CUF wamchokoza JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF wamchokoza JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sokomoko, Oct 20, 2008.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  CUF wamchokoza JK

  na Mwanne Mashugu, Zanzibar


  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimesema suala la mafuta na gesi asilia si la Muungano na kumtaka Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Abeid Karume, kuanzisha wizara maalumu ya mafuta na gesi asilia.

  Kauli hiyo ya CUF imetolewa jana visiwani Zanzibar na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Kibanda Maiti.

  Mbali na kumtaka Karume kuunda wizara hiyo, pia wametaka kuwepo kwa Shirika la Maendeleo ya Mafuta Zanzibar, ili liweze kutoa vibali vya uchimbaji wa mafuta na gesi katika vitalu namba 9, 10, 11 na 12 vilivyopo katika ukanda wa bahari kuu ya visiwa vya Unguja na Pemba .

  Maalim Seif, ameilaumu Serikali ya Muungano kwa kijinufaisha peke yake katika suala hilo, kwa kisingizio kuwa Zanzibar haiwezi kuchimba gesi na mafuta kwa kuwa suala hilo ni la muungano.

  Alisema Serikali ya Muungano imemzuia mwekezaji kutoka nchi za Falme za Kiarabu kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta kwa kisingizio cha kuchafua mazingira.

  Alisema badala yake viongozi wa Serikali ya Muungano walimshawishi mwekezaji huyo kujenga Tanzania Bara, kwa madai kuwa hakiwezi kuchafua mazingira ya Bara, kwa kuwa kuna eneo kubwa.

  Maalim Seif, alisema baada ya vikwazo hivyo aliwasiliana na wawekezaji hao ambao walisema bado wana nia ya kuwekeza lakini sasa watalazimika kupitia Serikali ya Muungano.

  Alisema aliwaambia wawekezaji hao kuwa Wazanzibari wataupinga kwa nguvu zote uwekezaji wa kupitia muungano ila watauunga mkono uwekezaji kupitia Serikali ya Zanzibar.

  Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imenyimwa fursa ya kujiendeleza kiuchumi pamoja na vijana wengi wa Zanzibar kupata ajira.

  “Huu ni mkakati wa Serikali ya Muungano kuhakikisha kuwa suala la mafuta na gesi asilia linaendelea kuwa la muungano,” alisema katibu mkuu huyo.

  Katibu mkuu huyo, alisema anayo taarifa kuwa Serikali ya Muungano inaandaa muswada, ili sheria ya uundwaji wa Shirika la Maendeleo la Mafuta Tanzania (TPDC) irekebishwe, kwa lengo la kuliwezesha shirika hilo liwe na muungano na kufanya kazi hadi Zanzibar.

  “Mkakati huo umekuja baada ya kubainika kuwa Zanzibar kuna mafuta mengi hasa katika mwambao wa Zanzibar, ambako kumegundulika block 3 namba 9 hadi 12, ambazo zinaonyesha Zanzibar kuna mafuta, hasa katika mwambao wa Pemba.

  “Msimamo wa CUF ni kwamba suala la mafuta na gesi asilia ni mali ya Zanzibar… upo ushahidi wa kutosha mafuta na gesi asilia vimeingizwa kwenye muungano kwa ubabe, wakati huo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar alikuwa Abubakar Hamisi Bakari.

  “Baada ya suala hilo kupitishwa na Bunge, Abubakar alikwenda kulalamika kwa Nyerere (hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere), lakini hakuna lolote lililofanyika mpaka sasa,” alisema katibu mkuu huyo.

  Maalim Seif, alisisitiza kuwa ni busara suala la mafuta likabakia kuwa mali ya Zanzibar, kwa sababu Wazanzibari wengi hawapendi kuwa ya muungano, hivyo ni lazima kuepusha matatizo kama yale yanayotokea nchini Nigeria, ambapo kumekuwa na ugomvi wa mafuta.

  “Tumeona nchi nyingi zikiwemo nchi za Ghuba zilikuwa maskini, lakini baada ya kuchimbwa mafuta katika nchi zao, sasa wameweza kupata utajiri na kuondokana na umaskini … haya matatizo ya kulipia kodi naamini kwetu yataondoka ya kulipia watoto elimu, afya na huduma nyingine muhimu,” alisema.

  Alisema mbali na suala la mafuta, imegundulika kuwa Zanzibar ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na gesi nyingi, ikiongozwa na nchini ya Qatar.

  Aidha, alisema msimamo wa Wazanzibari hadi sasa ni kuwa bahari kuu yote na inayopakana nayo ni mali ya Zanzibar na rasilimali zake, ikiwa pamoja na kumiliki kilomita 50,000 kutoka ufukweni mwa bahari.

