CUF wamekuwa wakipokea mabiliomi ya ruzuku, zinaenda wapi?

Paddy

JF-Expert Member
Sep 22, 2010
462
304
CHADEMA Bara, CUF Zanzibar, kipi kitatufaa?

WATANZANIA wenzangu, nianze kwa kuhitimisha tathmini yangu juu ya CUF, nikizingatia kigezo cha nne, cha utafutaji/utumiaji wa rasilimali kwa ajili ya kugharamia harakati za kisiasa.

Kama nilivyowahi kugusia wiki zilizopita, utafutaji na utumiaji wa rasilimali za kufanikisha shughuli za kisiasa, ndiyo kigezo cha mwisho cha kupima ubora wa chama, kikitanguliwa na vigezo vingine vitatu; haiba ya chama, ajenda ya chama, na oganaizesheni au mtandao wa chama husika.

Katika vigezo hivyo vitatu, CUF imeonekana kuwa dhaifu mno katika haiba yake, dhaifu kiasi katika ajenda yake na yenye nguvu kiasi katika mtandao wake (oganaizesheni). Sasa tumalizie tathmini yetu kwa kigezo cha mwisho, je, ni kwa kiasi gani CUF imekuwa ikitafuta na kutumia vizuri pesa au rasilimali za kufanikisha harakati za kisiasa?

Vyama vya siasa nchini vimekuwa vikijipatia mapato yake kupitia ruzuku inayotolewa na serikali kupitia ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, na michango ya wanachama na wafadhili wake wa ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo, uzoefu unaonyesha kuwa ndani ya vyama vyote vya upinzani ni idadi ndogo tu ya wanachama ndiyo imekuwa ikichangia vyama vyao, na michango inayotolewa imekuwa si ya kukiwezesha chama husika kukidhi mahitaji yake ya kisiasa.

Hali hiyo imevifanya vyama vingi kutegemea zaidi ruzuku na michango ya wafadhili wa ndani na nje, na uwezo wa chama husika kutafuta wafadhili hao.

Suala la wafadhili na kiasi cha fedha wanazotoa, limekuwa ni siri kubwa ndani ya vyama vya siasa nchini. Pamoja na siri hiyo, mazingira yanaonyesha kuwa CUF imekuwa ikipata na kutegemea zaidi ruzuku kuliko fedha zinazotokana na wafadhili au michango ya wanachama wake. Hakuna ubishi kuwa CUF ndicho chama ambacho kimekuwa kikipokea kiasi kikubwa cha ruzuku kuliko vyama vingine vya upinzani.

Sehemu ya barua ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, yenye kumbukumbu namba BA.124/138/01A/39, ya Februari 19, mwaka huu, kwenda kwa Profesa Abdallah Safari, inabainisha ruzuku ya CUF kama ifuatavyo:

Kwa mujibu wa barua hiyo, CUF imekuwa ikipokea ruzuku ya serikali kwa kipindi cha kuanzia 1995 hadi 2008 kama ifuatavyo:

Ilipokea ruzuku ya sh 91,000,000 katika mwaka wa fedha wa 1995/1996, sh 91,000,000 (1996/1997), 246,000,000 (1997/98), 196,800,000 (1998/99), na sh 334, 704, 000 katika mwaka wa fedha 1999/00.

Ilipokea pia sh 210,544,192.80 katika mwaka wa fedha 2000/01, sh 266, 322,000 (2001/02), sh 567, 522,000 (2002/03), sh 829, 623, 108.10 (2003/04), sh 1, 873, 877, 431.56 (2004/05), sh 1, 022, 555, 543.20 (2005/06), sh 1, 537, 989, 900.00 (2006/07), na sh 2, 610, 144, 692.00 katika mwaka wa fedha wa 2007/08.

Izingatiwe kuwa fedha hizo ni nje ya mishahara ya wabunge na wawakilishi wake. Ikiwa ndani ya CUF kuna utaratibu wa wabunge na wawakilishi wake kukichangia chama chao kila mwezi, basi ni dhahiri kinapata fedha nyingi zaidi ya hizo nilizoainisha hapo juu.

