccm kama vile uvccm
   
 17. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  amentoroka kwa aib! Maskin sa c ange2aga! Ucjal akiona hatar kuku Pm wewe atan Pm mm ntamsaidia cz anaumwa kwel kwel!
   
 18. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hamad Rashid anataka CDM Waonewe kama wao walivyoonewa na Komando,Wakumbuke komando alikuwa anajiendesha bila ya kukubali ushauri wa mtu mtu yeyote.KtK uongozi wake mambo mengi ya muungano yamevurugika hata ccm alikuwa tishio kwao.Aliifanya Zenj kuwa nchi akawatia ndani akina hamad rashid na wenzake akina duni.Alipoondoka madarakani akina msekwa ndo wakawa vinara wa kusema kwamba zanzibar sio nchi hivyo haiwezi kufanyiwa uhaini.Karume Jr kaingia kwa kuwasamehe watu wote walikuwa jela kwa sabab ya makosa ya siasa.Pamoja na wale watu wa tume ya uchaguzi ambao hawakupeleka kwa makusudi masanduku ya kura kituo kilichopo umbali mdogo na ofsi za tume ya uchaguzi huko unguja.Ushauri wa bure kwa cuf,ccm si wenzenu,wataendelea kuwa marais na nyie wasindikizaji mnapewa kile mnachokiita umakamo wa rais.Wamevutia ili waweze kuwachakachua vizuri zaidi manake hamtayakataa matokeo tena mtakuwa mnabembelezwa kwa mbeleko ya serikali ya umoja wa kitaifa halaf mnanyamaza kama watoti wadogo.Kama akina Hamad rashid walipotoka gerezani walibembelezwa kwa kupewa uwakilishi wakanyamaza.Kwa sasa hv watasahau hata ile kauli yao HAAAkiii! watakuwa wa Haaki-kidumu chama cha mapinduzi,oyeeyee
   
 19. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hamadi Rashidi anasumbuliwa na vitu 4 -

  1.wivu wa mafanikio kwa CDM (maana keshaona CUF inajifia day by day)
  2.Uzanzibar
  3.Udini (kumbukeni ile siku ya mdahalo pale kempisiky hotel
  4.Kukosa uongozi wa kambi ya upinzani bungeni

  Ila kubwa linalonisikitisha toka kwa huyu bwana na CUF yao kwa ujumla,wanasahau kuwa the most of watanzania bara'z wanaona CDM ndicho chama pekee kinachoonyesha upinzani wa kweli zidi ya CCM na ndiyo maana wakapata wabunge wengi kuliko hivyo vyama fake ikiwamo CUF. Ushauli wangu kwa CUF na CCM ni kuwa mnapoteza mda wenu bure kwa kuishambulia CDM!.....Hapa hakuna cha udini wala uhaini......Thiz time watanzania hatudanganyiki ng'o.....hadi kieleweke! Shame on u HR na mabashazenu ccm
   
 20. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hashakum si matusi da zubeda jaribu kushirikisha halmashauri ya ubongo wako unapokuwa unachangia kwa great thinkers! Hapo kwenye red kwani kenya au zimbabwe kuna muungano wa nchi 2 kama hapa Tanzania kwetu. Inakuwaje upande m1 unakuwa part ya chama tawala then upande mwingine ukawe mpinzani wa ukweli. Kumbuka tuna bunge la JMT ambalo linajadiri maswala yote ya bara na visiwani hivyo ni ngumu kwa CUF kuwa chama kimoja chenye sura mbili tofauti katika bunge moja la Jamuhuri ya muungano wa Tz. Tungekuwa na bunge la kujadili maswala ya Tanzania bara pekee basi CUF kingekuwa chama cha upinzani kama vyama vinginevyo katika nchi yetu. Acha siasa za ushabiki usio na tija kwa maendeleo ya watz.

  Tuliokipigia kura CDM tunakisupport kwa yote wewe ambaye hukukipigia kura shida yako nini si uwaambie uliowapigia kura wakupatie maisha ya ndoto waliyokuahidi.
   
Loading...