CUF yafungua kesi dhidi ya Watu waliochoma bendera na kubadili rangi ofisi za chama

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Chama cha Wananchi (CUF) kimefungua kesi dhidi ya watu walioshiriki kuchoma bendera na kubadilisha rangi za ofisi zake visiwani na kuweka za Chama cha ACT- Wazalendo.

Kesi hiyo ya kiraia namba 16 ya mwaka 2019, imefunguliwa jana Jumatatu Machi 25, 2019 katika Mahakama ya Vuga iliyopo Mjini Unguja, Zanzibar.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumanne Machi 26, 2019 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa chama hicho, Khalifa Suleiman Khalifa amesema wamekusanya ushahidi wote wa vitendo vilivyofanywa na wanachama wa ACT-Wazalendo ambao wamemfuata aliyekuwa katibu mkuu wa Cuf, Maalim Seif Sharif Hamad.

"Maalim Seif na viongozi wenzake wa CUF walitoa agizo kwamba bendera za CUF zishushwe. Kitendo cha kushusha bendera na kuzichoma ni uvamizi wa ofisi, ni jinai. Sisi hatukutaka kupambana nao kwa kuwa hatuna nguvu, lakini tunajua sheria ndiyo maana tumelifikisha suala hili mahakamani," amesema Khalifa.

Katibu mkuu huyo amewataka Wazanzibari kufuata sheria na kuachana na vitendo vya kukihujumu chama hicho kwa kubadilisha ofisi zake kuwa za ACT-Wazalendo, vitendo ambavyo amesema ni jinai.

"Kwa kuwa mimi ndiyo katibu mkuu mpya, nitahakikisha kwa uwezo wa Mungu ninasimamia mali za CUF zinabaki kuwa mali za CUF,” amesema.

" Kuna usemi wao wanasema shusha tanga, pandisha tanga. Lakini wakumbuke wanaweza kuishia matanga.”

Kuhusu wabunge wa CUF ambao walikuwa upande wa Maalim Seif, Khalifa amewataka wafike ofisi za chama hicho kuonana na mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye aliahidi kushirikiana nao katika kukijenga chama hicho na kusahau tofauti zao.

"Wabunge wale wajue kwamba waliingia bungeni kwa tiketi ya CUF wasidhani waliingia kwa tiketi ya Maalim Seif. Yote yamepita, tunachotaka wafike ofisini kumuona mwenyekiti wetu. Hatutakuwa tayari kuona wanatumia rasilimali za chama kuimarisha ACT Wazalendo," amesema Khalifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimekuwa chama cha kushinda mahakamani badala ya kutatua matatizo na kutafuta suluhu na wananchi
 
Anaweza akawataja hao anaowashtaki kwa majina yao tuwatambue, mmekosa kazi za kufanya mmekalia kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu.
 
kwa maana hiyo kusudio la Msajili kuifuta ACT limesimamishwa hadi kesi hii ya msingi imalizike na hukumu na rufani zake zithibitishe kwamba ni kweli waliochoma bendera zile za CUF ni ACT.
 
Chama cha Wananchi (CUF) kimefungua kesi dhidi ya watu walioshiriki kuchoma bendera na kubadilisha rangi za ofisi zake visiwani na kuweka za Chama cha ACT- Wazalendo.

Kesi hiyo ya kiraia namba 16 ya mwaka 2019, imefunguliwa jana Jumatatu Machi 25, 2019 katika Mahakama ya Vuga iliyopo Mjini Unguja, Zanzibar.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumanne Machi 26, 2019 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa chama hicho, Khalifa Suleiman Khalifa amesema wamekusanya ushahidi wote wa vitendo vilivyofanywa na wanachama wa ACT-Wazalendo ambao wamemfuata aliyekuwa katibu mkuu wa Cuf, Maalim Seif Sharif Hamad.

"Maalim Seif na viongozi wenzake wa CUF walitoa agizo kwamba bendera za CUF zishushwe. Kitendo cha kushusha bendera na kuzichoma ni uvamizi wa ofisi, ni jinai. Sisi hatukutaka kupambana nao kwa kuwa hatuna nguvu, lakini tunajua sheria ndiyo maana tumelifikisha suala hili mahakamani," amesema Khalifa.

Katibu mkuu huyo amewataka Wazanzibari kufuata sheria na kuachana na vitendo vya kukihujumu chama hicho kwa kubadilisha ofisi zake kuwa za ACT-Wazalendo, vitendo ambavyo amesema ni jinai.

"Kwa kuwa mimi ndiyo katibu mkuu mpya, nitahakikisha kwa uwezo wa Mungu ninasimamia mali za CUF zinabaki kuwa mali za CUF,” amesema.

" Kuna usemi wao wanasema shusha tanga, pandisha tanga. Lakini wakumbuke wanaweza kuishia matanga.”

Kuhusu wabunge wa CUF ambao walikuwa upande wa Maalim Seif, Khalifa amewataka wafike ofisi za chama hicho kuonana na mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye aliahidi kushirikiana nao katika kukijenga chama hicho na kusahau tofauti zao.

"Wabunge wale wajue kwamba waliingia bungeni kwa tiketi ya CUF wasidhani waliingia kwa tiketi ya Maalim Seif. Yote yamepita, tunachotaka wafike ofisini kumuona mwenyekiti wetu. Hatutakuwa tayari kuona wanatumia rasilimali za chama kuimarisha ACT Wazalendo," amesema Khalifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sheria ifuate mkondo wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom