CUF YAMEGUKA: Mtatiro amuita muasi anayekivuruga chama hicho - Hama Rashid | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF YAMEGUKA: Mtatiro amuita muasi anayekivuruga chama hicho - Hama Rashid

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Dec 14, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=2]14 DECEMBER 2011[/h][h=3]
  [/h]

  *Hama Rashid adaiwa kuwa chanzo cha vurugu
  *Mtatiro amuita muasi anayekivuruga chama hicho
  *Asema kama anataka madaraka afuate taratibu

  Na Godfrida Jola

  KUTOKANA na Mbunge wa Wawi, Pemba Bw. Hamad Rashid Mohamed kutajwa kuwa chanzo cha vurugu zilizosababisha baadhi ya wanachama kukatwa
  mapanga, Chama cha Wanachi (CUF) kimesema mbunge huyo pamoja na wale wanaomuunga mkono kuwa ni waasi wa chama.

  Viongozi wengine wanaotuhumiwa kuhusuka katika uasi huo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wilaya ya Handeni, Tanga Bw. Doe Hassan, Bw. Yassin Mrotwa wa Mbeya na viongozi wa Baraza la Kuu katika chama hicho.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu katibu Mkuu Bara Bw. Julias Mtatiro ikiwa ni siku moja baaada ya vurugu kutokea katika mkutano ulioandaliwa na mbunge huyo kwenye Tawi la Mabika lililopo katika Wilaya ya Kinondoni.

  Akizungumza na majira Bw. Hamad alisema kuwa, ni kweli Ofiosi Kuu haikuwa na taarifa kuhusu mkutano huo na kuongeza kwamba, pamoja na kutokuwepo kwa taarifa hiyo katiba inaruhusu viongozi wa matawi kuandaa mkutano bila kuhusisha Ofisi Kuu.

  Alifafanua kwamba, sababu kubwa ya kufika katika tawi hilo lililopo Mabibo katika Wilaya ya Kinondoni ilikuwa ni kwenda kufufua tawi baada ya kuombwa na wanachama kwa madai kwamba, walikuwa wametelekeza.

  "Nilikwenda katika tawi la Chechnia kwa lengo la kufufua tawi chama kwani waliniomba, pia walinitaka kuwapatia msaada wa sh. laki tatu lakini niliwapatia laki 2," alisema.

  Katika tukio hilo, ilielezwa kwamba vijana wa wa CUF maarufu kwa jina la Blue Gard walivamia mkutano huo ambapo vurugu zilianzia hapo.

  Katika vurugu hizo baadhi ya vijana na wanachama wengine walijeruhiwa vibaya kwa kuwa, vurugu hizo zilitawaliwa na mapanga pamoja na mawe ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mali ikiwemo gari la CUF ambali lilitobolewa matairi pia kupasuliwa vioo.

  Taarifa ziliarifu kuwa, sababu kuwa ya kuanza kuzuka kwa vurugu hizo ni kutokana na Blue Guard kufika eneo la tukio na kuanza kuhoji kufanyika kwa mkutano wa CUF bila Ofisi ya Makao Makuu kuwa na taarifa za mkutano huo kama ilivyo ada.

  Bw. Mtatiro alisema kwamba, Bw. Hamad amekuwa kinara na kuwa, zaidi sasa anaungwa mkono na na watendaji waliopunguzwa kazi katika ofisi kuu za chama hicho huku wakiwa na lengo la kukivuruga na kukigawa chama.

  Alisema kuwa, Bw. Hamad amekuwa akiendesha mapambano kwa mgongo wa maalim Seif na kuwa, amekuwa akitumia fedha nyingi katika kuhakikisha kwamba lengo lake linafikiwa.

  Pamoja na mambo mengine Bw. Mtatiri alibainishwa kwamba, lengu kuu la mbunge huyo wa Wawi kuanza harakati zake mapema na kinyume cha taratibu za chama ni kusaka nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara huku akiwa na malengo yake binafsi.

