CUF ya sasa imegawika katika makundi mawili makubwa

Jamhuri ya Zanzibar

Senior Member
Jul 17, 2012
122
250
• Timu Lipumba na timu Muhunzi zaibuka
• Fukuzafukuza zachukua nafasi

Ikumbukwe CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola na taasisi mbali mbali za Serikali ya Muungano ilihakikisha Chama cha CUF kinasambaratika na Maalim Seif ana'ondolewa kwa nguvu zote katika chama hicho. Mpango huo ulifanikiwa kwa mashirikiano makubwa kutoka katika vyombo na taasisi za Dola hasa Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa, Ofisi ya Bunge, Ofisi ya usajili, ufilisi na udhamini (RITA), Mahakama na Jeshi la polisi. Lengo kuu la awali la kukamilisha mpango huo lilikuwa ni kuyafutilia mbali madai ya CUF na Maalim Seif juu ya kile walichokuwa wakikiita haki ya ushindi wao wa uchaguzi mkuu wa wa Zanzibar wa Oktoba 25, 2015 madai ambayo uhalali wake umekuwa ukivinjari na kuungwa mkono kote ndani na nje ya Tanzania.

Baada ya lengo kuu la kukisambaratisha chama cha CUF kutimia, chama hicho sasa kimekuwa nyenzo rasmi na muhimu ya CCM na serikali zake hasa kwa upande wa Zanzibar. Ikumbukwe kuwa kwa upande wa Zanzibar pekee, SMZ chini ya ridhaa ya Dr. Shein ilichangia kiasi cha shilingi milioni mia moja (100,000,000/-) kufanikisha Mkutano Mkuu wa chama hicho uliokuwa na agenda ya kumfukuza katika chama aliekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

Wakati CCM na SMZ wakikifanya chama hicho kama mtaji muhimu wa kuushughulikia upinzani kutokea ndani ya upinzani wenyewe, baadhi ya viongozi wa CCM Zanzibar ambao wapo katika nia ya kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar hawako nyuma kukitumia chama hicho ili kufikia malengo yao binafsi ya kusaka urais. Mmoja wa viongozi hao ni Issa Gavu ambae tayari anaungwa mkono na baadhi ya wakuu wa mikoa na baadhi ya mawaziri katika azma yake ya kugombesa urais wa Zanzibar kwa tketi ya CCM. Kundi hili linasemekana ndilo lililomchimba Mama Samia Suluhu hadi alipolazimika kutoka hadharani na kutoa kauli kwamba hana nia ya kugombea urais wa Zanzibar. Kundi hili pia ndilo linalofanya kila juhudi za kumchafua Dr. Hussein Mwinyi, kiongozi mpole na mtaratibu ambae kwa kiasi kubwa amekuwa akilinda heshima yake kwa chama na serikali zote mbili.

CUF ya sasa imegawika katika makundi mawili makubwa. Kundi la Profesa Lipumba (CUF-Lipumba) na kundi la Bwana Abbas Juma Muhunzi (CUF-Muhunzi) ambae ni Makamo Mwenyekiti. Kundi la Profesa Lipumba ndio lenye kubeba agenda za asili za kimkakati za chama hicho tokea Dola ilipoanza juhudi za kukisambaratisha. Ajenda hizo ni CUF kutumika kama mkono mpya wa CCM na serikali zake katika kufikia malengo mbali mbali ya kisiasa ndani ya nyumba ya upinzani. Katika kundi hili wamo viongozi wakubwa kama vile Khalifa Suleman (Katibu Mkuu), Ali Makame, Rukia Kassim, Ali Jabir, Mohd Haji Mbwana, Nadhifa, Dhifaa, Nassor Seif, Mussa Haji Kombo na Habibu Mnyaa. Kundi la pili ni lile ambalo limebaki katika CUF kwa sababu za kimaslahi hasa kujipatia fedha kutokana na ugumu wa maisha ili kumudu kuhudumia familia zao. Kundi hili linaongozwa na Bwana Abbas Juma Muhunzi wakiwemo ndani yake pia Faki Suleman (Naibu Katibu Mkuu wa Zanzibar), Thiney Juma, Said Omar (vibega) na wengineo.

Kundi la Abbas Muhunzi ambalo zaidi lipo kwa maslahi ya kiedha kama ilivyoelezwa huko nyuma haliaminiki vyema na CCM na serikali ya Zanzibar. Viongozi ndani ya kundi hili wanaonekana baadhi ya wakati kutoa misimamo na kauli zinazokwaza malengo mapya ya CUF na kwenda kinyume na matarajio ya CCM na SMZ. Hivyo basi wakati chama kinajipanga kuelekea katika chaguzi za serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani, CCM na SMZ wameona ipo haja ya chama hicho kusafishwa na wale wote wasioaminika kuondolewa katika safu za uongozi wakati bado ingali mapema. Anaekusudiwa kuondoshwa katika safu ya uongozi kwa awamu ya kwanza ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Faki Suleman ambae yeye anaonekana kuwa mtata zaidi na mwenye misimamo mikali.

Hivi sasa chama cha CUF chini ya uwenyekiti wa Lipumba kinaandaa kikao chake cha Baraza Kuu la uongozi la Taifa kinachotarajiwa kufanyika tarehe 18/09/2019 hapo Ofisi Kuu za Chama Buguruni kikiwa na agenda moja tu muhimu ya kuondoshwa katika uongozi Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Faki Suleman kama ambavyo imeelekezwa na CCM na SMZ. Kikao hiki ni matokeo ya kikao cha wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa upande wa Zanzibar kilichofanyika katika hoteli ya Golden Tulip Zanzibar ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wake Profesa Lipumba. Wajumbe wote wa kikao hicho ni wafuasi wa kundi la CUF lipumba ambao wanaonekana waliandaliwa vyema kumpa kashfa na tuhuma mbali mbali Naibu Katibu Mkuu, Faki Suleman ili kuelekea mkakati wa kumfuka katika uongozi. Mjumbe mmoja tu ajulikanae kwa jina la Khamis Faki ndie aliemtetea Faki Suleman katika kikao hicho. Alieongoza mashambulizi dhidi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar kikaoni ni Faki Ali Jabir, Mwenyekiti wa wilaya ya Wete na Mjumbe wa Baraza Kuu.

Kikao hiki cha Baraza Kuu ni matokeo ya kikao kilichofanyika siku mbili kabla kilichopanga mkakati na agenda ya kung’olewa kwa Faki Suleman katika wadhifa wake. Kikao hicho kilifanyika katika hoteli moja inayomilikiwa na Mbunge wa Tunguu kwa tiketi ya CCM aitwae Khalifa Salum. Hoteli hii ndio jiko kuu la kupikia mipango yote ya CCM na SMZ inayohitaji kutekelezwa kupitia Lipumba na chama chake cha CUF. Wajumbe wa kikao hicho walikuwa ni Issa Gavu, Dr. Juma Mohd wa Idara ya Habari Maelezo, Ali Makame na Said Omar, maarufu kwa jina la Vibega. Kikao hiki ndio kilichotoa maelekezo na muongozo mzima juu ya haja na namna ya kuondolewa Faki Suleman katika wadhifa wake wa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar ili kuepusha vikwazo ambavyo angeweza kuvisababisha huko mbele.

Vita hivi na mgawanyiko huu hasa umezuka baada ya viongozi wawili kutoka kambi hizi mbili tofauti ndani ya CUF, Khalifa Suleiman, Katibu Mkuu kutoka kambi ya CUF-Lipumba na Abbas Muhunzi, Makamo Mwenyekiti, kutoka kambi yake ya CUF-Muhunzi, wote wawili kuweka nia ya kutaka kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Ifahamike kwamba tayari CUF wameshaahidiwa na CCM Zanzibar kwamba watapatiwa nafasi ya Makamo wa Kwanza wa Rais baada ya uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020. Mtu wa kushika nafasi hiyo ya Makamo wa Kwanza wa Rais hata hivyo anatakiwa awe ni atakaekwenda sambamba na matakwa ya CCM na serikali zake. Abbas Muhunzi ambae yupo chini ya uungwaji mkono mkubwa wa Faki Suleman anaonekana hakubaliki katika upande wa CCM na serikali. Hivyo mkakati wa kuwaondoa mmoja mmoja katika nafasi za uongozi ndio ulioonekana nia pekee na nzuri ya kuweza kufanikisha kuwaondosha katika azma yao hiyo.
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
5,893
2,000
Get rich or die trying, fighting to the last man, politics is the game of death, hakunaga kuhurumiana huko....ukilemba unapasuliwa kama kawa
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,732
2,000
Lipumba ataanza kupata njaa baada ya uchaguzi wa 2020, kwasasa badoanapata Ruzuku za wabunge wa CUF.
CUF hawatapata mbunge hata mmoja, hapo ataungana na akina Dovutwa rasmi.
 

battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,044
2,000
CUF imesha kufa, Waislam wote sasa tunakutana kwa Kabwe, ACT Wazalendo
Alaa! kumbe waliobakia CUF si wislamu,au sio? Au Cuf yenyewe si chama cha kiislamu tena kama kilivyokuwa zamani?
:rolleyes: Lakini MHUUUUUU,
Nyie CCM hamuchoki fitina ,muna kazi kwei kweli,Hata Mbele za Mungu sijuwi mutajificha wafi kwa kufitinisha watanzania wenzenu ili nyie mubaki madarakani.
Kuna Maisha badala ya kufa ?Tahadharini?
Bakwata Tayari wanaanza kujitambua,nyie bado tuu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom