CUF wamtaka Diwani wao asiambatane na Salum Mwalimu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,185
103,688
CUF yamtaka Diwani wao kuacha kuandamana na mgombea wa Chadema

Katibu wa CUF Ally Mkandu amemtaka Diwani wa kata ya mzimuni Ally Kondo kuacha kuongozana na mgombea wa Chadema Salum Mwalimu.

Amesema kwamba diwani huo asipoacha kuongozana na mgombea huyo chama kitamchukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kutumia katiba kumvua uanachama.

Mkurugenzi wa Habari na uenezi Abduli Kambaya amewaambia wakazi wa mzimuni kwamba mwaka 2015 CUF ilipata ushindi kwa kufanya kazi kubwa kwenye kata ya mzimuni.

‘’Leo anajitokeza mtu anawashawishi mumchague mgombea mwingine inauma sana’’amesema Kambaya

Naye mgombea Rajabu Salum amesema kwamba ‘’Mimi nilikuwa meneja kampeni wa mgombea wa huyu aliyehamia CCM( Maulid Mtulia) hivyo mimi nilikuwa mwalimu wake’’

Amesema mgombea huyo sasa ameanza kutumia sera za Cuf kwenye majukwaa.

‘’CCM na Chadema wameahidi kunipa kura kwa kuwa wagombea wao hawakushiriki kwenye kura za maoni ‘’amesema Salum
 
acha wafu wawazike wafu wenzao
 
Back
Top Bottom