  “Eneo lote la mashariki ya Zanzibar ni eneo la Zanzibar, lakini Serikali ya Muungano inafanya jitihada ili masuala ya bahari yawe ya muungano,” alisema.

  Wakati huo huo, Maalim Seif, alisisitiza kuwa Zanzibar ni nchi, kwani ina sifa zote zinazotakiwa, ikiwa ni pamoja na kuwa na ukanda maalumu kiuchumi upatao kilomita 200.

  Katika mkutano huo, watu wengi walionekana kuvaa fulana zilizoandikwa ‘Zanzibar ni nchi’ na nyingine ‘mwisho wa ufisadi 2010’ na nyingine zilikuwa zikiendelea kuuzwa katika viwanja hivyo kwa bei ya sh 5,000.

  Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma, Salum Bimani, alisema Rais Kikwete ana deni kubwa Zanzibar, kwa kuwa hajatekeleza ahadi nyingi alizotoa wakati wa uchaguzi.

  Alisema wakati wa kampeni, Rais Kikwete aliahidi kuimarisha muungano na kutatua kero zilizomo, lakini mpaka sasa ameshindwa kufanya hivyo.

  Kuhusu mauaji ya maalbino yanayoendelea nchini, Bimani, aliwashauri wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwafichua watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

  Source: Tanzania Daima

   
 2. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Zanzibar mie naweza kusema hawana tena chao japo ukweli ni kuwa muungano ni wa nchi mbili. Ila majuzi nilipokuwa nasoma gazeti la mwanachi kwenye habari za mikoani nikakuta kuna habari za Zanzibar nikasema Yes atlist hawa Mwananchi wanajua somo kuwa Zanzibar ni mkoa tu!huo ni ukweli japo unauma sana kwa ndugu zetu wazenji ila hakuna wakuwatetea kwa hili ila wao wenywe they have to stand up and demand what they think is right for them.
   
 3. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tanzania bara kwanini tunawangangania hawa watu, wangeachwa tuone kama hayo mafuta yao watayapata au yataishia mikononi mwa viongozi wa CCM.
  Pemba bila muungano mtapata tabu sana kwani hawa jamaa wa CCM wako imara sana na wamejiandaa kuwanyanyasa shukuruni CCM bara inatuliza kidogo.
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  CCM: Maalim Seif si mkweli

  na Edward Kinabo

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kauli ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa CUF haiko tayari kurudi kwenye mazungumzo ya mwafaka kwa madai kuwa ulishakamilika na kinachosubiriwa ni saini ya viongozi hao, ni ya upotoshaji.

  Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Z. Chiligati, wakati akitoa tamko la chama hicho kuhusu hali ya kisiasa na kiusalama nchini, kwenye mkutano na waandishi habari uliofanyika kwenye ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM, jijini Dar es Salaam.

  Alisema CCM imesikitishwa na kauli hiyo ya CUF, kwani ina lengo la kupotosha umma.

  “Maalim Seif anaelewa kabisa kwamba hadi sasa hakuna makubaliano ya mwafaka yanayosubiri kutiwa saini na anajua vema kwamba kamati ya pamoja ambayo ina wajumbe wa CCM na CUF bado ina masuala ya kumalizia, ndipo maafikiano yapatikane, sasa hilo la kusubiriwa kwa saini, linatoka wapi?” alihoji, Chiligati.

  Alisema, wananchi wanapaswa kuelewa kwamba Kamati ya pamoja ilitoa mapendekezo ili kila chama kiyajadili na CCM ilipojadili, mapendekezo mengi ya CUF yalikubaliwa isipokuwa vipengele vichache ambavyo vilifanyiwa marekebisho na CCM iliongeza suala la kuweka utaratibu wa kuwashirikisha wananchi wa Zanzibar, ambalo halikuwemo katika mapendekezo ya CUF.

  Alisema CCM ilimtuma Katibu Mkuu wake, Yusufu Makamba, apeleke marekebisho hayo kwenye kamati ya pamoja na CUF ili yajadiliwe kwa lengo la kupata maafikiano lakini tatizo lililopo ni CUF kutotaka kurejea katika majadiliano.

  Alitoa wito kwa CUF warudi katika meza ya mazungumzo ambayo alidai wana uhakika maafikiano yatapatikana na kuzaa mwafaka utakaotiwa saini.

  Wiki iliyopita, Maalim Seif alinukuliwa akisema kuwa CUF imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, yenye kuarifu kwamba mazungumzo ya mwafaka yafufuliwe, na wao kujibu kwamba hawako tayari kufanya mazungumzo hayo kwani yamekamilika na kinachosubirwa ni uwekaji wa saini kwa pande zote mbili.
   
 5. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mfano halisi ni suala la Salim Ahmed Salim walivyompigia kampeni chafu wakisaidia na mtandao......
   
Loading...