CUF yakerwa kuitwa CCM-B; Wabunge sita watua Igunga kuongeza nguvu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779

*Wabunge sita watua Igunga kuongeza nguvu

Na Peter Mwenda, Igunga

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha mara moja kutangaza
kudanganya wananchi wa Jimbo la Igunga kuwa chama hicho kisipewe kura kwa madai kuwa ni CCM-B.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga juzi, Kaimu Katibu Mkuu wa CUF-Bara, Bw. Julius Mtatizo alisema CHADEMA imekuwa ikiwadanganya wananchi kuwa CUF ni CCM-B, wasikichague kwa sababu hakitaleta maendeleo jambo ambalo ni udanganyifu ambao unastahili adhabu.

Alisema CUF imevumilia sana kauli hizo na sasa imefika kikomo, hivyo kilichobaki ni wao kuweka hadharani mabaya ya CHADEMA kwa sababu ya upotoshaji huo kwa wapiga kura wa Igunga.

Bw. Mtatiro alisema cha kushangaza, ni kwa nini CHADEMA iseme uongo wakati CUF haijawahi kusema mtindo wa uongozi wa upendeleo uliopo katika chama hicho, ambao hauna tofauti na yale yanayofanywa na chama tawala CCM.

"Mfumo wa uongozi wa CHADEMA hauna tofauti na ule wa CCM kwa sababu ule mfumo wa uongozi wa kupeana ulipo CCM ambao hautawahi kutokea CUF," alisema Bw. Mtatiro.

Alisema CHADEMA ilipata viti maalumu 36 na kushindwa kugawa kwa kuzingatia uwakilishi wa wananchi, bali walipendeleana wao kwa wao kwa kugawa viti 16 kwa mkoa wa Kilimanjaro pekee ambako viongozi wa chama hicho, walitoa kwa wake zao, wadogo zao na jamaa zao.

Alisema CUF Tanzania bara na Zanzibar walipata viti maalum kumi ambavyo ilivigawa bila upendeleo Dodoma (Bi. Moza Abeid), Mwanza (Bi. Mkiwa Kimwanga , Tanga Bi, Amina Mwidau, Mtwara (Bi. Clara Mwatuka, Kaskazini Pemba (Bi. Riziki Omar Juma), Mjini Magharibi Bi. Amina Amour na Kusini Magharibi (Bi. Thuwaiba Idris) ambao wanakilisha wa wananchi badala ya kulimbikizia kundi chache.

Alisema suala la Serikali ya Umoja Zanzibar ni mfumo uliofikiwa na Wazinzibari wenyewe ili kuondoa uhasama uliokuwepo, sasa inakuaje CHADEMA iseme CUF imeingia mkataba wa urafiki na CCM.

Wabunge waongeza nguvu

Wabunge sita wa CUF kutoka Zanzibar waliokuwa katika msiba wa meli ya M.V Spice Islanders wamewasili Igunga kuanza kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho, Bw. Leopold Mahona.

Wakitambulishwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Nanga juzi jioni, Kaimu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Bw. Julius Mtatiro alisema pamoja kuwa msiba huo ni mkubwa na umegusa familia za wabunge hao, wamekuja kuongeza nguvu kuhakikisha chama hicho kinachukua kiti.

Waliotambulishwa ni Mbunge wa Nungwi ambako meli hiyo ilizama, Bw. Yusuf Haji Khamis, Bw. Rashid Ali Omar (Kojani), Mohamed Habib Mnyaa (Mkanyageni), Haroub Mohamed Shamis (Chonga), Bw. Salim Hemed Khamis (Chambani).

Katika mkutano huo mgombea ubunge wa CUF, Bw. Leopold Mahona alisema akichaguliwa atahakikisha wananchi wa Kata hiyo wataondokewa na kero zinazowasumbua kwa miaka mingi bila kupatiwa ufumbuzi

niweze

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
1,008
114
Wacha waendekuongeza nguvu ya kuia cuf na ccm. Hivi nani anajua kama cuf ni chama au ni tawi la ccm? Tatizo la cuf ni magonjwa ya ccm na kupenda matundo yao zaidi ya Utanzania kwanza...
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
Sikujua kuwa Bw. Mtatiro pia anadanganya kuwa wabunge wa kuteuliwa 16 wametoka Kilimanjaro
Sikujua ana matatizo ... Ana Matatizo huyu kijana

Wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA ambao majina yao yamepitishwa na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Lucy Owenya (Kilimanjaro), Esther Matiko (Mara) Mhonga Luhanywa (Kigoma), Anna Mallac (Katavi), Paulina Gekul (Manyara) na Conchesta Rwalumulaza (Kagera).

Wengine ni Suzan Kiwanga (Morogoro), Grace Kiwelu (Kilimanjaro), Suzan Lyimo (Kilimanjaro), Regia Mtema (Morogoro), Christowaja Mtinda (Singida), Anna Komu (Dar es Salaam), Mwanamrisho Abama (Zanzibar), Joyce Mukya (Arusha), Leticia Mageni Nyerere (Mwanza) na Naomi Kaihula (Dar es Salaam).

Majina mengine ya wateule hao ni Chiku Abwao (Iringa), Rose Kamili (Manyara), Christina Lissu (Singida), Raya Ibrahim Khamis (Zanzibar), Philipa Mturano (Dar es Salaam), Mariam Msabaha (Zanzibar) na Rachel Mashishanga (Dar es Salaam).

Didia

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
719
258
"Wabunge sita wa CUF kutoka Zanzibar waliokuwa katika msiba wa meli ya M.V Spice Islanders wamewasili Igunga kuanza kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho, Bw. Leopold Mahona".

Am afraid they may be political armatures of the Mainland Politics. Given sizes of constituencies in Zbar they may have never addressed a crowd of 5000.
Anyway they are warmly invited to get experience of mainland politics beyond parliamentary setting they are used to.
 
Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,524
13,099
Mod hii post unganisha na ile ya jana inayosema Mtatiro aishambulia chadema kwa sababu habari ni ile ile.
 
Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,882
1,124
unajua wanawake wengi haswa wale walioolewa hawapendi kuitwa kwa majina ya bwana zao.
kuna sababu nyingi lakini kubwa ni vyeti vya masomo na kupotezahaki zao kwenye pensheni.

cuf wana haki ya kukataa kuitwa ccmb.
 
SEAL Team 6

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
655
118
Labda kama wamekuja kuwaeleza wakazi wa Igunga umuhimu wa HIJABU. Suala la CUF kuwa CCM B hilo halipingiki, hata wabunge wao bungeni wanahubiri kuwa ni ccm B.
 
RUMANYIKA

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
315
74
Sikujua kuwa Bw. Mtatiro pia anadanganya kuwa wabunge wa kuteuliwa 16 wametoka Kilimanjaro
Sikujua ana matatizo ... Ana Matatizo huyu kijana

Wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA ambao majina yao yamepitishwa na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Lucy Owenya (Kilimanjaro), Esther Matiko (Mara) Mhonga Luhanywa (Kigoma), Anna Mallac (Katavi), Paulina Gekul (Manyara) na Conchesta Rwalumulaza (Kagera).

Wengine ni Suzan Kiwanga (Morogoro), Grace Kiwelu (Kilimanjaro), Suzan Lyimo (Kilimanjaro), Regia Mtema (Morogoro), Christowaja Mtinda (Singida), Anna Komu (Dar es Salaam), Mwanamrisho Abama (Zanzibar), Joyce Mukya (Arusha), Leticia Mageni Nyerere (Mwanza) na Naomi Kaihula (Dar es Salaam).

Majina mengine ya wateule hao ni Chiku Abwao (Iringa), Rose Kamili (Manyara), Christina Lissu (Singida), Raya Ibrahim Khamis (Zanzibar), Philipa Mturano (Dar es Salaam), Mariam Msabaha (Zanzibar) na Rachel Mashishanga (Dar es Salaam).

Mbona Shinyanga hamna hata mmoja wakati kuna wabunge wanne wa CDM? Mgawanyo ulikuaje kwa mkoa wa Shinyanga.
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,395

Zitto alinijibu siku ile kwamba walikuwa na vigezo vyao. Pengine akina mama wa Shinyanga hawakukidhi vigezo hivyo. Tumuulize Dr Kitila Mkumbo juu ya baadhi ya mikoa kuwa na viti maalum viwili wakati mikoa mingine hakuna. Aeleze pia ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa viongozi wakuu wa CHADEMA waliupataje Ubunge wa VITI MAALUM.
 
Kwetu Iringa

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
355
88
Sikujua kuwa Bw. Mtatiro pia anadanganya kuwa wabunge wa kuteuliwa 16 wametoka Kilimanjaro
Sikujua ana matatizo ... Ana Matatizo huyu kijana

Wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA ambao majina yao yamepitishwa na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Lucy Owenya (Kilimanjaro), Esther Matiko (Mara) Mhonga Luhanywa (Kigoma), Anna Mallac (Katavi), Paulina Gekul (Manyara) na Conchesta Rwalumulaza (Kagera).

