CUF ya Lipumba yasema itashiriki Uchaguzi Mdogo wa Agosti 12


Queen V

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2012
Messages
613
Likes
801
Points
180

Queen V

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2012
613 801 180
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya ambaye ytuko upande wa Profesa Lipumba amesema chama hicho kitashiriki uchaguzi wa ubunge katika majimbo ya Buyungu, Jangombe na kwenye Kata 79.

Akizungumza jana Sakaya alisema chama hicho kimepokea barua kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kikielezwa kuwa majimbo na kata hizo, yapo wazi.

Alisema kutokana na mabadiliko yaliyofanyika NEC na katika vyombo vya Dola ni wazi kuwa wataibuka na ushindi katika chaguzi hizo

“Naomba ifahamike kuwa CUF ipo moja na uamuzi wa chama ni kushiriki uchaguzi, wanachama wasisikilize maneno ya watu ambao hawahusiki na chama," alisema Sakaya.

Alisema wapo wanaojitambulisha kuwa viongozi wa CUF wanasema hawatoshiriki, si kweli wamachama na wenye nia ya kutaka kugombea ubunge na udiwani wajitokeze.

"Uchaguzi wa ubunge jimbo la Kinondoni tulilalamikia utaratibu ulivyokuwa na namna NEC walivyokiuka. Ila kw amabadiliko yaliyofanyika sasa, naamini hali itakuwa nzuri,” alisema Sakaya.

Pia nae Profesa Ibrahim Lipumba amewataka wanachama kuzipuuza habari kuwa wamesusia kushiriki chaguzi hizo.

Chanzo: Mpekuzi
 

Forum statistics

Threads 1,203,731
Members 456,939
Posts 28,126,749