CUF yafunika Igunga, Shughuli zasimama, Maduka yafungwa, CDM yapata aibu.

huyu lipumba ni mwenyekiti wa kichina ajiuzuru tu mwenyekiti wa CDM amechukua jimbo katika sehemu anayotoka mrema nao kachukua kikwete nae jimbo analotoka linaongozwa na chama chake yeye tu hana nguvu kabisa bora astaafu
 
C.jpg




HAKIKA POLITICS IS COMMEDY
 
Teh teh teh Ahahahaha!! Magwanda baada ya kuona hali imeishakuwa ngumu Igunga yameamua kuanzisha thread ya kujiliwaza na kujifariji, Teh teh teh

nashindwa kutofautisha uchangiaji wako na avatar yako!!naomba unisaidie katika hili....
 
C.jpg




CUF imezindua Kampeni zako huko igunga kwa mtindo wa aina yake wakati Punda Kihongo wakikokota mkokoteni uliomchukua Mwenyekiti wa Taifa Ibrahim Lipumba pamoja na mgombea wake wa Ubunge jimboni Igunga.

Siasa ni usanii yakhe!

NIKWELI TANZANIA IMEFIKIA HAPA!!!!

K
itendo hiki hakijafanywa na Viongozi wa CUF, wala hakijafanywa kwa mujibu wa kampeni, kwa hili hatuna cha kujificha, kitendo hiki kimefanywa na watanzania wote kwa ujumla wetu, hapa hatuna pa kujificha. Kitendo cha UNYANYASAJI, AIBU, UKATILI MKUBWA KIASI HIKI, Kinakiuka Sheria za haki za wanyama na pia ni dhambi kwa Mungu. Hakuna ubunifu wa Ukatili. mashirika yote ya haki za wanyama kama Animal protection League of NJ (f.k.a. NJ Animal Rights Alliance), The Bear Education and Resource Group, The Humane Society of the US, na the Animal Welfare Institute.. Vinapingana na dhana hii potofu ya kuendelea kuwanyanyasa wanyama hasa wanyama wafugwao nyumbani (Domestic animal Rights) Ni kweli kwamba kwa nyaka ti tofauti za nyuma wanyama kama Punda, Mbwa, Paka, Mbuzi, Ng'ombe, Kondoo na wengineo walitumika kama viumbe visivyo na uhuru wa kujitetea ndani ya jamii. lakini baadae Zimeundwa sheria nyingi kuwalinda wanyama hawa. Ziko mifano mingi ila kwa mnyama kama huyu Punda, kumekuwa na maswali mengi kwamba Je Punda, farasi na Ngamia, je inafaa waendelee na Kuwatumikia wanadamu kwa kuwabeba au kubeba mizigo yao? Iliazimiwa kwamba Wanyama hawa wasitumike kwenye utumwa huo, kwa sababu maendeleo ya sayansi na technologia yamesha-replace dhana hiyo ya uchukuzi kwa kuwa na vyombo mbalimbali vya nchi kavu, majini na angani kwa uchukuzi.
Ikumbukwe kwamba kuna wanafunzi nane walihukumiwa na mashirika hayo kwa kila mmoja kupanda punda akielekea shuleni. kama mwanafunzi kupanda punda ilikuwa hoja, sasa je hawa viongozi wazito, wakubwa wa vyama, watu wawazao, wanafanyanini kuueleza umma wa watanzania na Dunia kwa ujumla. Ni ukatili gani huu. na Muda si mrefu mtaona reaction ya mashirika haya..
HONGERA CUF KUZINDUA KAMPENDI ZENU (Ingawa tuko msibani mngepaswa kuomboleza kwanza) But kwa hili la Punda .... AIBU HII TUTAIWEKA WAPI
..........

Tusiwa wavivu wa kusoma, 1. Shrika la haki za wanyama (JN
 


Kutokana na kuanza kupoteza mvuto katika jimbo la Igunga hasa kutokana na mwitikio duni wa wananchi katika mkutano wa uzinduzi wa chama cha CUF, na pia kwa makada wake kuonekana kuikampenia CCM, kuna uwezekano mkubwa sana kwa chama hicho kufanya alichofanya Fahmi Dovutwa wa UPDP mwaka jana, kutangaza kujitoa na kuwaambia wafuasi wake jimboni humo wamopigie kura mgombea wa CCM.


Kinachosubiriwa ni kwa profesa kutangaza hivyo muda si mrefu kuanzia sasa!

Siasa haziendi hivyo. Kama hii ikitokea maana yake ni sawa kupigilia msumari wa mwisho kwenye Jeneza la kuizika CUF Bara. Huo utakuwa mwisho rasmi wa CUF. Na ikitokea hivyo basi tutarajie the next day Lipumba anatangaza kurudi CCM.
 
Binafsi naamini huu ndio utakuwa mwanzo wa kifo cha CUF.....! Kwa maana kutatokea mpasuko mkubwa sana huko, na kudhihirishia umma kuwa kumbe wao ni CCM - B.....!
 
Teh teh teh Ahahahaha!! Magwanda baada ya kuona hali imeishakuwa ngumu Igunga yameamua kuanzisha thread ya kujiliwaza na kujifariji, Teh teh teh
Hivi wewe ritz huwa unafanya kazi saa ngapi maana huwa nakuona masaa 24 humu tena unachangia puimba au ndo mmoja wa watu walio kwenye bajeti ya uchaguzi wa magamba kule igunga?
 
C.jpg




CUF imezindua Kampeni zako huko igunga kwa mtindo wa aina yake wakati Punda Kihongo wakikokota mkokoteni uliomchukua Mwenyekiti wa Taifa Ibrahim Lipumba pamoja na mgombea wake wa Ubunge jimboni Igunga.

Siasa ni usanii yakhe!
Wanasema, kwa Mchezaji wa Mpira, Mpira unapoisha mguuni hukimbilia Mdomoni. Hata kwenye siasa mtu anapoishiwa hukimbilia kwenye Usanii.
Kama Mtakumbuka wakati anaelekea kufulia kisiasa, Mzee wetu Mrema nae alishawahi kuzindua kampeni kwa kupanda GUTA. Kwa hiyo watu kama sie tunaoona mbali tumeshaachana na Lipumba kwamba keshajifia kisiasa huyo kabaki kuwa Mchekeshaji sasa.
 
MaChama cha Wananchi CUF jana kimeifunika Igunga, mapokezi makubwa ya kwanza ya kihistoria yamefanyika baada ya Mwenyekiti wa CUF profesa Ibrahim Haruna Lipumba kuwasili. DSC00817.JPG Mapokezi hayo yalianzia nje kidogo mji wa Igunga ambapo Profesa Lipumba alipokelewa kwenye kijiji cha Makomelo. Lipumba alipokelewa kwa magari yaliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu chama hicho upande wa Tanzania bara Julius Mtatiro. Baada ya mapokezi hayo ya mwanzo msafara wa magari 12 ulielekea ndani ya mji wa Igunga ambapo mamia ya wakazi walijitokeza kwa wingi kutoka katika Tarafa ya Igunga na kata za jirani.

Lipumba alipoufikia umati huo alipandishwa kwenye gari maalum lililokokotwa na Punda akiwa na mgombea wa CUF Mahona Leopold Lucas (29) na msafara wao ukaelekea viwanja vya sokoine na kuzindu kampeni kwa kishindo kikubwa.

Kilichowashangaza wakazi wa Igunga ni umati mkubwa wa mamia ya wananchi wasiohesabika uliojitokeza kumpokea Lipumba. Watu wengi walijikuta katika butwaa na wengine wakisema hakuna kiongozi aliyewahi kupata mapokezi hayo. Wananchi wengi wa Igunga walikwenda viwanja vya Sokoine ili kusikiliza sera za chama hicho na mgombea wake na wengi pia walisubiri kwa hamu kusikiliza majibu ya tuhuma ambazo CHADEMA wamezieneza jimboni hapa kuwa CUF ni CCM B na kuwa CUF imejileta Igunga kumsaidia mume wake CCM na kugawa kura za CHADEMA, tuhuma ambazo pia zilitolewa kwenye mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa kampeni za CHADEMA ulioongozwa na Mhe Mbowe na Dr Slaa(PHD).

Jambo la kushangaza ni kuwa CUF walipoteza muda wote kuishambulia CCM , kumshambulia mkapa pamoja na serikali ya Kikwete na kuwaeleza wananchi kuwa CCM imechoka na imeshindwa na kuwa iondolewe haraka kupitia masanduku ya kura na kumuweka madarakani Mahona Leopold Lucas wa CUF. Kuanzia mwanzo wa mkutano wa CUF uliofurika kisawasawa hadi mwisho neno CHADEMA halikutajwa kabisa(Sielewi kama ilikuwa ni kwa makusudi au la?).

Jioni ya jana na leo siku nzima ukifika Igunga gumzo kubwa ni CUF katika kila kijiwe na hasa wananchi wanasifia namna kijana wa CUF alivyo na uwezo mkubwa wa kujieleza na kuwashawishi wananchi wampigie kura. Jana bwana Mahona aliongea kwa dakika 35 huku mgombea wa CCM katika uzinduzi wao akiongea kwa dakika 7 na mgombea wa CHADEMA dkk 9. Kwa hakika wananchi wa Igunga wameanza kushawishiwa na kijana huyu wa CUF na kwa hakika kama hali ikisonga hivyo kutakuwa na ushindani mkubwa sana.(Wananchi wanalalamika kuwa mgombea wa CHADEMA na yule wa CCM hawawezi kujieleza vizuri na ka kirefu kama anavyofanya mgombea wa CUF).

Mgombea wa CUF ana kauli mbiu yake iitwayo "NIKIJA",
NI - NISHATI, MADINI NA MALIASILI,
KI - KILIMO NA UFUNGAJI na
JA- JAMII NA HUDUMA ZAKE.

Kwa mara ya kwanza jukwaani hapo Mtatiro alitaja kauli hiyo na akaeleza kuwa mgombea wa CUF ataifafanua baadaye na ndipo ilipofika zamu ya mgombea MAHONA akaifafanua namna hiyo.

Katika hatua nyingine wazee maarufu wa Igunga walimkabidhi ndugu Mahona vazi maalum la jadi, Mkuki, Upinde na mshale na walimkalisha katika kigoda maalum huku kina mama wakimvisha shanga na kumpaka unga kama ishara ya baraka zao kwa kijana huyo mwenye mvuto wa aina yake.

Hata hivyo pamoja na mafanikio hayo ya CUF bado hali ni tete ndani ya jimbo kwani vyama vya CHADEMA na CCM vimezidi kuwekeza nguvu kubwa hasa kukabiliana na mgombea wa CUF ambaye alipambana na Rostam Azizi mwaka 2010 na aliungwa mkono na makumi elfu ya wapiga kura. Kwa hiyo CUF haitapata mteremko kata kama mgombea wake anakubalika na wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri.

Mgombea wa CHADEMA ameendelea kuchanja mbuga katika tarafa mbalimbali akinadiwa na Dr Slaa na wanafanikiwa kufanya mikutano mikubwa kama ilivyo kwa CUF.

CCM wao wameanza leo baada ya kumaliza siku tatu za maombolezo ya msiba uliotokana na ajali ya kuzama meli Zanzibar lakini mikutano yao haina mvuto kabisa, kesho nitawawekea hapa picha yenye kuonesha mikutano ya CCM na mtasikitika, wananchi hawaoni kipi kipya watakisikiliza kutoka CCM.

Kwa vyovyote vile ushindani mkubwa unabakia kuwa kati ya CUF na CHADEMA na CCM zaidi wanaweza kutegemea nguvu ya dola ili kulisaka jimbo hili kwa kuwatumia vijana wao wa JANJAWEED walioko katika kambi maalum Nzega na Uyui.

Mwandishi maalum,
Igunga 0712 293 695.
 
Huo sio unyanyasaji wa wanyama kweli?

Ni kitu kipya kwa watanzania, lakini nchi zilizoendelea utakuwa hawa wanyama wangali na nafasi yao katika jamii kihistoria na shughuli zao. Mbona farasi wanaelekezwa sheria za traffic huku wanakokota mikokoteni na wakati huo huo wamefungwa minyororo na lijamu vinywani mwao, maana yake wananyanyaswa kwa mtazamo wako. Kama uzito umepimwa kwa kiwango kinachokubalika na uwezo wake si unyanyasaji.
 
Back
Top Bottom