CUF wana uroho wa madaraka

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
2,000
Jamani kwa muda wote nimekuwa nafuatilia hizi kelele za kambi ya Upinzani na hasa lawama kwa Chadema kuunda umoja wa pekee yao na kuacha CUF na TLP nk .Bora hapa UDP wangalisema lakini vyama saliti kama CUF ambao hata kwenye kampeni wakionyesha chuki za wazi kabisa kwa Chadema na Mrema na live agent wa CCM how do you deal with them when you want to get serious na maisha ya watanzania ?

Rashid anasumbuliwa na madaraka kwani hawezi kukaa Bungeni bila ya kuwa kiongozi wa Upinzani na bado akawa Mbunge wa huko alikotoka ? Nadhani kuna kutumiana na kuvurugana hapa nawashauri Chadema kuendelea na misimamo yao badala ya kuanza kuyumbishwa na hawa wapenda madaraka na wasiojua wanacho kitaka .Yaani wao Seif kuwa makamu wa rais kumewamaliza wote na mwisho wa CUF ni huo ama watakuja timuana kwa mashoka na kuweka CUF ya maana maana muungano wao ni mtego tu huu .Narudia CUF na TLP na NCCR unawezaje kuwaamini hawa ?
 

Mapinduzi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
2,424
0
Lunyungu habari za kupotea.

Kwa mtazamo wangu, nadhani wenye uchu wa madaraka ni CHADEMA. Wanatafuta sympathy ya wananchi ili waonekane wao ndio wenye kujua kuongoza hii nchi na ndio watakaoiletea hii nchi maendeleo. Ukifanya critical analysis unaona kuwa chadema bado ni chama kichanga sana kuendesha nchi (Niambieni kama nao wanataka serikali ya umoja wa kitaifa, serikali mseto). Vinginevyo hawana kabisa elements za kuongoza nchi kwa sasa. Kwa nini nasema hivi? Ukiangalia sera zao ni sera mbadala ambazo kiukweli hawajaainisha ni jinsi gani watazitekeleza. they are just wishful thoughts, their ambitions.

Call me any name lakini ukweli utabaki kuwa CHADEMA aka cha-chali ndio wenye uchu wa madaraka. Wanataka watawale hii by hooks and crooks. Mshindani wa kweli anakubali kushindwa, anajipanga upya kwa mpambano ujao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom