CUF watishia kujitoa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF watishia kujitoa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 6, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  CUF watishia kujitoa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa


  [​IMG]
  Tume ya Uchaguzi, (NEC).  Chama cha CUF kimetishia kujiondoa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Temeke, endapo Tume ya Uchaguzi, (NEC) haitapunguza idadi ya vituo vya uandikishaji wa wapiga kura.
  Akiongea na gazeti hili, Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi Taifa, Bw. Shaweji Mketo amesema wingi wa vituo hivyo unawatia hofu.
  ``Huu wingi wa vituo una harufu ya mchezo mbaya wa kuingiza wapiga kura hewa,’’ akadai.
  Amesema anashangazwa na kitendo cha Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Temeke Bw. Stephen Kongwa kuweka vituo 10 na zaidi kwa kila mtaa wakati wilaya za Kinondoni na Ilala zimeweka utaratibu wa zamani wa kila mtaa kuwa na kituo kimoja au viwili pekee.
  "Hili jambo hatuwezi kulivumilia, kuna mchezo mchafu wanaotaka kufanya ili kuongeza wapiga kura na kama hawajaliangalia hili, tutaweka pingamizi na kujiondoa kwenye uchaguzi," akasema Bw. Mketo.
  Akitoa mfano, ameeleza kuwa kuna mtaa mmoja eneo la Charambe ambao una vituo 22 vya uandikishaji wa daftari la wapiga kura.
  "Kabla hatujachukua jukumu hilo, tutakwenda kuonana na mwanasheria wa Temeke ili atueleze kwa nini wamechukua hatua kama hii," akaongeza kusema.
  Akizungumzia suala hilo, Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya hiyo, Bw. Kongwa amesema uamuzi wa kuweka vituo vingi vya uandikishaji wa wapiga kura umetokana na waraka wa Serikali unaoelekeza kila kituo kiwe na watu wa kuandikisha wasiopungua 500 pekee.
  Amesema kutokana na mitaa mingi ndani ya eneo hilo kuwa na wakazi wengi, mitaa mingi imekuwa na vituo kuanzia sita na zaidi ili kukidhi idadi inayotakiwa.
  "Sisi tunafanya kazi kwa mujibu wa taratibu tulizowekewa, hatukurupuki, Wizara imetupa muongozo na ndio tunaoufuata, hatuwezi kudhulumu haki ya mtu," akasema Bw. Kongwa.
  Ameongeza kuwa utaratibu wa kuandikisha wapiga kura utaanza kama ulivyopangwa na akaomba vyama vyote kuhakikisha vinahamasisha watu wasiokuwa na vitambulisho vya kupigia kura kwenda kujiandikisha.
  "Hatuwezi kuingiza watu wa kupiga kura kama walivyosema, tunachoomba ni vyama vyote kuhakikisha vinahamasisha watu waende kujiandikisha," akasema.  CHANZO: ALASIRI

  http://www.ippmedia.com/
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kwanini maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa TAMISEMI hawawashirikishi vyama vya siasa ili kama kweli miongozo hii inatolewa,kusionekane haja ya kutokea hitilafu kama hizi.
   
Loading...