CUF 'Yalipua Bomu' Dar

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
48,851
18,948
Mwandishi Wetu
Daily News; Wednesday,May 14, 2008 @08:00


CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeanika hadharani nyaraka zote zinazoonyesha kuwa mazungumzo baina yake na Chama Cha Mapinduzi (CCM) yamekamilika, na miongoni mwa mambo yaliyoko katika rasimu ya makubaliano ni kuundwa kwa Serikali ya Kitaifa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Saalam jana, chama hicho kimetoa nyaraka zote kwa wanahabari zinazoonyesha tangu vyama hivyo vianze mazungumzo, ikiwamo rasimu ya mazungumzo iliyoandaliwa na kamati ya mazungumzo licha ya CCM kudai haijawahi kuwapo.

Nyaraka hizo zina ushahidi wa kukamilika kwa mazungumzo yaliyohitimishwa na makatibu wakuu na wenyeviti wenza wa kamati ambako walikubaliana njia za utekelezaji za kikatiba na sheria, hatua za siasa na hatua za utawala.

“Kama kuna ajenda iliyobaki ambayo haijajadiliwa ni ya sita iliyozushwa na CCM inayohusu kura ya maoni, na haikuwamo katika orodha ya ajenda za mazungumzo,” lilidai tamko la chama hicho lililosomwa jana na Jussa Ismail Ladwa.

Kuhusu nafasi ya Waziri Kiongozi, chama hicho kimefafanua kuwa ni kweli walikubaliana Serikali shirikishi kuundwa mwaka 2010, lakini wakakubaliana kuwa baada ya kusainiwa makubaliano hayo, kwanza ingeundwa serikali ya kitaifa itakayohusisha CUF.

“Mbona hili CCM hawataki kulisema?” alihoji Jussa ambaye alisoma tamko hilo mbele ya viongozi wakuu wa chama hicho ambao walikuwa wanashiriki kwenye mazungumzo hayo wakiongozwa na Katibu Mkuu, Seif Sharrif Hamad.

Tamko hilo la CUF linatokana na tamko la CCM lililotolewa na mwanasiasa Kingunge Ngombale-Mwiru na Katibu Mkuu wake, Yusuf Makamba, ambao walikishutumu chama hicho cha upinzani kuwa viongozi wake ni waongo na kwamba hakuna rasimu ya makubaliano iliyofikiwa katika mazungumzo.

CCM pia ilisema mazungumzo hayo hayajawahi kukamilika ndiyo maana wanaitaka CUF irudi kwenye meza ya mazungumzo. Kingunge pia alimshutumu Seif kuwa alikiuka makubaliano ya mazungumzo hayo.

Katika mazungumzo ya jana, CUF ilisema suala la Waziri Kiongozi lililofafanuliwa na Seif liko katika rasimu ya makubaliano yaliyofikiwa na vyama hivyo wakati wa kuunda serikali ya kitaifa kuelekea uchaguzi wa 2010.

Chama hicho kinadai katika makubaliano hayo ya kuundwa kwa serikali ya kitaifa, CUF ingeingizwa serikalini baada tu ya kusainiwa makubaliano na chama hicho kingetoa Waziri Kiongozi na mawaziri saba na manaibu waziri watatu.

“Waziri na naibu wake wangetoka vyama tofauti…na sisi tulishapeleka mapendekezo yetu kwa CCM na wala chama hicho hakikuwahi kujibu barua ya kuyakataa, hali inayoonyesha kuwa yalikubaliwa na chama hicho tawala,” linasema tamko hilo la CUF.

Kuhusu Seif kutangaza hadharani makubaliano hayo, CUF imesema kiongozi wake alifanya hivyo kwa vile tayari walishapata taarifa za mbinu za CCM za kupanga kuwapiku katika siasa ndiyo maana wakatangaza hadharani makubaliano hayo Machi 17, mwaka huu.

Chama hicho kinasisitiza kuwa rasimu ya makubaliano ipo na ilipitishwa kwa pamoja na kamati ya makatibu wakuu katika kikao cha 18. CUF inadai rasimu hiyo ilikuwa na kurasa 13 na baadaye ilifanyiwa marekebisho.

Kuhusu kura ya maoni, chama hicho kimetoa sababu nane za kukataa hoja hiyo na moja ya sababu kinadai kuwa kura ya maoni haiwezi kutatua mgogoro wa Zanzibar bila ya kwanza taasisi zote zinazohusika na masuala ya uchaguzi kufanyiwa marekebisho.

Chama hicho pia kinaamini kuwa kura ya maoni ni njia ya hadaa ya kupoteza muda tu hadi 2010 ili kutayarisha mazingira ya uchaguzi mkuu mwingine utakaotawaliwa na vurugu na fujo, kwa sababu tu CCM inaogopa uchaguzu huru na wa haki.

Kuhusu uhusiano wa chama hicho na Hizbu, CUF ilidai CCM ndiyo yenye sifa zote za uhusiano wa karibu na Hizbu. Alisema CCM Zanzibar kuna mawaziri katika serikali ya sasa ambao waliwahi kuwa wanachama wa Hizbu.

Kwa upande wake, Seif alisema hawawezi kurudi kwenye mazungumzo badala yake chama hicho bado kina imani na Rais Jakaya Kikwete ya kuwakutanisha yeye na Rais Amani Karume.

“Katika hali ya namna hii mazungumzo hayawezi tena kuendelea, mwenye uwezo wa kuokoa suala hili ni Rais Kikwete peke yake,” alisema Seif.
 
Upumbavu Wa Katibu Mkuu Ccm Waumaliza Mwafaka..wakati Akisaini Wamekubaliana Hakujua Wanatakiwa Kwenda Kwenye Nec Kuwajkilisha Kwanza..
Big Up Cuf..hatutaki Viongozi Wazembe Wanaoendeza Per Dm Badala Ya Amani..huyu Katibi Wa Ccm Anajua Kuna Mfuko Unatoka Wa Muwafaka Na Ndio Maana Wanangania ....cuf Waambien Wakakutane Na Nyerere!!!!!!watanzania Wamechoka Na Ujinga
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom