CUF wanacheza na wanachama wao?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,191
673
Pale mazungumzo yalipokwama viongozi wa cuf walikimbilia mbio kwa wafuasi wao na kuwaomba radhi kwa kuwaficha kinachoendelea juu ya mzungumzo hayo.

Lakini sasa yanaendelea wamewatupa kule, wakiulizwa majibu ndio kamahayo. hivi wanacheza nao jee wanaahadi ya kuwadanganya kama watoto wa kuku hadi lini?

Hii ndio sura ya upinzani ilivyo, jee wakipata serikali wataweza kutekeleza ahadi gani hawa ikiwa hii ndogo tu hata miezi 6 haijafika imeshawashinda?


Maalim Seif atetea usiri vikao vya muafaka CCM,CUF
Na Muhibu Said

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, ametetea mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar kati ya chama chake na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuwa ya siri.

Alitoa kauli hiyo alipoulizwa na waandishi wa habari Makao Makuu ya CUF, jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mapendekezo ya chama hicho yaliyofikiwa katika vikao vyake vilivyofanyika Agosti, mwaka huu, kutaka mazungumzo hayo yasiendelee kuwa ya siri na kuazimia kuyafikisha mapendekezo hayo kwa wenzao wa CCM kabla ya utekelezaji.

Akijibu swali hilo, Maalim Seif alisema jambo hilo haliwezekani kwa kuwa duniani kote hakuna mazungumzo yanayokuwa ya wazi.

"Tumekubaliana (na CCM) tuchukue hatua ya kuupatia (mpasuko wa kisiasa Zanzibar) ufumbuzi. Ukiniuliza lipi linazungumzwa, utakuwa unanionea. Hakuna duniani mazungumzo ya aina hiyo. Tuachieni wachezaji tucheze mpaka mwisho," alisema Maalim Seif.

Maalim Seif pia hakuwa tayari kueleza tarehe ambayo wamekubaliana na wenzao wa CCM ya kwisha kwa mazungumzo hayo badala yake aliomba wapewe muda na kusema kuwa karibuni mazungumzo hayo yatafikia tamati.

Hivi karibuni, mjumbe wa kamati ya mazungumzo hayo kutoka CUF, Hamad Rashid Mohamed, alikaririwa na gazeti hili akisema kuwa katika moja ya vikao hivyo, walikubaliana mazungumzo hayo yasiendelee kuwa ya siri kama ilivyokuwa awali na kuahidi kuufikisha msimamo wao huo kwa wenzao wa CCM ili waujadili kabla ya kutekelezwa.

Majibu hayo ya Maalim Seif kwa waandishi wa habari, yalitanguliwa na maazimio 22 yaliyofikiwa na kikao cha Baraza la Uongozi Taifa, kilichofanyika katika ofisi kuu ya CUF, Oktoba 23-26, mwaka huu, yaliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mahusiano na Umma wa CUF, Mbaralah Maharagande, makao makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam jana.

Akisoma maazimio hayo, Maharagande alisema Baraza Kuu linahimiza kuongezwa kwa kasi ya mazungumzo ili yakamilishwe mapema na kutoa muda wa kutosha wa kutekeleza yatakayokubaliwa na vyama vyao katika mazungumzo hayo na pia kuisafisha nchi na doa linalosababishwa na mgogoro wa kisiasa visiwani humo uliodumu kwa muda mrefu sasa.

Alisema Baraza Kuu linawapongeza Maalim Seif na wajumbe wote wa timu ya mazungumzo ya CUF kwa mchango wao mkubwa unaolenga kufanikisha mazungumzo hayo na pia linawapongeza wajumbe wa timu ya CCM kwa mashirikiano yao katika kufanikisha lengo hilo.

Mazungumzo hayo yaliyoanza Zanzibar Januari 17, mwaka huu, yalikwama baadaye baada ya makatibu wakuu wa vyama hivyo, Seif Shariff Hamad (CUF) na Makamba (CCM), kukubaliana kwa maandishi kwamba, ifikapo Agosti 15, yawe yamekwisha.

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=2561
 
Back
Top Bottom