CUF yapendekeza Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama Zanzibar

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,750
139,545
Mwenyekiti wa CUF Prof Lipumba amemtaka serikali ya JMT iwe ya. Umoja wa Kitaifa kama Zanzibar

CUF Ilikuwa inawasilisha maoni yake mbele ya Kikosi kazi cha Profesa Mkandala na Zitto Kabwe.
===

Chama cha Wananchi (CUF) kimependekeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kama ilivyo Zanzibar.

CUF imesema hatua hiyo itatengeneza utulivu wa Taifa kama Zanzibar iliyopunguza uhasama tangu mwaka 2010 baada ya Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya 1984.

Marekebisho hayo yaliweka msingi wa kugawana madaraka kati ya mshindi wa uchaguzi mkuu na mshindi wa pili.

CUF imetoa mapendekezo hayo mbele ya Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia nchini, kinachoendelea.

Chanzo: Eatv
 
Huu ni wivu baada ya kuona makamanda wamekaribishwa kivyao na kuwaacha CCM B kwenye mataa
 
Chama cha Wananchi (CUF) kimependekeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kama ilivyo Zanzibar.

CUF imesema hatua hiyo itatengeneza utulivu wa Taifa kama Zanzibar iliyopunguza uhasama tangu mwaka 2010 baada ya Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya 1984.

Marekebisho hayo yaliweka msingi wa kugawana madaraka kati ya mshindi wa uchaguzi mkuu na mshindi wa pili.

CUF imetoa mapendekezo hayo mbele ya Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia nchini, kinachoendelea.

Nini maoni yako.
 
Mwenyekiti wa CUF Prof Lipumba amemtaka serikali ya JMT iwe ya.Umoja wa Kitaifa kama Zanzibar

CUF Ilikuwa inawasilisha maoni yake mbele ya Kikosi kazi cha Profesa Mkandala na Zitto Kabwe

Chanzo: Eatv
CUF wanawaza madaraka tu. Pamoja na Zanzibar kuwa na SUK, kuna nini cha zaidi kama siyo wanasiasa wamegawana tu vyeo na wananchi wamebaki na maumivu yao? Sisi tunakata katiba ya kutatua matatizo ya wananchi na siyo katiba ya kutatua matatizo ya viongozi kukosa uongozi!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom