Cuf walamba matapishi yao wenyewe!!!waja na itifaki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cuf walamba matapishi yao wenyewe!!!waja na itifaki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jan 13, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Chama cha Wananchi (CUF) kimewapiga marufuku mawaziri wake wanaounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutumia magari ya Serikali kwa shughuli za kisiasa za chama hicho kwa madhumuni ya kulinda misingi ya utawala bora.

  Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Ismail Jussa Ladhu, alisema uamuzi huo tayari umeshachukuliwa na chama baada ya kujitokeza baadhi ya mawaziri kutumia magari ya Serikali katika mikutano ya hadhara ya chama, kitendo ambacho kinakwenda kinyume na misingi ya utawala bora.
  Alisema tayari mawaziri wote wameshataarifiwa kuhusu uamuzi huo, na kuwataka watumie magari yao binafsi katika shughuli za kichama, na kwa wale wasiokuwa na magari watafute utaratibu mwingine utakaowawezesha kufika katika shughuli za kichama.


  Hata hivyo, alisema kwa upande wa Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alisema kwa mujibu wa itifaki, ni vigumu kutenganisha cheo chake anapokuwa katika shughuli za kiserikali na chama, hivyo ataendelea kutumia utaratibu wa sasa wa kushirikia shughuli za kichama kwa kutumia magari ya serikali kwa vile jambo hilo liko nje ya uwezo wa chama ambapo hakiwezi kuingilia masuala ya itifaki.

  “Ni kweli tulipokuwa wapinzani, tulikuwa tukipiga kelele kuhusiana na matumizi mabaya ya mali za umma ikiwemo magari ya serikali kutumika kwa shughuli za kichama, leo CUF ni sehemu ya Serikali, hatuwezi kwenda kinyume na misingi ya utawala bora, hilo tumeliona, lakini tayari tumeshawataarifu mawaziri na Naibu mawaziri wote kutotumia magari ya serikali katika shughuli za kichama,” alisema.


  Hata hivyo, Jussa alisema misingi ya utawala bora inahitaji kupewa nafasi kubwa hivi sasa hasa kwa kuzingatia kuwa CUF ni sehemu ya chama ambacho kimeshiriki katika kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
  Hivi karibuni baadhi ya magari ya Serikali yakiwemo ya mawaziri na naibu mawaziri yamekuwa yakitumika kupeleka watoto shuleni na vyuo vya madrasa pamoja na shughuli za nyumbani ikiwemo sokoni, maulidini na harusini, tofauti na makusudio yaliyopangiwa kutumika kwa shughuli za kikazi, jambo ambalo ni kinyume na misingi ya utawala bora.
  Kuhusu uvamizi wa maeneo ya wazi, Jussa alisema ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya watu wachache ambao ama kwa kutumia vyeo vyao au uwezo wa kifedha, wakivamia maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa shughuli za kijamii na michezo kujenga nyumba za makazi au biashara.
  Alisema maendeleo yoyote katika nchi yanapatikana ikiwa nchi itafuata utawala wa sheria, na kuunga mkono hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya awamu ya saba ya kufuta baadhi ya hati za ardhi zilizotolewa kinyume na sheria kuruhusu ujenzi katika maeneo yasiyokuwa katika mipango miji.
  Jussa ambaye ni mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, alisema hivi sasa kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa hifadhi ya mji huo kutokana na kuruhusiwa kujenga majengo yenye urefu wa ghorofa tano wakati sheria ya Mamlaka ya Mji Mkongwe imeweka ukomo wa ghorofa zisizozidi tatu.
  Alisema kwa mji huo umo katika hifadhi ya urithi chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), haiba na hadhi ya mji huo huenda ikapotea kutokana na ujenzi holela usiozingatia ramani ya mipango miji na kupoteza hadhi yake na kutoa mfano uwanja wa michezo wa Malindi ambao hivi sasa unaendelea na ujenzi wa maduka wakati eneo hilo ni mojawapo ya maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa shughuli za michezo na kijamii.
  Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, tayari ameshatoa uamuzi wa kufutwa kwa hati zaidi ya 26 na kuamuru kuvunjwa kwa majengo yaliyokuwa yameruhusiwa kinyume cha sheria katika maeneeo ya Mombasa kwa Mchina pamoja na Mazizini karibu na ofisi za Mufti wa Zanzibar, baada ya watendaji wa idara ya ardhi na upimaji kugawa viwanja katika eneo la wazi lililotengwa kama sehemu ya akiba ya barabara.
   
 2. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  wenye magari ni serikali.....hivyo anaetakiwa kuto amri hiyo ni serikali na siyo Cuf au Ladhu

  huo ndio utamu wa ndoa ya mkeka
   
 3. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huo ni mwanzo tumengi mengine yanakuja. Maalimu Seif kuwa makamu wa Rais ndio inazuia asipande gari alilokuwa akipanda kabla hajawa makamu wa Rais, CUF Jaman acheni uongo huo. Kama ni usalama, mbona alilindwa kabla hajawa makamu wa Rais kwani mtashindwa kumlinda sasa??? Ndio maana tunawaita CCM B.
   
Loading...