  Alisema, CUF ni chama makini na kina utaratibu unaoeleweka na ulio wazi kwa wajumbe na wanachama wote na kuwa, taratibu zilizowekwa ingempasa kuzifuata ili kufikisha hoja ama mapendekezo yake katika chama.

  Alisema, kwa kufanya hivyo angekuwa na nafasi nzuri ya kusikilizwa mapendekezo yake hivyo kuboresha chama tofauti na sasa ambapo anaonekana kuwagawa wanachama.

  "Harakati za kusaka nafasi ya ukatibu mkuu anazotumia mwenzetu (Bw. Hamad) si sahihi, staili hii ni ya umafia, chama chetu kina katiba na inaeleza kila kitu wala si kama anachofanya Hamad cha kugawa watu," alisema Bw. Mtatiro.

  Alisema, Bw. Hamadi anaweza kuwa na malengo mengine tofauti na yale anayoyaeleza hadharani kwa kuwa, kiongozi aliye na mapenzi mema na chama chake hawezi kushawishi wananchi kuhama chama hicho iwapo yule asiyemtaka atashindwa kuondoka katika nafasi hiyo.

  "Tunamshangaa Bw. Hamadi kwa kuwa, pamoja na kuwa na madai yake na kuwaeleza wananchi nia yake, lakini amekuwa akiwashawishi wanachama wa CUF kukihama chama ikiwa atakosa nafasi hiyo," alisema Bw. Mtatiro

  Akizungumzia vurugu zilizotokea juzi, Bw. Mtatiro alisema, CUF inao utaratibu unaoeleweka hasa pale mbunge wa chama hicho anapotaka kuzunguza ama kufanya mkutano na wananchi pia wanachama.

  Alisema, hakuna ruhusa yoyote kwa mbunge ama mtu yoyote kuitisha mkutano wa wanachama wa chama hicho bila idhini ya chama, na kwamba kufanya hivyo ni kukiuka maadili na miiko ya chama.

  Bw. Mtatiro alidai kuwa, tofauti na matarajio ya wanachama wengi, Bw. Hamad aliamua kukodi vijana 100 kwa kuwalipa pesa lengo likiwa ni kuhudhuria mkutano huo na kuonesha kuwa anakubalika ambapo vijana hao ndio waliohusika kuanzisha vurugu kwa kuwapiga mapanga walinzi wa CUF.

  Katika madai hayo Bw. Hamadi alisema, hatumii fedha kununua wanachama wala hana vurugu zozote isipokuwa lengo lake ni kukiimarisha chama.

  "Siwezi kutumia fedha, lengo langu ni kukiimarisha chama na ndio maana niliamua kuitikiwa wito kutoka kwa wanachama wa tawi," alisema.

  Bw. Mtatiro alisema, Ofisi Kuu baada ya kupata taarifa ya kuwepo kwa mkutano ulioitishwa kwa jina la CUF, ofisi iliamua kuwatuma walinzi kwenda katika eneo hilo ili kuweza kupata ukweli na ndipo hapo vurugu ilipoanza.

  "Baada ya kusikia kuwa kuna kikao, tuliwatuma askari wanane kwenda kuuliza, lakini hawakupatiwa majibu na badala yake walipigwa mapanga na kujeruhiwa," alisema Bw. Mtatiro

  Alisema, wahusika wa vurugu hizo wawameitwa katika kamati ya maadili ili kujieleza na kupata ukweli kuhusu tukio hilo ili wachukuliwe hatua.

  Katika vurugu hizo askari wanne walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao na kufungua jarada Kituo cha Polisi Magomeni.   
 2. josefast

  josefast JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  shauri yao kazi ni kwao
   
 3. A

  Awo JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Na kule kwingine Kafulia wameshamvua gamba. Hii ni dhambi ya kuisakama CDM inawatafuna tartibuuuuuuuuuuuuu?
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ndoa ndoana.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Meno ya mbwa hayo, hayaumani
   
 6. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mtatiro nafasi yake matatani,masikini weeeeeeeee,tulimwambia huko siko hakusikia sasa anajuta
   
Loading...