CUF yapokea wito wa Mahakama Kuu ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF yapokea wito wa Mahakama Kuu ya Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jan 16, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Hatimaye Chama cha Wananchi (CUF) kimethibitisha kupokea taarifa ya wito wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, inayowataka kufika mahakamani hapo Januari 19, mwaka huu, kujibu tuhuma za kukiuka amri halali ya mahakama.

  Amri hiyo ilitolewa na mahakama hiyo Januari 4, mwaka huu, saa 3.45 asubuhi.
  Amri hiyo ilizuia kikao cha Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa kufanyika hadi hapo kesi ya msingi iliyofunguliwa na Mbunge wa

  Wawi, Hamad Rashid Mohamed, na wenzake 10 itakaposikilizwa na kuamuliwa.
  Kikao hicho kilichofanyika siku hiyo, kiliwavua uanachama Hamad na wenzake hao na kuwavua uongozi wanachama wengine na wengine kupewa karipio kali.

  Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alihitbitisha kupokea taarifa ya wito huo wa mahakama.
  “Ni kweli tumepokea summons (hati ya wito wa mahakama) kutoka Mahakama Kuu. Tunapaswa kuhudhuria kwenye shauri tarehe 19,” alisema Mtatiro alipozungumza na NIPASHE Jumapili jana.

  Alisema shauri hilo limepangwa kutajwa siku hiyo na baadaye wapate nafasi ya kuwasilisha majibu dhidi ya maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Hamad na wenzake.
  Hamad na wenzake wameiomba Mahakama Kuu iiamuru Bodi ya Wadhamini ya CUF wajieleze ni kwa nini wasitiwe hatiani kwa kukiuka amri ya mahakama hiyo.

  Pia waliomba mahakama iamuru wajumbe wa Baraza Kuu, akiwamo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, wajieleze kwa nini wasitiwe hatiani kwa kukiuka amri hiyo.
  Vilevile, wanaiomba mahakama hiyo ibatilishe uamuzi wa Baraza Kuu wa kuwavua uanachama hapo Januari 4, 2012, kwa madai kwamba walikiuka katiba ya CUF.

  Kabla ya uamuzi huo wa kuwavua uanachama, Januari 3, mwaka huu, Hamad na wenzake waliwasilisha ombi Mahakama Kuu chini ya hati ya dharura wakiomba mkutano wa Baraza Kuu uliokuwa ukitarajiwa kufanyika Zanzibar, uzuiwe kuwajadili.
  Kupitia kwa mawakili wao, kampuni ya uwakili ya GF Law Chambers Advocates, walidai baraza hilo lina nia ya ama kuwasimamisha

  au kuwavua uanachama na kwamba uamuzi huo ungeathiri haki zao za kikatiba.
  Waliendelea kudai kwamba, kuna kesi ya msingi ya madai namba 1 ya mwaka 2012 waliyoifungua mahakamani hapo wakihoji

  muundo wa Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho na uteuzi wa wajumbe wa kamati hiyo.
  Uamuzi wa kuzuia kikao hicho cha Baraza Kuu, ulitolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Augustine Shangwa.
  Hamad alirejea amri hiyo ya Mahakama Kuu chini ya Jaji na kueleza kwamba CUF walikaidi na badala yake kuendelea na kutekeleza azma yake ya kuwavua uanachama.

  Mbali na Hamad, wengine waliofukuzwa uanachama CUF, ni Doyo Hassan Doyo, Shoka Khamis Juma na Juma Saanane, wote wakiwa wajumbe wa Baraza Kuu.
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Duh yale yale ya madiwani wa Chadema Arusha; keep watching the move.
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Dhambi ya kumuibia chama ndg. Mapalala itaendelea kuwatafuna.
   
Loading...