Wengine ni Suzan Kiwanga (Morogoro),
Grace Kiwelu (Kilimanjaro), Suzan Lyimo (Kilimanjaro), Regia Mtema (Morogoro), Christowaja Mtinda (Singida), Anna Komu (Dar es Salaam), Mwanamrisho Abama (Zanzibar), Joyce Mukya (Arusha), Leticia Mageni Nyerere (Mwanza) na Naomi Kaihula (Dar es Salaam).

Majina mengine ya wateule hao ni Chiku Abwao (Iringa),
Rose Kamili (Manyara), Christina Lissu (Singida), Raya Ibrahim Khamis (Zanzibar), Philipa Mturano (Dar es Salaam), Mariam Msabaha (Zanzibar) na Rachel Mashishanga (Dar es Salaam).

Mbona hamna wa kutoka Mbeya na Ruvuma?? Dodma??
 
Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,476
1,773
Zitto alinijibu siku ile kwamba walikuwa na vigezo vyao. Pengine akina mama wa Shinyanga hawakukidhi vigezo hivyo. Tumuulize Dr Kitila Mkumbo juu ya baadhi ya mikoa kuwa na viti maalum viwili wakati mikoa mingine hakuna. Aeleze pia ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa viongozi wakuu wa CHADEMA waliupataje Ubunge wa VITI MAALUM.

Huu mgawanyo wa viti maalum binafsi sikuupenda hata kidogo.
Wakati mwingine CDM inafanya mambo ambayo yanawapa nafasi watu kuisema vibaya. nashawishika kuamini kwamba Kitila Mkumbo alishinikizwa kuwapendelea baadhi ya wabunge.
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,395
VITI MAALUM ni MZIGO kwa kodi zetu. Kuna mikoa sasa hivi ina Wabunge wa viti maalum zaidi ya wanne. CHADEMA ina wao, CCM ina wao na CUF ina wa kwao. Nini wanafanya, kwa manufaa ya nani, hakuna anayejua.
 
Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,282
17,036
Alisema CUF Tanzania bara na Zanzibar walipata viti maalum kumi ambavyo ilivigawa bila upendeleo Dodoma (Bi. Moza Abeid), Mwanza (Bi. Mkiwa Kimwanga) , Tanga Bi, Amina Mwidau, Mtwara (Bi. Clara Mwatuka), Kaskazini Pemba (Bi. Riziki Omar Juma), Mjini Magharibi Bi. Amina Amour na Kusini Magharibi (Bi. Thuwaiba Idris) ambao wanakilisha wa wananchi badala ya kulimbikizia kundi chache.

Huyu Mtatiro mtu wa ajabu kweli.....sijui alikuwako msikitini walipogawa hivyo viti maalumu vya CUF
 
MPG

JF-Expert Member
May 12, 2011
483
53
Cuf si chama we cha kushangaza mwenyekiti wao hana hata nyumba Tabora huko kwao,akifa atazikwa makaburi ya kinondoni B hapo dare salaam mana hata ndugu zake wakifa huwa anawazika Dar badala ya Tabora kwao,Igunga hawana chao kule wanapunguza 2 kula za CCM za wale wanywa kahawa na wacheza bao.
 
Shenkalwa

JF-Expert Member
May 3, 2011
580
132

*Wabunge sita watua Igunga kuongeza nguvu

Na Peter Mwenda, Igunga

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha mara moja kutangaza
kudanganya wananchi wa Jimbo la Igunga kuwa chama hicho kisipewe kura kwa madai kuwa ni CCM-B.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga juzi, Kaimu Katibu Mkuu wa CUF-Bara, Bw. Julius Mtatizo alisema CHADEMA imekuwa ikiwadanganya wananchi kuwa CUF ni CCM-B, wasikichague kwa sababu hakitaleta maendeleo jambo ambalo ni udanganyifu ambao unastahili adhabu.

Alisema CUF imevumilia sana kauli hizo na sasa imefika kikomo, hivyo kilichobaki ni wao kuweka hadharani mabaya ya CHADEMA kwa sababu ya upotoshaji huo kwa wapiga kura wa Igunga.

Bw. Mtatiro alisema cha kushangaza, ni kwa nini CHADEMA iseme uongo wakati CUF haijawahi kusema mtindo wa uongozi wa upendeleo uliopo katika chama hicho, ambao hauna tofauti na yale yanayofanywa na chama tawala CCM.

"Mfumo wa uongozi wa CHADEMA hauna tofauti na ule wa CCM kwa sababu ule mfumo wa uongozi wa kupeana ulipo CCM ambao hautawahi kutokea CUF," alisema Bw. Mtatiro.