Aidha, chama hicho kinapata fedha nyingi sana ikiwa pia zitajumlishwa fedha nyingine inazozipata kutokana na michango ya wafadhili na wanachama wake wa kawaida. Kwa mantiki hiyo, upataji wa fedha si tatizo la msingi ndani ya CUF, kwani chama hicho kinaonekana kupata fedha nyingi kuliko chama chochote cha upinzani nchini. Je, CUF imekuwa ikizitumiaje fedha zake hizo? Tulijadili hili kwa pamoja.

Si rahisi sana kujua ni jinsi gani CUF imekuwa ikitumia fedha zake. Hata hivyo, tukizingatia shughuli za kisiasa zinazopaswa kuonekana machoni mwa jamii ambayo ndiyo inayolengwa (kushawishiwa), ni dhahiri kuwa chama hicho kimekuwa kikielekeza fedha nyingi upande wa Zanzibar kuliko vile inavyostahili. Upande wa Bara ambako ni kukubwa, CUF imeonekana kutotumia fedha nyingi katika kufanya shughuli zake za kisiasa kama inavyostahili.

Mathalani, kampeni za CUF katika uchaguzi mdogo wa Busanda zilionekana kuwa na uchache wa vifaa vya kampeni. Magari na idadi ya watendaji/wanasiasa vilikuwa kidogo sana kulinganisha na mahitaji, hali iliyoonyesha dhahiri kuwa chama hicho hakikuwekeza fedha nyingi katika uchaguzi huo.

Kwa chaguzi na matukio ya kisiasa yanayofanyika Zanzibar kama maandamano, CUF imeonekana kutumia gharama kubwa, tena za mara kwa mara pengine kuzidi ukubwa wa kisiwa hicho au maeneo husika, ikilinganishwa na kile inachokifanya Tanzania Bara ambako ndiko kukubwa.

Hali hiyo inatoa picha kuwa fedha za chama hicho zimekuwa zikitumiwa bila kuwa na programu au mkakati wenye vipaumbele vizuri vya matumizi ya fedha kisiasa.

Kutokuwa na mkakati mzuri wenye vipaumbele sahihi vya matumizi ya mapato yake, nako kunaweza kuwa kumechangia kukifanya chama hicho kuwa na nguvu katika eneo dogo tu la nchi (Zanzibar), na kudorora katika eneo kubwa la nchi (Tanzania Bara).

Chama kinachowekeza sehemu kubwa ya fedha kufanya siasa katika eneo dogo tu la nchi, hupoteza sifa ya kuwa chama cha kitaifa. Vivyo hivyo, uwekezaji mdogo wa fedha katika eneo kubwa la nchi (lenye wapiga kura wengi), hukifanya chama husika kuwa mbali kabisa na ndoto ya kuwa chama mbadala, kwani ni vigumu kwa chama hicho kuchukua dola.

Sasa tuanze kuitathmini CHADEMA tukizingatia vigezo vilevile tulivyotumia kuijadili CUF. Nimetumia zaidi ya wiki tano kuitathmini CUF kwa sababu wakati huo huo nilikuwa nikifanya kazi nyingine ya kuvifafanua vigezo nilivyovitumia.

Kwa kuwa vigezo hivyo nimekwisha kuvifafanua, sasa naitathmini CHADEMA kwa kuilinganisha na CUF kama ifuatavyo:

Wakati CUF imeonekana kuporomoka katika kigezo cha kwanza cha haiba, haiba ya CHADEMA imekuwa nzuri na kukua kwa kasi kubwa tangu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2005 hadi sasa.

Kwa haiba yake, CHADEMA imeweza kujitambulisha kama chama cha kisomi au kinachotumia mikakati ya ubunifu wa hali ya juu na nyenzo za kisayansi katika kufanya harakati zake za kisiasa.

Matumizi ya helikopta, salamu ya ‘People's Power' (Nguvu ya Umma) na vazi la kombati linalotumiwa na baadhi ya viongozi wake hususan mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, ni sehemu ya mambo yaliyochangia kuijenga haiba ya CHADEMA na kukifanya kionekane kama chama kipya na chenye mvuto kwa jamii ya leo, licha ya kuwapo tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza nchini.

Umahiri wa kisiasa wa viongozi wake wa kitaifa, hasa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Willbrod Slaa, na Naibu wake Bara, Zitto Kabwe, wa kuhutubia vizuri na kujenga hoja juu ya masuala mbalimbali kuhusu yanayohusu nchi na wananchi, pia vimechangia sana kujenga, kudumisha na kukuza haiba na umaarufu wa CHADEMA.

CHADEMA imeweza kujipambanua kama chama cha kizazi kipya, kikisifika kwa kuvutia vijana wengi hasa wasomi kutoka vyuo vikuu. Baadhi ya vijana hao hivi sasa ni sehemu ya viongozi wakuu wa chama hicho, huku wengine wakiwa tayari ni wabunge wanaovuma ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zitto Kabwe, Halima Mdee, Mhonga Said Ruhanywa, John Mnyika, John Mrema, John Heche, Msafiri Mtemelwa na wengineo wengi ni baadhi tu ya vijana wa CHADEMA wanaoonekana kuwa sehemu ya injini inayokiendesha chama hicho na kukijengea haiba ya kusifika mbele ya wananchi, hususan kwa vijana ambao ndio wanafanya idadi kubwa ya wapiga kura wote nchini.

Kwa haiba yake hiyo, CHADEMA imeweza kupata mafanikio makubwa kisiasa, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wabunge wake kwa zaidi ya asilimia 100 katika uchaguzi wa 2005 ikilinganishwa na wale iliokuwa nao miaka iliyopita.

Imeweza kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge Tarime, na kutoa ushindani mkali dhidi ya CCM katika chaguzi ndogo za Kiteto, Busanda na Biharamulo.

Imeshinda pia chaguzi ndogo kadhaa za udiwani zilizofanyika maeneo mbalimbali nchini, baada ya mwaka 2005, zikiwamo zile za Kiteto na Tarime Mjini.

Leo CHADEMA ndicho chama pekee cha upinzani kilichoweza kuongoza halmashauri tatu, ambazo ni Karatu, Tarime na Kigoma Ujiji (kwa kupokezana na CCM). Kimeshikilia halmashauri hizo baada ya kupata wabunge na madiwani wengi kwenye majimbo hayo katika uchaguzi uliopita.

Kwa haiba yake hiyo, CHADEMA imeweza kuvutia mamia na maelfu ya wanachama wapya hata baada ya uchaguzi mkuu wa 2005, huku ikikadiriwa kuwa na mashabiki wengi Tanzania Bara kuliko chama chochote cha upinzani hivi sasa.

Miongoni mwa waliovutiwa kujiunga na CHADEMA wamo viongozi na makada waandamizi kutoka vyama vingine vya upinzani, akiwamo Wilfred Lwakatare aliyekuwa CUF na Joseph Selasini aliyejiunga jana akitokea NCCR-Mageuzi.

Hata hivyo, licha ya chama hicho kuwa na mvuto unaokifanya kivutie wengi, bado kinakabiliwa na changamoto kubwa ya kutuhumiwa kuwa chama cha kikabila (Uchaga).

Tuhuma hizo hata hivyo zimekuwa ni propaganda tu zinazofanywa na wapinzani wake, hasa CCM, kama ilivyoifanyia CUF kwa kuituhumu kwa udini na Uzanzibari. Tofauti na CUF, CHADEMA haijaonekana kuathiriwa sana na propaganda zinazoelekezwa dhidi yake. Lakini kutoathiriwa huko kutategemea tu ni jinsi gani chama hicho kitaendelea kukabiliana na propaganda hizo.

Kwa sasa CHADEMA inaonekana kufanikiwa katika kuelimisha Watanzania kupuuza propaganda hiyo ya ukabila, kwa kuimarisha harakati zake za kuwapigania wananchi dhidi ya ufisadi unaoendelea nchini.

Matokeo yake, idadi ya Watanzania wanaoelewa kuwa CCM ni chama cha mafisadi inaongezeka kwa kasi kubwa kila kukicha, kuliko idadi ya wale wanaorubuniwa kuwa CHADEMA ni chama cha kikabila.

Kama ambavyo siamini kuwa CUF ni chama cha kidini (Kiislamu), pia siamini kuwa CHADEMA ni chama cha kikabila kama inavyodaiwa na baadhi ya makada na viongozi wachache wa CCM.

Wanaoihusisha CHADEMA na ukabila wanafanya hivyo kwa kuelekeza mashambulizi dhidi ya kabila la mwenyekiti wa chama hicho (Mchaga), huku wakifumba macho kwa makusudi, kuhusu uwepo wa viongozi wengi ndani ya chama hicho ambao si Wachaga.

Itiliwe maanani kuwa CHADEMA imeweza kuenea, kupata ushindi, na kuonyesha ushindani mkali katika mikoa mbalimbali nchini mbali na mkoa wa Kilimanjaro anakotokea mwenyekiti wake.

CHADEMA inatamba Kigoma Mjini, Kigoma Kaskazini, Mpanda Kati (Rukwa), Karatu (Arusha), Tarime (Mara), Mbeya Vijijini, Biharamulo (Kagera), Busanda (Mwanza), na maeneo mengine mengi ya nchi.

Izingatiwe kuwa CHADEMA ndicho chama cha upinzani chenye idadi kubwa ya madiwani (zaidi ya madiwani 101), kuliko chama chochote kile cha upinzani. Madiwani wote hao wamepatikana katika kata zaidi ya 101 zilizo ndani ya mikoa na wilaya mbalimbali nchini kote, ushahidi unaoifanya hoja ya CHADEMA kuwa chama cha Kichaga kuwa ya uongo au propaganda tu, inayofanywa na wapinzani wake ili kukichafua.

Source: Tanzania Daima 26/8/2009

My take: Kwa hizo ruzuku, CUF ingekua na majengo ya ofisi makubwa, TV, RADIO, etc. Hamna Harufu ya ufisadi hapa? Hela zinaenda wapi? WanaJF tujadili hili
 
Ilitosha sana kuandika issue za CUF negatively na usingeweka kabisa za CCM au Chadema, tungejadili CUF deeply na sasa umeweka room ya CDM kukiponda cuf hapa kwa sababu CDM na CUF wan beef! na JF wengi ni cdm! ukiwamo wewe! na nadhani ndio basis ya maoni yako. KAMA umeweza kupata za CUF unazo pia za CDM?? kama zipo ebu zi-post ili kuwa na fair ground hapa! maana kumbuka CDM mikoani walilalamika kuhusu ruzuku na Chacha wange (makamu mwenyekiti wa CDM alilalamika pia!!!!!)

Kwa kifupi ni hivi, hakuna na bado hamna wapinzani wa wewe kuwaamini, naweza kuwa nawaonea CUF ila ukweli ni kuwa wapinzani wetu woote matumbo mbele na they are serious in making profits at any cost even if they need to deceive majority they will do that!

CUF-Zanzibar mikono juu! nawaheshimu wako mbali na wamefikia hapo baada ya misukosuko mingi, kulikuwa hakuendeki kule!! walishawahi kugomea bunge miaka 3 with no posho, kitu ambacho CDM hawataweza hata aje mtume gani!

CUF-Bara, CDM(chadema), TLP, nccr, CCM ni walewale wanaotumia ujinga wa watanzania kufanikisha malengo yao ya muda mfupi (chooni) na muda mrefu (investmment).

Fuatilia chadem you will find the shocking news, waulize kama wana statement ya mwaka jana! sign zote anapiga Mbowe! hivi uko wapi wewe??

Hupo??
 
Waberoya... I am shocked!!!

I always look to you as one of a few neutral and analytical qualities of JF when it comes to political matters, i do also expect some moderation and parity in your post

In this one i see you are trying to say two wrongs ni poa, kama huyu kachemsha basi mbona na wewe unachemsha.. sort of; too low kwa mtu kama wewe

Not sure if this is one of your worst posts but to me it is...

Sorry about that
 
@Paddy... tupe basi abstract maana umechapisha kama mhariri wa gazeti la habari leo:embarrassed:
 
nyingi zililipia gharama za hotel alikokaa mwenye chama na safari zake za nje!!!!. Hakika 40% ya fedha zote zilikuwa zinatumia na Mtukufu Mheshimiwa sana Makamu wa kwanza wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyo pia Serikali ya Umoja wa Kitaifa Sheikh Maalim Seif Hamad. Huyu ndiye katibu Mkuu Mtendaji asiyeulizwa chochote na Yeye ndiye mmiliki wa chama ati!
 
Waberoya... I am shocked!!!

I always look to you as one of a few neutral and analytical qualities of JF when it comes to political matters, i do also expect some moderation and parity in your post

In this one i see you are trying to say two wrongs ni poa, kama huyu kachemsha basi mbona na wewe unachemsha.. sort of; too low kwa mtu kama wewe

Not sure if this is one of your worst posts but to me it is...

Sorry about that

Mkuu Acid ndio maana wengine tumeamua kukaa kimya
 
Waberoya... I am shocked!!!

I always look to you as one of a few neutral and analytical qualities of JF when it comes to political matters, i do also expect some moderation and parity in your post

In this one i see you are trying to say two wrongs ni poa, kama huyu kachemsha basi mbona na wewe unachemsha.. sort of; too low kwa mtu kama wewe

Not sure if this is one of your worst posts but to me it is...

Sorry about that

Asante kwa kunipa ujiko japo sipendelei sana.

Wewe umeelewa hiyo article, lengo la mwandishi ni nini? what is his hidden agenda?? be fair

Yuko inclined CDM na ninamueleza hata wao asiwaamini maana hanajweka data ya wao kuwaamini, wala hizo data za CUF hajaziweka hili kujua zinafanya nini!

Nikkigusa CDM tu kosa, mbona CUF -bara hawalalamiki? nimesema wote wezi I mean CDM ,CUF-bara ( ambao majuzi wameviondoa vyeo vya wakurugenzi) wote wezi, sasa siko humu kupata commend yako au la! you can simply put me in your ignored list,

muanzisha maada kachanganya mambo, angalia title, angweka kitu kimoja kingekuwa vizuri we were supposed to discuss CUF na fedha zao, pengine tungewatafuta waje hapa kujibu tuhuma hizi.

Hiyo ya kuwa two wrongs ni poa umeisema wewe na umeielewa ww mimi siko huko, wala sikuandika nikiwa na mawazo hayo. Misimamo yangu tangu awali hata kabla ya kujua CUF fedha zao zikoje niliishasema na ninastand hapo kuwa vyama hivi ni wezi!! sikutaka kujua habari za Cuf wala nani wote wezi tu!
 
ni kweli kabisa waberoya... ila two wrongs wont make it right na ndicho nilichosema

si kwamba akiegemea huku basi na wewe lazima uegemee kule...

au nimekosea?
 
ni kweli kabisa waberoya... ila two wrongs wont make it right na ndicho nilichosema

si kwamba akiegemea huku basi na wewe lazima uegemee kule...

au nimekosea?

Ndio umekosea..ulitaka aseme CDM ndio wasafi tuuu ila hau KAFU ndio wachafu.
 
Ulichosema kuhusu Chadema kinaweza kuwa sahihi kwa namna fulani. Lakini mimi naamini "ukombozi wa Tanzania utaletwa na Chadema". Mwanzo mgumu ila kadiri chama kinavyokomaa ndipo baadhi ya mapungufu hupungua ama kupotea kabisa. Naamini Chadema wanaweza pia wakawa weak kwenye ishu ya ruzuku lakini they are far better than CUF. Hela za kampeni wanazotumia Chadema ni nyingi sana, wanazitoa wapi? Umejiuliza hili pia?
 
Back
Top Bottom