CUF yapeleka wafuasi Arusha na mabasi kutoka Dar

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katika kuficha aibu kesho na kuiongopea dunia kwamba kinaungwa mkono Arusha,chama cha wananchi-CUF kimepeleka maelfu ya wafuasi wake kutokea Dar kwenda Arusha.Kwa mujibu wa shuhuda wetu amekutana na msururu wa mabasi yapatayo saba-7 yakiondoka Ubungo huku yakipambwa bendera za CUF na nyimbo za hamasa za wafuasi hao.
Wachunguzi wa siasa wanasema ni aibu kubwa kwa chama kusafirisha wafuasi umbali wa mwendo wa saa 10 kisa kujaza uwanja na kuhalalisha hila chafu dhidi ya vyama vingine.

Source:Facebook Wall Page-Mwasiwelwa Perfect.

603615_3796830481154_1104467570_n.jpg
 
Nami nimekutana na costa kama nne hivi zimepambwa bendera za Cuf maeneo ya Kimara. Ina maana zinaelekea Arusha? Basi kama ndo hivyo kudanganya kuna gharimu sana.
.
 
Cuf kwa hiyo wana tumia mbinu ya Ccmweli kubeba wafuasi!
 
mbona ni kawaida yao?
Hata siku ya kumpokea lipumba walikusanya watu pale temeke hospitali, wakawapakia kwenye mabus na malori kwenda kumlaki "sultani"........
 
Nami nimekutana na costa kama nne hivi zimepambwa bendera za Cuf maeneo ya Kimara. Ina maana zinaelekea Arusha? Basi kama ndo hivyo kudanganya kuna gharimu sana.
.

Ndiyo safari ya kuelekea Arusha hiyo.
 
mbona ni kawaida yao?
Hata siku ya kumpokea lipumba walikusanya watu pale temeke hospitali, wakawapakia kwenye mabus na malori kwenda kumlaki "sultani"........

Mkuu wangu kusafirisha watu Dar hadi Arusha kisa mkutano ni ujinga uliopitiliza.
 
Ni utaratibu wa chama chetuu!
Kwani hamjui siasa!
Nawengine watatoka tanga!
MWASHANGAA NII?
 
Sasa ili ukweli uje Juu naomba mtuwekee ili kuondoa utata mimi niko Himo nitangojea msafara na picha nitaweka kuanzia huko njiani wekeni ushahidi maaana wana unishi wale
 
Sasa ili ukweli uje Juu naomba mtuwekee ili kuondoa utata mimi niko Himo nitangojea msafara na picha nitaweka kuanzia huko njiani wekeni ushahidi maaana wana unishi wale

Ni jambo jema utakuwa umesaidia wadau.
 
Back
Top Bottom