Alisema CHADEMA ilipata viti maalumu 36 na kushindwa kugawa kwa kuzingatia uwakilishi wa wananchi, bali walipendeleana wao kwa wao kwa kugawa viti 16 kwa mkoa wa Kilimanjaro pekee ambako viongozi wa chama hicho, walitoa kwa wake zao, wadogo zao na jamaa zao.

Alisema CUF Tanzania bara na Zanzibar walipata viti maalum kumi ambavyo ilivigawa bila upendeleo Dodoma (Bi. Moza Abeid), Mwanza (Bi. Mkiwa Kimwanga , Tanga Bi, Amina Mwidau, Mtwara (Bi. Clara Mwatuka, Kaskazini Pemba (Bi. Riziki Omar Juma), Mjini Magharibi Bi. Amina Amour na Kusini Magharibi (Bi. Thuwaiba Idris) ambao wanakilisha wa wananchi badala ya kulimbikizia kundi chache.

Alisema suala la Serikali ya Umoja Zanzibar ni mfumo uliofikiwa na Wazinzibari wenyewe ili kuondoa uhasama uliokuwepo, sasa inakuaje CHADEMA iseme CUF imeingia mkataba wa urafiki na CCM.

Wabunge waongeza nguvu

Wabunge sita wa CUF kutoka Zanzibar waliokuwa katika msiba wa meli ya M.V Spice Islanders wamewasili Igunga kuanza kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho, Bw. Leopold Mahona.

Wakitambulishwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Nanga juzi jioni, Kaimu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Bw. Julius Mtatiro alisema pamoja kuwa msiba huo ni mkubwa na umegusa familia za wabunge hao, wamekuja kuongeza nguvu kuhakikisha chama hicho kinachukua kiti.

Waliotambulishwa ni Mbunge wa Nungwi ambako meli hiyo ilizama, Bw. Yusuf Haji Khamis, Bw. Rashid Ali Omar (Kojani), Mohamed Habib Mnyaa (Mkanyageni), Haroub Mohamed Shamis (Chonga), Bw. Salim Hemed Khamis (Chambani).

Katika mkutano huo mgombea ubunge wa CUF, Bw. Leopold Mahona alisema akichaguliwa atahakikisha wananchi wa Kata hiyo wataondokewa na kero zinazowasumbua kwa miaka mingi bila kupatiwa ufumbuziWatu wengine wanashangaza sana. Naona hawa nao wameambukizwa kufikiri kwa masaburi. Kitu kiko wazi wazi ndoa ilifanyika zanzibar kati yao na magamba, leo mchana kweupe unakataa. Hivi wewe sasa hivi unaweza kufanya kitu chochote kitakachomuudhi mwenza wako?? Kwa nini unakana kitu ambacho kiko wazi na kimefanyika mchana machoni pa kila mtu?? Ama kweli ukitembea na mwizi na wewe utakuwa mwizi na hivyo hivyo ukitembea na mtu anayefikiri kwa masaburi na wewe utafikiri kwa masaburi hivyo hivyo. Masaburi yenu
 
Kabakabana

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
5,553
1,157
kama hawataki kuitwa hivyo waache kufanya mambo yanayopelekea kuitwa hivyo kwa kulalamika tu wanaonyesha kuwa wao kweli ni ccm B
 
Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,597
1,812
Hawafanyi kazi kwa kufuata matakwa ya MAGAMBA, mwenye uwezo na nia ndio anapewa nafasi

Zitto alinijibu siku ile kwamba walikuwa na vigezo vyao. Pengine akina mama wa Shinyanga hawakukidhi vigezo hivyo. Tumuulize Dr Kitila Mkumbo juu ya baadhi ya mikoa kuwa na viti maalum viwili wakati mikoa mingine hakuna. Aeleze pia ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa viongozi wakuu wa CHADEMA waliupataje Ubunge wa VITI MAALUM.
 
Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,597
1,812
Alisema CUF Tanzania bara na Zanzibar walipata viti maalum kumi ambavyo ilivigawa bila upendeleo Dodoma (Bi. Moza Abeid), Mwanza (Bi. Mkiwa Kimwanga , Tanga Bi, Amina Mwidau, Mtwara (Bi. Clara Mwatuka, Kaskazini Pemba (Bi. Riziki Omar Juma), Mjini Magharibi Bi. Amina Amour na Kusini Magharibi (Bi. Thuwaiba Idris) ambao wanakilisha wa wananchi badala ya kulimbikizia kundi chache.

Huyu Mtatiro anaongea vitu bila kujifikiria, mbona hata wao hivyo viti kumi walivyopata mbona vimegawanywa kwa kizingatia itikadi za kidini??
 
Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
4,502
Wabunge wa nchi jirani hawatasaidia chochote Igunga mazingira ni tofauti sana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom